Javascript must be enabled to continue!
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
View through CrossRef
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee ya uandishi ambayo watu wasioona hutumia katika mawasiliano na usomi wao. Vilevile, kutokuwepo kwa kipengele muhimu cha matamshi katika kamusi za breili na vitabu vya sarufi hasa vya sekondari. Jambo jingine ni kwamba, wanafunzi wanaotumia breili hupewa maswali mbadala wakati wanapotahiniwa katika maeneo ya fonolojia, mofolojia, na hata katika uchanganuzi wa sentensi. Aidha, kutokuwepo kwa ishara bainifu za isimu katika maandishi ya breili ya Kiswahili. Kichocheo cha mwisho, praima mbili za breili ya Kiswahili: ya 1978 na 1995 zinazotumiwa Afrika Mashariki hazina ishara za kiisimu. Utafiti huu ulikusudia kujibu maswali yafuatayo: changamoto zipi zinazozuia usimilishaji wa ishara za kiisimu katika breili ya Kiswahili? Rasimu za Kiingereza na Kiswahili huathiriana kwa njia zipi? Ukosefu wa ishara za isimu katika breili huathiri ufundishaji wa isimu kwa njia gani? Na mwisho, mikato ya Kiswahili na ya Kiingereza inayotumia nukta zinazofanana huathiri uchapishaji wa vitabu vya isimu kwa njia zipi? Utafiti huu ulilenga kutimiza malengo yafuatayo – kwanza, kubainisha na kutatua changamoto zinazozuia usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Pili, Kuchanganua rasimu ya Kiingereza na ya Kiswahili. Aidha, kuchunguza athari ya ukosefu wa ishara hizi katika ufundishaji wa isimu. Mwisho, kutathmini athari ya matumizi ya mikato inayotumia nukta zinazofanana katika uchapishaji wa vitabu vya isimu. Makala haya yameshughulikia vikwazo vya usimilishaji wa ishara za isimu katika breili. Mtafiti alitumia mbinu ya mahojiano katika kukusanya dataUtafiti huu ulichanganua usimilishaji wa ishara hizi kwa kuzingatia nadharia ya usomaji na uandishi wa breili iliyoasisiwa na Kizuka na Fuji (2005). Mtafiti aligundua kuwa uchache wa nukta nundu umesababisha uradidi mwingi wa matumizi ya nukta nundu hizi. Uradidi huu umechangia kuwepo kwa utata wa kimaana katika fonolojia na sintaksia ya Kiswahili, vikwazo vya ufundishaji wa isimu miongoni mwa wanafunzi wasioona, makosa katika vitabu vya sarufi hasa kidato cha kwanza na kidato cha pili na changamoto zinazotinga usimilishaji wa ishara za kiisimu katika Breili. Utafiti huu utawafaidi wanafunzi wanaotumia breili na walimu na wahadhiri wanaofunza isimu
East African Nature and Science Organization
Title: Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Description:
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili.
Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu.
Kwanza, breili ndio njia ya pekee ya uandishi ambayo watu wasioona hutumia katika mawasiliano na usomi wao.
Vilevile, kutokuwepo kwa kipengele muhimu cha matamshi katika kamusi za breili na vitabu vya sarufi hasa vya sekondari.
Jambo jingine ni kwamba, wanafunzi wanaotumia breili hupewa maswali mbadala wakati wanapotahiniwa katika maeneo ya fonolojia, mofolojia, na hata katika uchanganuzi wa sentensi.
Aidha, kutokuwepo kwa ishara bainifu za isimu katika maandishi ya breili ya Kiswahili.
Kichocheo cha mwisho, praima mbili za breili ya Kiswahili: ya 1978 na 1995 zinazotumiwa Afrika Mashariki hazina ishara za kiisimu.
Utafiti huu ulikusudia kujibu maswali yafuatayo: changamoto zipi zinazozuia usimilishaji wa ishara za kiisimu katika breili ya Kiswahili? Rasimu za Kiingereza na Kiswahili huathiriana kwa njia zipi? Ukosefu wa ishara za isimu katika breili huathiri ufundishaji wa isimu kwa njia gani? Na mwisho, mikato ya Kiswahili na ya Kiingereza inayotumia nukta zinazofanana huathiri uchapishaji wa vitabu vya isimu kwa njia zipi? Utafiti huu ulilenga kutimiza malengo yafuatayo – kwanza, kubainisha na kutatua changamoto zinazozuia usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili.
Pili, Kuchanganua rasimu ya Kiingereza na ya Kiswahili.
Aidha, kuchunguza athari ya ukosefu wa ishara hizi katika ufundishaji wa isimu.
Mwisho, kutathmini athari ya matumizi ya mikato inayotumia nukta zinazofanana katika uchapishaji wa vitabu vya isimu.
Makala haya yameshughulikia vikwazo vya usimilishaji wa ishara za isimu katika breili.
Mtafiti alitumia mbinu ya mahojiano katika kukusanya dataUtafiti huu ulichanganua usimilishaji wa ishara hizi kwa kuzingatia nadharia ya usomaji na uandishi wa breili iliyoasisiwa na Kizuka na Fuji (2005).
Mtafiti aligundua kuwa uchache wa nukta nundu umesababisha uradidi mwingi wa matumizi ya nukta nundu hizi.
Uradidi huu umechangia kuwepo kwa utata wa kimaana katika fonolojia na sintaksia ya Kiswahili, vikwazo vya ufundishaji wa isimu miongoni mwa wanafunzi wasioona, makosa katika vitabu vya sarufi hasa kidato cha kwanza na kidato cha pili na changamoto zinazotinga usimilishaji wa ishara za kiisimu katika Breili.
Utafiti huu utawafaidi wanafunzi wanaotumia breili na walimu na wahadhiri wanaofunza isimu.
Related Results
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Athari ya Mitindo Mbalimbali ya Breili katika Unukuzi wa Maandishi ya Breili ya Kiswahili
Athari ya Mitindo Mbalimbali ya Breili katika Unukuzi wa Maandishi ya Breili ya Kiswahili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usahihi wa unukuzi wa maandishi ya breili hadi maandishi ya kawaida na kinyume chake, ili kuleta maana iliyokusudiwa. Katika kutimiza lengo hilo, ut...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Upambanuzi wa Mikakati ya Kitashtiti katika Vibonzo vya Kisiasa Vya Gado
Upambanuzi wa Mikakati ya Kitashtiti katika Vibonzo vya Kisiasa Vya Gado
Taalumu ya uchoraji na uchapishaji wa vibonzo vya kisiasa umekuwepo tangu karne ya kumi na nane. Saana hii huwavutia watafiti wengi kutokana na uwezo wake wa kusimba jumbe zisizowe...
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulid...
Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo
Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo
Makala haya yanahusu uchanganuzi wa ruwaza za Toni katika Vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo. Lengo kuu la makala haya ni kuchunguza ruwaza ya ujitokezaji wa toni katika vite...
Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.
Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.
Makala hii inaonyesha tofauti iliyopo kati ya majukumu na maumbo ya uhusika katika vichwa vya habari vya siasa kwenye gazeti la Taifa Leo. Nadharia ya uhusika iliyoasisiwa na Charl...

