Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda

View through CrossRef
Katika makala haya, mtafiti anaeleza namna ambavyo Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa kwa nchi ya Uganda. Ni kweli kwamba nchini Uganda, watu kadhaa wakiwemo baadhi ya wanasiasa hawaoni umuhimu wa lugha ya Kiswahili. Hata hivyo, nchi ya Uganda inaweza kunufaika pakubwa sana hasa kiuchumi kutokana na lugha ya Kiswahili. Ni jambo la wazi kuwa uchumi duni hufanya nchi ikose kupata maendeleo ilhali uchumi imara hufanya nchi iwe na maendeleo. Nchi zenye nguvu kama vile Marekani na zile za Ulaya zimeweza kupata maendeleo makubwa kwa sababu ya kuwa na uchumi imara. Kwa hiyo, nchi mbalimbali huweka mikakati maalumu ya kuimarisha uchumi zao. Nchi huwa zinaimarisha uchumi zaokwa kuimarisha sekta za biashara, kilimo, viwanda, uvuvi na utalii. Halikadhalika, nchi nyingi hutenga kiasi kikubwa cha pesa katika bajeti zao za kila mwaka wa kifedha kwa ajili ya kuimarisha sekta mbalimbali zinazoimarisha uchumi. Nchi mbalimbali pia huendeleza sekta ya kibinafsi katika harakati zao za kuimarisha uchumi na kuondoa umaskini katika jamii. Kwa hiyo, watu binafsi huwa wanahamasishwa kuanzisha miradi mbalimbali na kubuni kazi kwa wananchi badala ya kusubiri serikali. Hata hivyo, nchini Uganda, wanasiasa hawajaona umuhimu wa lugha ya Kiswahili na nchi hii ni mwanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa hiyo, katika makala hii, mtafiti anaeleza jinsi Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa kwa Waganda. Utafiti huu ulikusudia kujibu swali; Je, Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa yoyote kwa nchi ya Uganda? Katika kazi hii, mkabala wa utafiti ulikuwa wa nyanjani. Mtafiti aliendeleza utafiti katika Wilaya ya Bududa nchini Uganda. Wahojiwa walikuwa walimu katika shule za sekondari. Taarifa zilikusanywa kutoka kwa walimu 100. Baada ya taarifa kukusanywa, mtafiti alizichanganua data hizo na kubainisha hoja tofautitofauti. Umuhimu wa utafiti huu ni kuwa ulipelekea wananchi wa Uganda kuona umuhimu wa lugha ya Kiswahili na hivyo kuanza kuitetea badala ya kuipiga vita.
East African Nature and Science Organization
Title: Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Description:
Katika makala haya, mtafiti anaeleza namna ambavyo Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa kwa nchi ya Uganda.
Ni kweli kwamba nchini Uganda, watu kadhaa wakiwemo baadhi ya wanasiasa hawaoni umuhimu wa lugha ya Kiswahili.
Hata hivyo, nchi ya Uganda inaweza kunufaika pakubwa sana hasa kiuchumi kutokana na lugha ya Kiswahili.
Ni jambo la wazi kuwa uchumi duni hufanya nchi ikose kupata maendeleo ilhali uchumi imara hufanya nchi iwe na maendeleo.
Nchi zenye nguvu kama vile Marekani na zile za Ulaya zimeweza kupata maendeleo makubwa kwa sababu ya kuwa na uchumi imara.
Kwa hiyo, nchi mbalimbali huweka mikakati maalumu ya kuimarisha uchumi zao.
Nchi huwa zinaimarisha uchumi zaokwa kuimarisha sekta za biashara, kilimo, viwanda, uvuvi na utalii.
Halikadhalika, nchi nyingi hutenga kiasi kikubwa cha pesa katika bajeti zao za kila mwaka wa kifedha kwa ajili ya kuimarisha sekta mbalimbali zinazoimarisha uchumi.
Nchi mbalimbali pia huendeleza sekta ya kibinafsi katika harakati zao za kuimarisha uchumi na kuondoa umaskini katika jamii.
Kwa hiyo, watu binafsi huwa wanahamasishwa kuanzisha miradi mbalimbali na kubuni kazi kwa wananchi badala ya kusubiri serikali.
Hata hivyo, nchini Uganda, wanasiasa hawajaona umuhimu wa lugha ya Kiswahili na nchi hii ni mwanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa hiyo, katika makala hii, mtafiti anaeleza jinsi Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa kwa Waganda.
Utafiti huu ulikusudia kujibu swali; Je, Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa yoyote kwa nchi ya Uganda? Katika kazi hii, mkabala wa utafiti ulikuwa wa nyanjani.
Mtafiti aliendeleza utafiti katika Wilaya ya Bududa nchini Uganda.
Wahojiwa walikuwa walimu katika shule za sekondari.
Taarifa zilikusanywa kutoka kwa walimu 100.
Baada ya taarifa kukusanywa, mtafiti alizichanganua data hizo na kubainisha hoja tofautitofauti.
Umuhimu wa utafiti huu ni kuwa ulipelekea wananchi wa Uganda kuona umuhimu wa lugha ya Kiswahili na hivyo kuanza kuitetea badala ya kuipiga vita.

Related Results

Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika ...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda
Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda
Umahiri wa kuzungumza lugha ni miongoni mwa matokeo yanayotarajiwa kutoka kwa mtu yeyote anayejifunza lugha ya kigeni au lugha ya pili. Mathalani nchini Uganda imebainika kuwa kiwa...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...

Back to Top