Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Usawiri wa Mwanamke wa Kisasa wa Kiislamu katika Filamu ya Maria.

View through CrossRef
Swahili Utafiti huu ulilenga kuchunguza usawiri wa mwanamke wa kisasa wa Kiislamu katika filamu ya Maria. Mada ya utafiti ilitokana na utanzu wa fasihi simulizi, ambapo drama, kama zao la uigizaji, inaporekodiwa kwa kamera, kuhaririwa, na kuunganishwa na sauti, hubadilika kuwa filamu. Lengo la msingi lilikuwa kueleza nafasi ya mwanamke wa Kiislamu katika jamii na kuchunguza jinsi anavyowakilishwa kwa mtazamo chanya na hasi, huku ikizingatiwa tasnia ya fasihi simulizi kupitia filamu. Utafiti ulitumia mbinu ya kimaelezo, ambapo vipindi mia moja vya filamu ya Maria vilichanganuliwa kwa kutumia sampuli lengwa. Data zilikusanywa kupitia matini za kifilamu na kuchanganuliwa kwa njia ya uchanganuzi wa maandishi. Nadharia ya Ufeministi wa Kiislamu ilitumika kama msingi wa uchunguzi, ikizingatia mihimili mitatu: mfumo mzima wa familia, tofauti za kijinsia katika wajibu wa maisha, na ukewenza. Imegunduliwa kuwa mwanamke wa Kiislamu amesawiriwa kwa mitazamo miwili katika filamu ya Maria. Mtazamo chanya ulionyesha mwanamke kama mshauri, mlezi, mkombozi, mchumi, na mwenye mapenzi ya dhati. Hata hivyo, mtazamo hasi ulimchora kama msherati, mshirikina, mgomvi, na mwenye mipango ya hadaa. Filamu hii ilionyesha kuwa usawiri wa mwanamke unaakisi changamoto na fursa zilizopo katika jamii ya Kiislamu ya kisasa. Utafiti ulihitimisha kuwa nafasi ya mwanamke wa Kiislamu mara nyingi huathiriwa na mfumo dume unaodunisha mchango wake. Hata hivyo, mwanamke pia amesawiriwa kama mhusika mwenye nguvu na mabadiliko yanayoweza kuleta mabadiliko ya kijamii. Imependekezwa kuwa jamii ibadili mtazamo wake kuhusu wanawake wa Kiislamu kwa kuwapa nafasi sawa za ajira, elimu, na heshima. Pia, waandishi na watunzi wa filamu wanashauriwa kuonyesha taswira chanya zaidi ili kuchangia mabadiliko ya kijamii.English This study aimed to examine the portrayal of the modern Muslim woman in the film Maria. The research topic was derived from the genre of oral literature. Drama, as a product of performance, when recorded on camera, edited, and combined with sound, transforms into film. The main objective was to explain her role in society and to investigate how she is represented both positively and negatively, while considering the field of oral literature through film. The study employed a descriptive method and analysed one hundred episodes of the film using purposive sampling. Data were collected from film texts and analysed through textual analysis. The guiding theoretical framework was Islamic Feminism, which is based on three pillars: the holistic family system, gender differences in life responsibilities, and polygamy. The study found that the Muslim woman is portrayed from two perspectives. The positive perspective depicts her as a counsellor, caregiver, liberator, economist, and a person of genuine affection. However, the negative perspective portrays her as promiscuous, superstitious, quarrelsome, and deceptive. The film revealed that the portrayal of women reflects both challenges and opportunities within the modern Muslim society. The study concluded that the woman’s role is often influenced by patriarchy, which undermines her contribution. Nonetheless, women are also depicted as strong characters and agents of change. The recommendations are that society should shift its perception of women and grant them equal opportunities in employment, education, and respect. Furthermore, scriptwriters and filmmakers are encouraged to present more positive images to contribute to social transformation. Keywords: Feminism, film, modern Muslim woman, polygamy, portrayal
Title: Usawiri wa Mwanamke wa Kisasa wa Kiislamu katika Filamu ya Maria.
Description:
Swahili Utafiti huu ulilenga kuchunguza usawiri wa mwanamke wa kisasa wa Kiislamu katika filamu ya Maria.
