Javascript must be enabled to continue!
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
View through CrossRef
Swahili
Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi wa kufana hujengeka kwa tamaduni zinazokubalika na zenye kuheshimika. Makala haya yalipambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Malengo mahususi yalikuwa ni: kutathmini utamaduni wa uongozi wa shule; kubainisha ni jinsi gani Kiswahili kinatumika kujenga utamaduni wa uongozi wa shule; na kupambanua mitazamo ya washikadau kuhusu matumizi ya Kiswahili katika uongozi wa Shule ya Msingi ya Mungakha. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Tabia ya Uongozi ya Fleenor (2006). Mkabala wa kithamano na muundo wa kimfano uliongoza utafiti huu. Mbinu ya ukusanyaji wa data iliyotumiwa ni hojaji. Sampuli lengwa ilihusisha shule moja ya msingi, mwalimu mkuu, naibu wake, wakuu wa jopo, viranja, wanachama wa halmashauri ya uongozi wa shule, wafanyakazi na wazazi. Usampulishaji wa kimaksudi uliteua Shule ya Msingi ya Mungakha, mwalimu mkuu na naibu wake. Usampulishaji wa kinasibu uliwachagua wanachama wa halmashauri ya usimamizi wa shule, wakuu wa jopo, viranja na wafanyakazi. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kutumia kielelezo cha nyaraka, kisha ikawasilishwa kwa kurejelea malengo ya utafiti kwa maelezo ya kifafanuzi na mijadala kutolewa. Matokeo yalibainisha kuwa utamaduni katika Shule ya Msingi ya Mungakha ulikuwa wa umoja, uongozi wa kielelezo, mazingira bora ya ujifunzaji, ugatuzi wa mamlaka, kushirikishwa kwa wanafunzi, kuhusishwa kwa wazazi na mawasiliano ya wazi. Lugha ya Kiswahili na Kiingereza zilitumika kwa kiwango kizuri huku Kinyala kikitumika kwa kiwango cha chini. Washikadau walipendelea matumizi ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa kiwango cha wastani na Kinyala kwa kiwango cha chini sana katika shule hii.
English
The aim of this article is to examine the role of Kiswahili in the establishment of leadership culture at Mungakha Primary School in Kakamega County, Kenya. Successful leadership is based on acceptable and respectful traditions. This paper outlined the role of Kiswahili in establishing leadership tradition at Mungakha Primary School in Kakamega County, Kenya. The specific objectives were to establish the leadership tradition in the school; to outline how Kiswahili is used in the establishment of leadership tradition in the school; and lastly, to discuss the views of stakeholders on leadership tradition at Mungakha Primary School. The research was guided by the Trait Approach to Leadership by Fleenor (2006). This research adopted a descriptive research design, specifically the case study design. The method of data collection used was questionnaires. The target sample entailed one primary school, the head teacher, and the deputy head teacher. The board of management members, subject panel heads, prefects, and non-teaching staff were sampled randomly. The data collected were analysed using document analysis and presented descriptively according to the study objectives, alongside discussions. The study found that there was a leadership tradition of unity, leading by example, a safe and conducive learning environment, delegation of duties, student-centred leadership, parental involvement, and an open communication policy in the school. Kiswahili and English were used at a good level, while Kinyala was used at a low level in establishing leadership tradition. The stakeholders preferred the use of Kiswahili and English at a higher level, while Kinyala was preferred at a low level in the leadership of the school.
Key words: Establishing, Kiswahili, language, leadership, tradition.
Editon Consortium Publishing
Title: Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Description:
Swahili
Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya.
Uongozi wa kufana hujengeka kwa tamaduni zinazokubalika na zenye kuheshimika.
Makala haya yalipambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya.
Malengo mahususi yalikuwa ni: kutathmini utamaduni wa uongozi wa shule; kubainisha ni jinsi gani Kiswahili kinatumika kujenga utamaduni wa uongozi wa shule; na kupambanua mitazamo ya washikadau kuhusu matumizi ya Kiswahili katika uongozi wa Shule ya Msingi ya Mungakha.
Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Tabia ya Uongozi ya Fleenor (2006).
Mkabala wa kithamano na muundo wa kimfano uliongoza utafiti huu.
Mbinu ya ukusanyaji wa data iliyotumiwa ni hojaji.
Sampuli lengwa ilihusisha shule moja ya msingi, mwalimu mkuu, naibu wake, wakuu wa jopo, viranja, wanachama wa halmashauri ya uongozi wa shule, wafanyakazi na wazazi.
Usampulishaji wa kimaksudi uliteua Shule ya Msingi ya Mungakha, mwalimu mkuu na naibu wake.
Usampulishaji wa kinasibu uliwachagua wanachama wa halmashauri ya usimamizi wa shule, wakuu wa jopo, viranja na wafanyakazi.
Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kutumia kielelezo cha nyaraka, kisha ikawasilishwa kwa kurejelea malengo ya utafiti kwa maelezo ya kifafanuzi na mijadala kutolewa.
Matokeo yalibainisha kuwa utamaduni katika Shule ya Msingi ya Mungakha ulikuwa wa umoja, uongozi wa kielelezo, mazingira bora ya ujifunzaji, ugatuzi wa mamlaka, kushirikishwa kwa wanafunzi, kuhusishwa kwa wazazi na mawasiliano ya wazi.
Lugha ya Kiswahili na Kiingereza zilitumika kwa kiwango kizuri huku Kinyala kikitumika kwa kiwango cha chini.
Washikadau walipendelea matumizi ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa kiwango cha wastani na Kinyala kwa kiwango cha chini sana katika shule hii.
English
The aim of this article is to examine the role of Kiswahili in the establishment of leadership culture at Mungakha Primary School in Kakamega County, Kenya.
Successful leadership is based on acceptable and respectful traditions.
This paper outlined the role of Kiswahili in establishing leadership tradition at Mungakha Primary School in Kakamega County, Kenya.
The specific objectives were to establish the leadership tradition in the school; to outline how Kiswahili is used in the establishment of leadership tradition in the school; and lastly, to discuss the views of stakeholders on leadership tradition at Mungakha Primary School.
The research was guided by the Trait Approach to Leadership by Fleenor (2006).
This research adopted a descriptive research design, specifically the case study design.
The method of data collection used was questionnaires.
The target sample entailed one primary school, the head teacher, and the deputy head teacher.
The board of management members, subject panel heads, prefects, and non-teaching staff were sampled randomly.
The data collected were analysed using document analysis and presented descriptively according to the study objectives, alongside discussions.
The study found that there was a leadership tradition of unity, leading by example, a safe and conducive learning environment, delegation of duties, student-centred leadership, parental involvement, and an open communication policy in the school.
Kiswahili and English were used at a good level, while Kinyala was used at a low level in establishing leadership tradition.
The stakeholders preferred the use of Kiswahili and English at a higher level, while Kinyala was preferred at a low level in the leadership of the school.
Key words: Establishing, Kiswahili, language, leadership, tradition.
Related Results
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika ...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Uongozi na Uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Uongozi na Uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Kiswahili
Lengo la makala hii ni kuchunguza uongozi na uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (MME) katika tamthilia teule za Kiswahili. Kazi hii iliongozwa na Nadharia ya Uhis...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...

