Javascript must be enabled to continue!
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
View through CrossRef
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulidhamiria kuchunguza na kubainisha usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia kutoka kiswahili lugha isiyo na viwakilishi bainifu vya jinsia kwenda kiingereza lugha yenye viwakilishi bainifu ya jinsia.
Mbinu: Data za utafiti zilipatikana kwa kusoma, kuchanganua na kuhakiki tafsiri ya vitabu teule vya fasihi: Siku Njema ya Walibora (1996) na tafsiri yake A Good Day iliyotafsiriwa na Kweyu na Kawegere (2019), Kaburi bila Msalaba iliyoandikwa na Kareithi (1969) na tafsiri yake ya Kiingereza Unmarked Grave iliyotafsiriwa na Githiora (2017). Vilevile, mtafiti aliangazia tamthilia mbili; Tamthilia ya Natala iliyoandikwa na Mberia (1997) na tafsiri yake ya Kiingereza Natala iliyotafsiriwa na Kasu na Marami (2011). Tamthilia ya Kinjekitile iliyoandikwa na Hussein (1969) na tafsiri yake Kinjekitile iliyotafsiriwa na Hussein mwenyewe (1970) ilichunguzwa. Mtafiti aliteua vitabu hivi kwa kuwa vilionesha utajiri wa data inayohusu uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Skopos na Nadharia ya Usawa wa Kidhima. Nadharia ya Skopos iliyoasisiwa na Hanns Vermeer (1978) ambayo husisitiza kuwa, kimsingi kutafsiri kunafaa kushughulikia jukumu la matini chanzi na matini lengwa yaani tafsiri ni kitendo chenye malengo. Nadharia ya Usawa wa Kidhima iliasisiwa na Nida (1964) na inatilia mkazo usawa wa kimaana na athari sawa kwa hadhira katika mchakato wa tafsiri. Baada ya kubainisha uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia, data hiyo ilichanganuliwa kitaamuli na kitakwimu na matokeo kuwasilishwa kupita maandishi ya kinadhari majedwali na michoro ya miche duara kutathimini usahihi uhawilishaji huo.
Matokeo: Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa wafasiri wa vitabu teule wamehawilisha viwakilishi vya jinsia kwa usahihi na uhawilishaji mwingine ukazua utata. Uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia unachangamoto nyingi kwa hivyo wafasiri wanapaswa kumakinika kwani, uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia huwa na athari asi na chanya kwa hadhira lengwa. Mchango wa kipekee kwa nadharia, vitendo na sera: Utafiti huu unapendekeza utafiti zaidi kufanywa katika uhawilishaji wa viwakilishi vya nyakati katika tafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza kwani kama uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia, uhawilishaji wa viwakilishi vya wakati vilevile, vinaweza kuwa na athari kwa ujumbe asilia.
CARI Journals Limited
Title: Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Description:
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza.
Utafiti huu ulidhamiria kuchunguza na kubainisha usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia kutoka kiswahili lugha isiyo na viwakilishi bainifu vya jinsia kwenda kiingereza lugha yenye viwakilishi bainifu ya jinsia.
Mbinu: Data za utafiti zilipatikana kwa kusoma, kuchanganua na kuhakiki tafsiri ya vitabu teule vya fasihi: Siku Njema ya Walibora (1996) na tafsiri yake A Good Day iliyotafsiriwa na Kweyu na Kawegere (2019), Kaburi bila Msalaba iliyoandikwa na Kareithi (1969) na tafsiri yake ya Kiingereza Unmarked Grave iliyotafsiriwa na Githiora (2017).
Vilevile, mtafiti aliangazia tamthilia mbili; Tamthilia ya Natala iliyoandikwa na Mberia (1997) na tafsiri yake ya Kiingereza Natala iliyotafsiriwa na Kasu na Marami (2011).
Tamthilia ya Kinjekitile iliyoandikwa na Hussein (1969) na tafsiri yake Kinjekitile iliyotafsiriwa na Hussein mwenyewe (1970) ilichunguzwa.
Mtafiti aliteua vitabu hivi kwa kuwa vilionesha utajiri wa data inayohusu uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia.
Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Skopos na Nadharia ya Usawa wa Kidhima.
Nadharia ya Skopos iliyoasisiwa na Hanns Vermeer (1978) ambayo husisitiza kuwa, kimsingi kutafsiri kunafaa kushughulikia jukumu la matini chanzi na matini lengwa yaani tafsiri ni kitendo chenye malengo.
Nadharia ya Usawa wa Kidhima iliasisiwa na Nida (1964) na inatilia mkazo usawa wa kimaana na athari sawa kwa hadhira katika mchakato wa tafsiri.
Baada ya kubainisha uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia, data hiyo ilichanganuliwa kitaamuli na kitakwimu na matokeo kuwasilishwa kupita maandishi ya kinadhari majedwali na michoro ya miche duara kutathimini usahihi uhawilishaji huo.
Matokeo: Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa wafasiri wa vitabu teule wamehawilisha viwakilishi vya jinsia kwa usahihi na uhawilishaji mwingine ukazua utata.
Uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia unachangamoto nyingi kwa hivyo wafasiri wanapaswa kumakinika kwani, uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia huwa na athari asi na chanya kwa hadhira lengwa.
Mchango wa kipekee kwa nadharia, vitendo na sera: Utafiti huu unapendekeza utafiti zaidi kufanywa katika uhawilishaji wa viwakilishi vya nyakati katika tafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza kwani kama uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia, uhawilishaji wa viwakilishi vya wakati vilevile, vinaweza kuwa na athari kwa ujumbe asilia.
Related Results
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika ...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili
Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Uhawilishaji Mkazo wa Kiswahili kwa wajifunzaji Kiswahili kama Lugha ya Pili : Uchunguzi kifani wajifunzaji Warundi nchini Burundi
Uhawilishaji Mkazo wa Kiswahili kwa wajifunzaji Kiswahili kama Lugha ya Pili : Uchunguzi kifani wajifunzaji Warundi nchini Burundi
Kiswahili
Makala hii imechunguza uhawilishaji mkazo wa Kiswahili kwa wajifunzaji Warundi wanaojifunza lugha hiyo kama lugha ya pili. Lengo kuu la makala hii ni kuchunguza namna mka...

