Javascript must be enabled to continue!
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
View through CrossRef
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa vizuri katika mtihani wa kitaifa. Upande wa Kiswahili, kuna ugumu katika ujifunzaji wa ushairi wa Kiswahili na ugumu huu umesababisha matokeo mabaya katika mtihani wa kitaifa katika somo la ushairi wa Kiswahili nchini Uganda. Wanafunzi hawa husomea katika mandhari sawa. Hili linazua swali: kwa nini wanafunzi wanaofanya mtihani wa ushairi wa Kiganda watende vizuri kuliko wanafunzi wa ushairi wa Kiswahili? Makala hii itaweka wazi mambo ambayo ushairi wa Kiswahili waweza kukopa kutoka ushairi wa Kiganda na kujiendeleza. Madhumuni ya makala hii yatakuwa: Kudadavua jinsi ushairi wa Kiganda unaweza kusahilisha mtindo katika ushairi wa Kiswahili kupitia ufunzaji na ujifunzaji na kutathimini jinsi ushairi wa Kiganda unaweza kukuza maudhui katika ushairi wa Kiswahili kupitia ufunzaji na ujifunzaji. Mashairi yalikusanywa kutoka diwani mbili za Kiswahili na mbili za Kiganda. Mashairi 60 yalikusanywa yaani 30 ya Kiganda na 30 ya Kiswahili na 15 yalichaguliwa kutoka kila lugha kwa kutumia uteuzi nasibu. Mashairi yalitolewa kwenye diwani za Kiswahili; “Malenga wa ziwa kuu” na “Malenga wa karne moja” na za Kiganda; “Ab’Oluganda ab’Enda emu” na “Balya n’ensekeezi”. Makala hii unafafanua jinsi mwalimu wa ushairi wa Kiswahili anavyoweza kuhamisha maarifa kutoka ushairi wa Kiganda hadi wa Kiswahili. Utamsaidia kuendeleza ushairi wa Kiswahili kuhamisha maarifa ya ujifunzaji na ufunzaji kutokana na ushairi wa Kiganda ili kusahilisha ujifunzaji wa ushairi wa Kiswahili.
SASPR Edu International Pvt. Ltd
Title: Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Description:
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili.
Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa vizuri katika mtihani wa kitaifa.
Upande wa Kiswahili, kuna ugumu katika ujifunzaji wa ushairi wa Kiswahili na ugumu huu umesababisha matokeo mabaya katika mtihani wa kitaifa katika somo la ushairi wa Kiswahili nchini Uganda.
Wanafunzi hawa husomea katika mandhari sawa.
Hili linazua swali: kwa nini wanafunzi wanaofanya mtihani wa ushairi wa Kiganda watende vizuri kuliko wanafunzi wa ushairi wa Kiswahili? Makala hii itaweka wazi mambo ambayo ushairi wa Kiswahili waweza kukopa kutoka ushairi wa Kiganda na kujiendeleza.
Madhumuni ya makala hii yatakuwa: Kudadavua jinsi ushairi wa Kiganda unaweza kusahilisha mtindo katika ushairi wa Kiswahili kupitia ufunzaji na ujifunzaji na kutathimini jinsi ushairi wa Kiganda unaweza kukuza maudhui katika ushairi wa Kiswahili kupitia ufunzaji na ujifunzaji.
Mashairi yalikusanywa kutoka diwani mbili za Kiswahili na mbili za Kiganda.
Mashairi 60 yalikusanywa yaani 30 ya Kiganda na 30 ya Kiswahili na 15 yalichaguliwa kutoka kila lugha kwa kutumia uteuzi nasibu.
Mashairi yalitolewa kwenye diwani za Kiswahili; “Malenga wa ziwa kuu” na “Malenga wa karne moja” na za Kiganda; “Ab’Oluganda ab’Enda emu” na “Balya n’ensekeezi”.
Makala hii unafafanua jinsi mwalimu wa ushairi wa Kiswahili anavyoweza kuhamisha maarifa kutoka ushairi wa Kiganda hadi wa Kiswahili.
Utamsaidia kuendeleza ushairi wa Kiswahili kuhamisha maarifa ya ujifunzaji na ufunzaji kutokana na ushairi wa Kiganda ili kusahilisha ujifunzaji wa ushairi wa Kiswahili.
Related Results
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Uathirianomatini wa Kimtindo katika Ushairi wa Kiswahili: Mfano wa “Utenzi wa Hati” na “Utenzi wa Mwanakupona”
Uathirianomatini wa Kimtindo katika Ushairi wa Kiswahili: Mfano wa “Utenzi wa Hati” na “Utenzi wa Mwanakupona”
Bakhtin (1981) anaeleza kwamba matini za kifasihi huathiriana na kuhusiana. Kila matini ya kifasihi ina sauti zinazoingiliana na kuhusiana na matini nyingine zilizopo, zilizopita a...
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza namna ambavyo Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa kwa nchi ya Uganda. Ni kweli kwamba nchini Uganda, watu kadhaa wakiwemo baadhi ya wanasiasa ha...
Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda
Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda
Umahiri wa kuzungumza lugha ni miongoni mwa matokeo yanayotarajiwa kutoka kwa mtu yeyote anayejifunza lugha ya kigeni au lugha ya pili. Mathalani nchini Uganda imebainika kuwa kiwa...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili
Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Maoni ya wanafunzi wa taasisi za kiufundi za kitaifa kuhusu nafasi ya Kiswahili katika elimu ya ufundi nchini Kenya
Maoni ya wanafunzi wa taasisi za kiufundi za kitaifa kuhusu nafasi ya Kiswahili katika elimu ya ufundi nchini Kenya
Utafiti huu ulinuia kutafuta maoni ya wanafunzi wa taasisi za kiufundi za kitaifa kuhusu nafasi ya lugha ya Kiswahili katika elimu ya kiufundi. Muundo wa Uchunguzi Kimaelezo ulitum...

