Javascript must be enabled to continue!
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
View through CrossRef
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi yoyote ile. Nchini Kenya, vipengele katika katiba ya 2010, vinavyohusu lugha vilipandisha hadhi lugha ya Kiswahili ili iweze kutumika kama lugha ya taifa na rasmi sambamba na Kiingereza. Hata hivyo, katiba hii haijaweka kanuni zinazolenga kuimarisha na kudumisha uanuwai wa lugha za kiasili kote nchini Kenya. Machukulio ni kwamba, vipengele vya katiba vinasheheni sifa stahilifu kama vile, usawa wa kimatumizi, utekelezwaji, mikao ya kieneo, matakwa, pamoja na hiari za wananchi. Kwa kuangazia hali ya kiisimu-jamii katika Kaunti ya Bungoma, utata upo katika udumishaji wa mfumo ‘rasmi’ wa sera ya lugha Kitaifa, na utekelezwaji wa sera ya lugha kupitia asasi za serikali na zile za umma. Kazi hii inalenga kuchanganua uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu kupitia ruwaza zinazodhihirika katika mawanda mbalimbali ya lugha katika Kaunti ya Bungoma. Mihimili ya nadharia ya sera ya lugha iliyoendelezwa na Spolsky (2004, 2007) ambayo ni Usimamizi wa lugha na Ikolojia ya lugha pamoja na ruwaza za lugha ilivyoelezwa na Paltridge (2001) ndiyo nguzo ya kuchanganua utafiti huu. Aidha, mtazamo wa Haugen (1972) unaohusu Ikolojia ya lugha umetumika katika kudhihirisha michakato baina ya lugha na mazingira inamotumika. Muundo mseto uliojumuisha, muundo wa kimaelezo, kiupelelezi na wa kiiktisadi ulitumiwa. Usampulishaji dhamirifu ulitumiwa kuteua matumizi ya lugha ya KS, KB na KS/KB katika ruwaza za lugha zilizodhihirika katika mawanda ya biashara, kanisani na utawala hasa kwenye mikutano ya umma au baraza za Chifu katika maeneo mbalimbali ya Kaunti ya Bungoma. Data ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchunzaji usio-shirikishi na ya kiiktisadi ilikusanywa kwa kuhesabu hali ambazo lugha za KS, KB au KS/KB zilitumiwa. Ilibainika kuwa lugha ya KS na KB hukamilishana kiuamilifu katika mawanda mbalimbali ya kijamii katika Kaunti ya Bungoma.
East African Nature and Science Organization
Title: Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Description:
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu.
Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi yoyote ile.
Nchini Kenya, vipengele katika katiba ya 2010, vinavyohusu lugha vilipandisha hadhi lugha ya Kiswahili ili iweze kutumika kama lugha ya taifa na rasmi sambamba na Kiingereza.
Hata hivyo, katiba hii haijaweka kanuni zinazolenga kuimarisha na kudumisha uanuwai wa lugha za kiasili kote nchini Kenya.
Machukulio ni kwamba, vipengele vya katiba vinasheheni sifa stahilifu kama vile, usawa wa kimatumizi, utekelezwaji, mikao ya kieneo, matakwa, pamoja na hiari za wananchi.
Kwa kuangazia hali ya kiisimu-jamii katika Kaunti ya Bungoma, utata upo katika udumishaji wa mfumo ‘rasmi’ wa sera ya lugha Kitaifa, na utekelezwaji wa sera ya lugha kupitia asasi za serikali na zile za umma.
Kazi hii inalenga kuchanganua uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu kupitia ruwaza zinazodhihirika katika mawanda mbalimbali ya lugha katika Kaunti ya Bungoma.
Mihimili ya nadharia ya sera ya lugha iliyoendelezwa na Spolsky (2004, 2007) ambayo ni Usimamizi wa lugha na Ikolojia ya lugha pamoja na ruwaza za lugha ilivyoelezwa na Paltridge (2001) ndiyo nguzo ya kuchanganua utafiti huu.
Aidha, mtazamo wa Haugen (1972) unaohusu Ikolojia ya lugha umetumika katika kudhihirisha michakato baina ya lugha na mazingira inamotumika.
Muundo mseto uliojumuisha, muundo wa kimaelezo, kiupelelezi na wa kiiktisadi ulitumiwa.
Usampulishaji dhamirifu ulitumiwa kuteua matumizi ya lugha ya KS, KB na KS/KB katika ruwaza za lugha zilizodhihirika katika mawanda ya biashara, kanisani na utawala hasa kwenye mikutano ya umma au baraza za Chifu katika maeneo mbalimbali ya Kaunti ya Bungoma.
Data ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchunzaji usio-shirikishi na ya kiiktisadi ilikusanywa kwa kuhesabu hali ambazo lugha za KS, KB au KS/KB zilitumiwa.
Ilibainika kuwa lugha ya KS na KB hukamilishana kiuamilifu katika mawanda mbalimbali ya kijamii katika Kaunti ya Bungoma.
Related Results
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nyanja mbalimbali katika jamii hutegemea matumizi ya lugha. Hali hii huzua changamoto ya namna ya kutumia raslimali za lugha zinazopatikana katika jamiilugha fulani. Juhudi ya kufa...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili
Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania
Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania
Makala haya yanaeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ujumuishaji wa kidemokrasia nchini Tanzania kwa kuzingatia matumizi ya lugha hiyo kwenye michakato ya uchaguzi. Lengo la...