Mada ya utafiti ilitokana na utanzu wa fasihi simulizi, ambapo drama, kama zao la uigizaji, inaporekodiwa kwa kamera, kuhaririwa, na kuunganishwa na sauti, hubadilika kuwa filamu.
Lengo la msingi lilikuwa kueleza nafasi ya mwanamke wa Kiislamu katika jamii na kuchunguza jinsi anavyowakilishwa kwa mtazamo chanya na hasi, huku ikizingatiwa tasnia ya fasihi simulizi kupitia filamu.
Utafiti ulitumia mbinu ya kimaelezo, ambapo vipindi mia moja vya filamu ya Maria vilichanganuliwa kwa kutumia sampuli lengwa.
Data zilikusanywa kupitia matini za kifilamu na kuchanganuliwa kwa njia ya uchanganuzi wa maandishi.
Nadharia ya Ufeministi wa Kiislamu ilitumika kama msingi wa uchunguzi, ikizingatia mihimili mitatu: mfumo mzima wa familia, tofauti za kijinsia katika wajibu wa maisha, na ukewenza.
Imegunduliwa kuwa mwanamke wa Kiislamu amesawiriwa kwa mitazamo miwili katika filamu ya Maria.
Mtazamo chanya ulionyesha mwanamke kama mshauri, mlezi, mkombozi, mchumi, na mwenye mapenzi ya dhati.
Hata hivyo, mtazamo hasi ulimchora kama msherati, mshirikina, mgomvi, na mwenye mipango ya hadaa.
Filamu hii ilionyesha kuwa usawiri wa mwanamke unaakisi changamoto na fursa zilizopo katika jamii ya Kiislamu ya kisasa.
Utafiti ulihitimisha kuwa nafasi ya mwanamke wa Kiislamu mara nyingi huathiriwa na mfumo dume unaodunisha mchango wake.
Hata hivyo, mwanamke pia amesawiriwa kama mhusika mwenye nguvu na mabadiliko yanayoweza kuleta mabadiliko ya kijamii.
Imependekezwa kuwa jamii ibadili mtazamo wake kuhusu wanawake wa Kiislamu kwa kuwapa nafasi sawa za ajira, elimu, na heshima.
Pia, waandishi na watunzi wa filamu wanashauriwa kuonyesha taswira chanya zaidi ili kuchangia mabadiliko ya kijamii.
English This study aimed to examine the portrayal of the modern Muslim woman in the film Maria.
The research topic was derived from the genre of oral literature.
Drama, as a product of performance, when recorded on camera, edited, and combined with sound, transforms into film.
The main objective was to explain her role in society and to investigate how she is represented both positively and negatively, while considering the field of oral literature through film.
The study employed a descriptive method and analysed one hundred episodes of the film using purposive sampling.
Data were collected from film texts and analysed through textual analysis.
The guiding theoretical framework was Islamic Feminism, which is based on three pillars: the holistic family system, gender differences in life responsibilities, and polygamy.
The study found that the Muslim woman is portrayed from two perspectives.
The positive perspective depicts her as a counsellor, caregiver, liberator, economist, and a person of genuine affection.
However, the negative perspective portrays her as promiscuous, superstitious, quarrelsome, and deceptive.
The film revealed that the portrayal of women reflects both challenges and opportunities within the modern Muslim society.
The study concluded that the woman’s role is often influenced by patriarchy, which undermines her contribution.
Nonetheless, women are also depicted as strong characters and agents of change.
The recommendations are that society should shift its perception of women and grant them equal opportunities in employment, education, and respect.
Furthermore, scriptwriters and filmmakers are encouraged to present more positive images to contribute to social transformation.
Keywords: Feminism, film, modern Muslim woman, polygamy, portrayal.

Related Results

Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Makala haya yalichunguza ujitokezaji wa ujumi wa Kiafrika katika ushairi wa Kiswahili wa Bongo Fleva pamoja na athari yake katika ushairi huo. Tafiti kuhusu vipengele vya ujumi wa ...
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Fonolojia ni taaluma iliyosheheni viarudhi au vipambasauti kama ambavyo wataalamu wengine huviita. Miongoni mwake ni toni, lafudhi, mkazo, nguvumsikiko, usilabi, kiimbo, unguvunguv...

Back to Top