Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo

View through CrossRef
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika kuwasilisha maudhui ya kidini, sera za matumizi ya lugha, na athari ya matumizi ya lugha ya Kiswahili katika kuwasilisha ujumbe wa kidini. Nadharia ya umilisi mawasiliano yake Dell Hymes (1966) iliongoza utafiti. Data ilikusanywa kwa kutumia hojaji, mahojiano na uchunzaji. Wanafunzi thelathini wa kidato cha nne, viongozi kumi wa kidini wa wanafunzi na kasisi mmoja wa shule walihusishwa katika ukusanyaji wa data. Matokeo yalibaini kuwa sera ya lugha katika shule ya wasichana ya Itigo ilipendelea matumizi ya Kingereza kama lugha ya mawasiliano. Wanafunzi walisema kuwa lugha ya Kiswahili inapotumika katika mahubiri, ujumbe hueleweka zaidi. Vilevile, ilidhihirika kuwa viongozi wa kidini wa wanafunzi hutumia lugha ya Kiswahili kuwasiliana katika mikutano yao lakini wao huandika kumbukumbu kwa lugha ya Kiingereza. Isitoshe, ilibainika kuwa lugha anayoitumia zaidi kasisi wa shule katika mahubiri yake ni Kiingereza. Licha ya uwezo wa Kiswahili katika kufanikisha mawasiliano kuhusu maswala ya kidini shuleni, Kiingereza ndicho hutumika zaidi. Kunahitajika mabadiliko katika sera ya lugha shuleni ili kuipa lugha ya Kiswahili nafasi zaidi katika mawasiliano ya kidini
Title: Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Description:
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo.
Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika kuwasilisha maudhui ya kidini, sera za matumizi ya lugha, na athari ya matumizi ya lugha ya Kiswahili katika kuwasilisha ujumbe wa kidini.
Nadharia ya umilisi mawasiliano yake Dell Hymes (1966) iliongoza utafiti.
Data ilikusanywa kwa kutumia hojaji, mahojiano na uchunzaji.
Wanafunzi thelathini wa kidato cha nne, viongozi kumi wa kidini wa wanafunzi na kasisi mmoja wa shule walihusishwa katika ukusanyaji wa data.
Matokeo yalibaini kuwa sera ya lugha katika shule ya wasichana ya Itigo ilipendelea matumizi ya Kingereza kama lugha ya mawasiliano.
Wanafunzi walisema kuwa lugha ya Kiswahili inapotumika katika mahubiri, ujumbe hueleweka zaidi.
Vilevile, ilidhihirika kuwa viongozi wa kidini wa wanafunzi hutumia lugha ya Kiswahili kuwasiliana katika mikutano yao lakini wao huandika kumbukumbu kwa lugha ya Kiingereza.
Isitoshe, ilibainika kuwa lugha anayoitumia zaidi kasisi wa shule katika mahubiri yake ni Kiingereza.
Licha ya uwezo wa Kiswahili katika kufanikisha mawasiliano kuhusu maswala ya kidini shuleni, Kiingereza ndicho hutumika zaidi.
Kunahitajika mabadiliko katika sera ya lugha shuleni ili kuipa lugha ya Kiswahili nafasi zaidi katika mawasiliano ya kidini.

Related Results

Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania
Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania
Makala haya yanaeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ujumuishaji wa kidemokrasia nchini Tanzania kwa kuzingatia matumizi ya lugha hiyo kwenye michakato ya uchaguzi. Lengo la...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili

Back to Top