Javascript must be enabled to continue!
Upambanuzi wa Mikakati ya Kitashtiti katika Vibonzo vya Kisiasa Vya Gado
View through CrossRef
Taalumu ya uchoraji na uchapishaji wa vibonzo vya kisiasa umekuwepo tangu karne ya kumi na nane. Saana hii huwavutia watafiti wengi kutokana na uwezo wake wa kusimba jumbe zisizoweza kusemwa wazi wazi. Ifahamike kuwa sifa kuu ya vibonzo vya kisiasa ni kuwa vinapaswa kuwa cheshi na vyenye tashtiti ndiposa viweze kuwasilisha masuala tata kwa njia ya kimzaha. Kutokana na hali hii, utafiti huu ulichunguza tashtiti katika vibonzo vya kisiasa vya Gado vilivyochapishwa katika mwaka wa 2017 kwenye tovuti yake. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kupambanua mikakati iliyotumika katika kuendeleza maudhui ya kitashtiti katika vibonzo vilivyoteuliwa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Semiotiki iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure, na baadaye kuhakikiwa na Chandler na pia Wamitila. Mihimili ya nadharia hii ilitumika kuchambua mikakati iliyotumiwa na Gado katika vibonzo vyake kwa minajili ya kuendeleza maudhui ya kitashtiti. Utafiti huu ni wa kimaelezo na ulifanyika mtandaoni, pale ambapo mtafiti alipekua tovuti ya Gado (www.gadocartoons.com) na kuteua kimaksudi vibonzo vinane kutokana na jumla ya vibonzo ishirini vilivyokuwa vimechapishwa katika mwaka wa 2017. Uteuzi huu ulijikita katika vibonzo vilivyofungamana na madhumuni ya utafiti huu. Kwa jumla, utafiti huu ulidhibitisha kuwa mwanakibonzo Gado alitumia mbinu za lugha kama vile; kinaya, kejeli, metonimia, sitiara, analojia na mwingiliano matini kama mikakati ya kuibua kitashtiti katika vibonzo vyake. Vilevile, utafiti huu ulionyesha kuwa Gado alitumia ishara kama vile; matumizi ya rangi mbalimbali, pamoja na alama kama vile; heshtegi, mviringo na nyota kama mikakati ya kuibua tashtiti katika vibonzo vyake. Mwishowe, utafiti huu ulidhibitisha kuwa vibonzo vilivyochapishwa kwenye mtandao, vilidhihirisha uhuru na ukali mwingi katika usawiri wa masuala mbalimbali, jambo ambalo lilisaidia katika kufanikisha lengo kuu la tashtiti; ambalo ni ushambulizi unaochochea mabadiliko. Mwishowe, matokeo ya utafiti huu yalitarajiwa kuwanufaisha wanamawasiliano, wanasemiotiki na wasomi wa masuala ya kisiasa kwa kuwapa mtazamo mpya kuhusiana na matumizi ya maneno na ishara katika kusimba jumbe tata zinazochapishwa kwenye mtandao ambapo kuna uhuru mwingi wa kuelezea masuala tata bila kudhibitiwa.
East African Nature and Science Organization
Title: Upambanuzi wa Mikakati ya Kitashtiti katika Vibonzo vya Kisiasa Vya Gado
Description:
Taalumu ya uchoraji na uchapishaji wa vibonzo vya kisiasa umekuwepo tangu karne ya kumi na nane.
Saana hii huwavutia watafiti wengi kutokana na uwezo wake wa kusimba jumbe zisizoweza kusemwa wazi wazi.
Ifahamike kuwa sifa kuu ya vibonzo vya kisiasa ni kuwa vinapaswa kuwa cheshi na vyenye tashtiti ndiposa viweze kuwasilisha masuala tata kwa njia ya kimzaha.
Kutokana na hali hii, utafiti huu ulichunguza tashtiti katika vibonzo vya kisiasa vya Gado vilivyochapishwa katika mwaka wa 2017 kwenye tovuti yake.
Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kupambanua mikakati iliyotumika katika kuendeleza maudhui ya kitashtiti katika vibonzo vilivyoteuliwa.
Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Semiotiki iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure, na baadaye kuhakikiwa na Chandler na pia Wamitila.
Mihimili ya nadharia hii ilitumika kuchambua mikakati iliyotumiwa na Gado katika vibonzo vyake kwa minajili ya kuendeleza maudhui ya kitashtiti.
Utafiti huu ni wa kimaelezo na ulifanyika mtandaoni, pale ambapo mtafiti alipekua tovuti ya Gado (www.
gadocartoons.
com) na kuteua kimaksudi vibonzo vinane kutokana na jumla ya vibonzo ishirini vilivyokuwa vimechapishwa katika mwaka wa 2017.
Uteuzi huu ulijikita katika vibonzo vilivyofungamana na madhumuni ya utafiti huu.
Kwa jumla, utafiti huu ulidhibitisha kuwa mwanakibonzo Gado alitumia mbinu za lugha kama vile; kinaya, kejeli, metonimia, sitiara, analojia na mwingiliano matini kama mikakati ya kuibua kitashtiti katika vibonzo vyake.
Vilevile, utafiti huu ulionyesha kuwa Gado alitumia ishara kama vile; matumizi ya rangi mbalimbali, pamoja na alama kama vile; heshtegi, mviringo na nyota kama mikakati ya kuibua tashtiti katika vibonzo vyake.
Mwishowe, utafiti huu ulidhibitisha kuwa vibonzo vilivyochapishwa kwenye mtandao, vilidhihirisha uhuru na ukali mwingi katika usawiri wa masuala mbalimbali, jambo ambalo lilisaidia katika kufanikisha lengo kuu la tashtiti; ambalo ni ushambulizi unaochochea mabadiliko.
Mwishowe, matokeo ya utafiti huu yalitarajiwa kuwanufaisha wanamawasiliano, wanasemiotiki na wasomi wa masuala ya kisiasa kwa kuwapa mtazamo mpya kuhusiana na matumizi ya maneno na ishara katika kusimba jumbe tata zinazochapishwa kwenye mtandao ambapo kuna uhuru mwingi wa kuelezea masuala tata bila kudhibitiwa.
Related Results
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.
Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.
Makala hii inaonyesha tofauti iliyopo kati ya majukumu na maumbo ya uhusika katika vichwa vya habari vya siasa kwenye gazeti la Taifa Leo. Nadharia ya uhusika iliyoasisiwa na Charl...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo
Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo
Makala haya yanahusu uchanganuzi wa ruwaza za Toni katika Vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo. Lengo kuu la makala haya ni kuchunguza ruwaza ya ujitokezaji wa toni katika vite...
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulid...
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Swahili
Suala la upole limetafitiwa na wasomi wengi kwenye mawasiliano, ikiwemo mazungumzo ya abiria na wahudumu wa magari ya uchukuzi kwa lugha ya Kikamba. Hata hivyo, utafiti huu...

