Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania

View through CrossRef
Makala haya yanaeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ujumuishaji wa kidemokrasia nchini Tanzania kwa kuzingatia matumizi ya lugha hiyo kwenye michakato ya uchaguzi. Lengo la makala haya ni kuonesha maeneo muhimu ya uchaguzi ambamo lugha ya Kiswahili inatumika, na kupendekeza mikakati inayoweza kufanikisha lugha hiyo kutumika zaidi katika masuala ya uchaguzi na kwenye michakato mingine ya ujenzi wa demokrasia Tanzania. Makala haya yanaakisi matumizi na mchango muhimu wa lugha ya Kiswahili katika michakato ya siasa za uchaguzi nchini Tanzania kama sehemu ya ujumuishaji wa kidemokrasia. Inaonesha kuwa katika michakato ya uchaguzi nchini Tanzania, lugha ya Kiswahili inatumiwa ili kufanya mawasiliano yanayoweza kuwajumuisha Watanzania wengi kwenye hatua mbalimbali za shughuli za uchaguzi. Makala haya yanatumia Nadharia ya Uchambuzi Kilongo. Nadharia hii inaeleza kuwa athari za matumizi ya lugha hazibaki kwenye eneo lake la matumizi pekee bali huvuka mipaka ya muktadha wa matumizi yake na kuathiri masilugha mengine. Makala haya yametumia data za upili ambapo nyaraka ngumu na laini zilizoandikwa kwa Kiswahili kuhusu shughuli za uchaguzi nchini Tanzania zilisomwa. Data za utafiti huu zimewasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo ya utafiti uliozaa makala haya yanaonesha kwamba lugha ya Kiswahili inawawezesha Watanzania wengi kujumuishwa kwenye demokrasia ya uchaguzi kupitia michakato mbalimbali ambayo ni uandikaji wa matini tumizi ya uchaguzi, nyimbo za kampeni za uchaguzi, utangazaji wa matokeo ya uchaguzi, uapisho wa viongozi wateule, uandikaji wa ripoti ya uchaguzi na tathmini ya uchaguzi. Makala haya yanapendekeza kuwa matumizi ya lugha ya Kiswahili yaimarishwe zaidi kwenye michakato ya uchaguzi na kwenye michakato mingine ya kisiasa ili kujenga ujumuishi mpana wa kidemokrasia.
University of Dar es Salaam
Title: Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania
Description:
Makala haya yanaeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ujumuishaji wa kidemokrasia nchini Tanzania kwa kuzingatia matumizi ya lugha hiyo kwenye michakato ya uchaguzi.
Lengo la makala haya ni kuonesha maeneo muhimu ya uchaguzi ambamo lugha ya Kiswahili inatumika, na kupendekeza mikakati inayoweza kufanikisha lugha hiyo kutumika zaidi katika masuala ya uchaguzi na kwenye michakato mingine ya ujenzi wa demokrasia Tanzania.
Makala haya yanaakisi matumizi na mchango muhimu wa lugha ya Kiswahili katika michakato ya siasa za uchaguzi nchini Tanzania kama sehemu ya ujumuishaji wa kidemokrasia.
Inaonesha kuwa katika michakato ya uchaguzi nchini Tanzania, lugha ya Kiswahili inatumiwa ili kufanya mawasiliano yanayoweza kuwajumuisha Watanzania wengi kwenye hatua mbalimbali za shughuli za uchaguzi.
Makala haya yanatumia Nadharia ya Uchambuzi Kilongo.
Nadharia hii inaeleza kuwa athari za matumizi ya lugha hazibaki kwenye eneo lake la matumizi pekee bali huvuka mipaka ya muktadha wa matumizi yake na kuathiri masilugha mengine.
Makala haya yametumia data za upili ambapo nyaraka ngumu na laini zilizoandikwa kwa Kiswahili kuhusu shughuli za uchaguzi nchini Tanzania zilisomwa.
Data za utafiti huu zimewasilishwa kwa njia ya maelezo.
Matokeo ya utafiti uliozaa makala haya yanaonesha kwamba lugha ya Kiswahili inawawezesha Watanzania wengi kujumuishwa kwenye demokrasia ya uchaguzi kupitia michakato mbalimbali ambayo ni uandikaji wa matini tumizi ya uchaguzi, nyimbo za kampeni za uchaguzi, utangazaji wa matokeo ya uchaguzi, uapisho wa viongozi wateule, uandikaji wa ripoti ya uchaguzi na tathmini ya uchaguzi.
Makala haya yanapendekeza kuwa matumizi ya lugha ya Kiswahili yaimarishwe zaidi kwenye michakato ya uchaguzi na kwenye michakato mingine ya kisiasa ili kujenga ujumuishi mpana wa kidemokrasia.

Related Results

Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika ...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...

Back to Top