Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili

View through CrossRef
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazosawiri mfumo wa maisha unaowaunganisha Waafrika kuishi kwa umoja na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo (Mbaabu, 1985). Riwaya za mwanzo zilihusisha mambo mbalimbali kama vile kusifia uhuru, falsafa ya Ubuntu, na Azimio la Arusha. Kwa kuwa, falsafa ya Ubuntu ilikuwepo toka zamani, ilichunguzwa pia katika riwaya za mwanzo (Roman, 2019). Vilevile, kuna tafiti zimeonesha kuwa falsafa ya Ubuntu imepotea kipindi cha utandawazi (Masimo, 2023). Hivyo, shabaha ya makala hii ni kuonesha mtagusano wa vipengele vya utandawazi na vya falsafa ya Ubuntu katika riwaya za kisasa za Kiswahili. Inasemekana kuwa, uandishi wa riwaya za kisasa ulianza miaka 1990 hadi sasa, ingawa utafiti huu umehusisha riwaya za kisasa zilizoandikwa miaka 2000 hadi 2010. Hii ni kwa sababu, riwaya zilizoandikwa miaka hiyo ni za aina tofauti, kama vile riwaya za kihistoria, za kisasa, na za kisaikolojia (Mulokozi, 2017). Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Mwingilianomatini iliyoasisiwa na Julia Kristeva mwaka 1960. Data zilikusanywa na kuchambuliwa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini wa matini zinazohusiana na utafiti ambazo ni riwaya za kisasa mbili za Kiswahili, nazo ni Babu Alipofufuka (2001) na Makuadi wa Soko Huria (2002). Riwaya hizo zimeteuliwa kwa sababu, zina sifa inayoendana na mada ya utafiti, na ni miongoni mwa riwaya za kisasa zilizoandikwa miaka 2000 mpaka 2010. Vilevile, data zilizopatikana zilifafanuliwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli. Aidha, matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa vipengele vya utandawazi vimetagusana na vipengele vya falsafa ya Ubuntu katika riwaya za kisasa.
Title: Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Description:
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa.
Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazosawiri mfumo wa maisha unaowaunganisha Waafrika kuishi kwa umoja na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo (Mbaabu, 1985).
Riwaya za mwanzo zilihusisha mambo mbalimbali kama vile kusifia uhuru, falsafa ya Ubuntu, na Azimio la Arusha.
Kwa kuwa, falsafa ya Ubuntu ilikuwepo toka zamani, ilichunguzwa pia katika riwaya za mwanzo (Roman, 2019).
Vilevile, kuna tafiti zimeonesha kuwa falsafa ya Ubuntu imepotea kipindi cha utandawazi (Masimo, 2023).
Hivyo, shabaha ya makala hii ni kuonesha mtagusano wa vipengele vya utandawazi na vya falsafa ya Ubuntu katika riwaya za kisasa za Kiswahili.
Inasemekana kuwa, uandishi wa riwaya za kisasa ulianza miaka 1990 hadi sasa, ingawa utafiti huu umehusisha riwaya za kisasa zilizoandikwa miaka 2000 hadi 2010.
Hii ni kwa sababu, riwaya zilizoandikwa miaka hiyo ni za aina tofauti, kama vile riwaya za kihistoria, za kisasa, na za kisaikolojia (Mulokozi, 2017).
Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Mwingilianomatini iliyoasisiwa na Julia Kristeva mwaka 1960.
Data zilikusanywa na kuchambuliwa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini wa matini zinazohusiana na utafiti ambazo ni riwaya za kisasa mbili za Kiswahili, nazo ni Babu Alipofufuka (2001) na Makuadi wa Soko Huria (2002).
Riwaya hizo zimeteuliwa kwa sababu, zina sifa inayoendana na mada ya utafiti, na ni miongoni mwa riwaya za kisasa zilizoandikwa miaka 2000 mpaka 2010.
Vilevile, data zilizopatikana zilifafanuliwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli.
Aidha, matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa vipengele vya utandawazi vimetagusana na vipengele vya falsafa ya Ubuntu katika riwaya za kisasa.

Related Results

Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jami...
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulid...
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Makala hii inalinganisha dhamira zilizowasilishwa kupitia wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili zilizoandikwa na wanawake wa Kenya na Tanzania. Tumaini (2006) ya Clara...

Back to Top