Javascript must be enabled to continue!
Nafasi ya Riwaya za Kingano za Kiswahili katika Harakati za Kupigania Hadhi-Msingi ya Mwanamke. Mfano Riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba
View through CrossRef
Makala haya yanalenga kuonesha namna riwaya za kingano za Kiswahili zinavyoweza kutumika kumpigania na kumkomboa mtu mnyonge hususani mwanamke na mtoto. Baadhi ya watu wanadhani ngano ni kwa ajili ya watoto kuburudika na kuwatia hofu kama njia ya kuwajengea adili. Ukweli ni kuwa, ngano ni zaidi ya burudani na hofu. Ndani ya ngano mna mambo mazito yanayoweza kumlea mtoto kwa kumuumba upya ili awe kiumbe kipya cha haki na usawa duniani bila hofu. Baadhi ya ngano zinaonekana kuvuka mipaka ya kitamaduni ya mafunzo anayostahili kupata mtoto. Mfano wa ngano hizo ni riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba inayomsawiri mwanamke kama kiumbe mwenye mapaji na uwezo mkubwa hata kumshinda mwanaume dhalimu. Mtazamo huu ni kinyume na mafunzo yanayopatikana katika ngano nyingi tulizonazo sokoni - kutokana na utiisho uliokita katika mfumodume. Makala yanabeba muhtasari wa uchunguzi uliongozwa na nadharia ya Ufeministi kuitalii riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008). Uchunguzi umebaini kuwa, mwandishi amemchora mwanamke kwa mtazamo chanya kwa kuonesha hadhi-msingi alizoumbiwa mwanamke mbali ya changamoto anazozipitia katika kujitetea. Ingawa mwanamke anaonekana kuendelea kukandamizwa na mfumodume, bado ukombozi wa kifikra unamfanya asikubali kuutii na kuuabudu. Katika mapambano haya, mwanamke amefanikiwa kuonesha hadhi-msingi zake tofauti tofauti zikiwemo: huruma na upendo kwa wanyonge, mpinga dhuluma, mjasiri, mwenye bidii, ubunifu, ujuzi, maarifa na nyenzo bora za kumwezesha kuhimili mikikimikiki ya mfumodume. Kwa picha hii, makala haya yatasaidia kuongeza matini za Kiswahili zilizoshughulikia mchango wa riwaya za kingano katika ukombozi wa mwanamke na mtoto. Vilevile, makala haya yatasaidia kuwaongoza wahakiki na watafiti wanaotarajia kuitalii riwaya ya Marimba ya Majaliwa au kazi nyingine ya kingano ili kumsawiri mwanamke.
East African Nature and Science Organization
Title: Nafasi ya Riwaya za Kingano za Kiswahili katika Harakati za Kupigania Hadhi-Msingi ya Mwanamke. Mfano Riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba
Description:
Makala haya yanalenga kuonesha namna riwaya za kingano za Kiswahili zinavyoweza kutumika kumpigania na kumkomboa mtu mnyonge hususani mwanamke na mtoto.
Baadhi ya watu wanadhani ngano ni kwa ajili ya watoto kuburudika na kuwatia hofu kama njia ya kuwajengea adili.
Ukweli ni kuwa, ngano ni zaidi ya burudani na hofu.
Ndani ya ngano mna mambo mazito yanayoweza kumlea mtoto kwa kumuumba upya ili awe kiumbe kipya cha haki na usawa duniani bila hofu.
Baadhi ya ngano zinaonekana kuvuka mipaka ya kitamaduni ya mafunzo anayostahili kupata mtoto.
Mfano wa ngano hizo ni riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba inayomsawiri mwanamke kama kiumbe mwenye mapaji na uwezo mkubwa hata kumshinda mwanaume dhalimu.
Mtazamo huu ni kinyume na mafunzo yanayopatikana katika ngano nyingi tulizonazo sokoni - kutokana na utiisho uliokita katika mfumodume.
Makala yanabeba muhtasari wa uchunguzi uliongozwa na nadharia ya Ufeministi kuitalii riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008).
Uchunguzi umebaini kuwa, mwandishi amemchora mwanamke kwa mtazamo chanya kwa kuonesha hadhi-msingi alizoumbiwa mwanamke mbali ya changamoto anazozipitia katika kujitetea.
Ingawa mwanamke anaonekana kuendelea kukandamizwa na mfumodume, bado ukombozi wa kifikra unamfanya asikubali kuutii na kuuabudu.
Katika mapambano haya, mwanamke amefanikiwa kuonesha hadhi-msingi zake tofauti tofauti zikiwemo: huruma na upendo kwa wanyonge, mpinga dhuluma, mjasiri, mwenye bidii, ubunifu, ujuzi, maarifa na nyenzo bora za kumwezesha kuhimili mikikimikiki ya mfumodume.
Kwa picha hii, makala haya yatasaidia kuongeza matini za Kiswahili zilizoshughulikia mchango wa riwaya za kingano katika ukombozi wa mwanamke na mtoto.
Vilevile, makala haya yatasaidia kuwaongoza wahakiki na watafiti wanaotarajia kuitalii riwaya ya Marimba ya Majaliwa au kazi nyingine ya kingano ili kumsawiri mwanamke.
Related Results
Usawiri wa Nafasi ya Mwanamke katika Tamthiliya ya Kiswahili "Tamthiliya ya Alikiona kama mfano"
Usawiri wa Nafasi ya Mwanamke katika Tamthiliya ya Kiswahili "Tamthiliya ya Alikiona kama mfano"
Makala hii inalenga kuchunguza usawiri wa nafasi ya mwanamke katika tamthiliya ya Kiswahili "Tamthiliya ya Alikiona kama mfano" Katika kufanikisha lengo hili, tulichambua usawiri ...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili
Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Usawiri wa Mwanamke wa Kisasa wa Kiislamu katika Filamu ya Maria.
Usawiri wa Mwanamke wa Kisasa wa Kiislamu katika Filamu ya Maria.
Swahili
Utafiti huu ulilenga kuchunguza usawiri wa mwanamke wa kisasa wa Kiislamu katika filamu ya Maria. Mada ya utafiti ilitokana na utanzu wa fasihi simulizi, ambapo drama, kama...

