Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.

View through CrossRef
Makala hii inaonyesha tofauti iliyopo kati ya majukumu na maumbo ya uhusika katika vichwa vya habari vya siasa kwenye gazeti la Taifa Leo. Nadharia ya uhusika iliyoasisiwa na Charles Fillmore mnamo mwaka wa 1968 imeongoza uchunguzi huu. Utafiti huu umefanywa baada ya kubaini kuwa wasomi mbalimbali wa gazeti hutafsili maana anuwai kwenye kichwa kimoja cha habari za siasa. Jambo hili husababisha utata wa kimaana na uenezaji wa jumbe zisizoithibatika katika jamii, hivyo basi, kuzalisha migogoro ya kisiasa nchini. Upekuzi wa yaliyomo kwenye matoleo ya gazeti la Taifa Leo ambayo yametawaliwa na vichwa vya habari za siasa na kuchapishwa kati ya mwaka 2017-2019 ni msingi wa data ya utafiti huu. Vichwa kumi na vinane vya habari za siasa vilisampulishwa kimakusudi na kutumika katika uchambuzi wa uchunguzi huu. Data katika makala hii imewasilishwa kupitia mfumo wa majedwali na maelezo. Matokeo ya tathmini ya uchunguzi huu yameshikilia kwamba Kiswahili hakina maumbo dhahiri ya uhusika ispokuwa katika nomino ambazo nafasi yake yaweza kuchukuliwa na viwakilishi vya nafsi ya pili na tatu umoja na wingi. Katika vichwa vya habari ambavyo nomino zake si za ngeli ya A-WA, viwakilishi faafu vya nomino hizo huchukua nafasi hiyo na kuwa maumbo ya uhusika. Kila aina ya uhusika ina jukumu lake la uhusika. Majukumu ya uhusika ni dhahania na hubadilika kulingana na aina ya uhusika. Uchunguzi huu utakuwa wenye umuhimu kwa wasomi wa magazeti na taifa kijumla. Wasomi wa magazeti wataongozwa na kigezo cha dhima ya maneno katika tungo kudondoa maana sawa katika vichwa lengwa vya habari za kisiasa na kupitisha tafsili hiyo moja kwa wanajamii. Kwa kufanya hivi, migogoro ya kisiasa katika jamii iletwayo na tafsili mbalimbali za kimaana itafutiliwa mbali.
Title: Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.
Description:
Makala hii inaonyesha tofauti iliyopo kati ya majukumu na maumbo ya uhusika katika vichwa vya habari vya siasa kwenye gazeti la Taifa Leo.
Nadharia ya uhusika iliyoasisiwa na Charles Fillmore mnamo mwaka wa 1968 imeongoza uchunguzi huu.
Utafiti huu umefanywa baada ya kubaini kuwa wasomi mbalimbali wa gazeti hutafsili maana anuwai kwenye kichwa kimoja cha habari za siasa.
Jambo hili husababisha utata wa kimaana na uenezaji wa jumbe zisizoithibatika katika jamii, hivyo basi, kuzalisha migogoro ya kisiasa nchini.
Upekuzi wa yaliyomo kwenye matoleo ya gazeti la Taifa Leo ambayo yametawaliwa na vichwa vya habari za siasa na kuchapishwa kati ya mwaka 2017-2019 ni msingi wa data ya utafiti huu.
Vichwa kumi na vinane vya habari za siasa vilisampulishwa kimakusudi na kutumika katika uchambuzi wa uchunguzi huu.
Data katika makala hii imewasilishwa kupitia mfumo wa majedwali na maelezo.
Matokeo ya tathmini ya uchunguzi huu yameshikilia kwamba Kiswahili hakina maumbo dhahiri ya uhusika ispokuwa katika nomino ambazo nafasi yake yaweza kuchukuliwa na viwakilishi vya nafsi ya pili na tatu umoja na wingi.
Katika vichwa vya habari ambavyo nomino zake si za ngeli ya A-WA, viwakilishi faafu vya nomino hizo huchukua nafasi hiyo na kuwa maumbo ya uhusika.
Kila aina ya uhusika ina jukumu lake la uhusika.
Majukumu ya uhusika ni dhahania na hubadilika kulingana na aina ya uhusika.
Uchunguzi huu utakuwa wenye umuhimu kwa wasomi wa magazeti na taifa kijumla.
Wasomi wa magazeti wataongozwa na kigezo cha dhima ya maneno katika tungo kudondoa maana sawa katika vichwa lengwa vya habari za kisiasa na kupitisha tafsili hiyo moja kwa wanajamii.
Kwa kufanya hivi, migogoro ya kisiasa katika jamii iletwayo na tafsili mbalimbali za kimaana itafutiliwa mbali.

Related Results

Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
Utafiti huu unahusu maudhui katika nyimbo teule kwenye vyombo vya habari, mfano ni nyimbo katika kipindi cha Rauka katika runinga ya Citizen. Utafiti ulichochewa na haja ya kutaka ...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Upambanuzi wa Mikakati ya Kitashtiti katika Vibonzo vya Kisiasa Vya Gado
Upambanuzi wa Mikakati ya Kitashtiti katika Vibonzo vya Kisiasa Vya Gado
Taalumu ya uchoraji na uchapishaji wa vibonzo vya kisiasa umekuwepo tangu karne ya kumi na nane. Saana hii huwavutia watafiti wengi kutokana na uwezo wake wa kusimba jumbe zisizowe...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulid...
Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo
Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo
Makala haya yanahusu uchanganuzi wa ruwaza za Toni katika Vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo. Lengo kuu la makala haya ni kuchunguza ruwaza ya ujitokezaji wa toni katika vite...

Back to Top