Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo

View through CrossRef
Makala haya yanahusu uchanganuzi wa ruwaza za Toni katika Vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo. Lengo kuu la makala haya ni kuchunguza ruwaza ya ujitokezaji wa toni katika vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo na kanuni zinazotawala utokeaji huo. Aidha, malengo mahususi: kubainisha silabi inayohusishwa na Tonijuu Msingi (kuanzia sasa TJM) na mbili, kujadili ruwaza ya utokeaji wa toni katika vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo na kanuni zinazotawala hutokeaji huo. Data ya Makala haya imetokana na utafiti mpana uliofanywa juu ya toni katika wilaya ya Rombo (2019) ambao   uliongozwa na Nadharia ya Fonolojia Vipandesauti Huru kwa kutumia Mkabala wa Tonijuu Msingi kama ulivyoasisiwa na Goldsmith (1976) na kuboreshwa na wanazuoni mbalimbali katika taaluma ya fonolojia. Aidha, mbinu za ukusanyaji data zilizotumika ni pamoja na mahojiano na ushuhudiaji. Katika mahojiano vitenzi visoukomo changamani viliandaliwa kwa Kiswahili na watoataarifa walihitajika kuvitamka kwa Kirombo huku mtafiti akirekodi na kualamisha toni katika vitenzi hivyo. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kuna ruwaza mbalimbali za kitoni zinazoleteleza utokeaji wa kanuni za kitoni ambazo hutofautiana kutegemeana na idadi ya silabi na uwapo au kutowapo kwa yambwa. Aidha, vitenzi visoukomo changamani vya silabi moja hutawaliwa na kanuni ya uhusishaji wa toni chini na vitamkwa na sharti la ukubalifu, wakati vitenzi visoukomo changamani vya silabi mbili hadi ama tano au sita za shina hutawaliwa na kanuni ya udondoshaji wa TJM pamoja na kanuni nyingine kitoni kama vile: kanuni ya msambao wa tonijuu kuelekea kulia mwa shina, uhamaji wa TJM kutoka silabi ya kwanza kwenda katika silabi ya pili ya shina, unakiliji wa TJM katika silabi ya mwisho kasoro moja. Aidha, TJM hupachikwa katika mofimu ya yambwa kwa vitenzi visoukomo changamani vya silabi moja ya shina. Pia, matokeo yanaonesha kwamba kuna TJM mbili, yaani, ya kwanza ni ya yambwa na ya pili ikiwa ya shina, ambapo katika mchakato wa ukokotozi wa uibuzi wa toni, TJM ya shina hudondoshwa kwa kuwa yambwa ina nguvu zaidi.  Makala haya yamesaidia kujua namna toni zinavyojitokeza katika vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo kwa ujumla.
East African Nature and Science Organization
Title: Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo
Description:
Makala haya yanahusu uchanganuzi wa ruwaza za Toni katika Vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo.
Lengo kuu la makala haya ni kuchunguza ruwaza ya ujitokezaji wa toni katika vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo na kanuni zinazotawala utokeaji huo.
Aidha, malengo mahususi: kubainisha silabi inayohusishwa na Tonijuu Msingi (kuanzia sasa TJM) na mbili, kujadili ruwaza ya utokeaji wa toni katika vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo na kanuni zinazotawala hutokeaji huo.
Data ya Makala haya imetokana na utafiti mpana uliofanywa juu ya toni katika wilaya ya Rombo (2019) ambao   uliongozwa na Nadharia ya Fonolojia Vipandesauti Huru kwa kutumia Mkabala wa Tonijuu Msingi kama ulivyoasisiwa na Goldsmith (1976) na kuboreshwa na wanazuoni mbalimbali katika taaluma ya fonolojia.
Aidha, mbinu za ukusanyaji data zilizotumika ni pamoja na mahojiano na ushuhudiaji.
Katika mahojiano vitenzi visoukomo changamani viliandaliwa kwa Kiswahili na watoataarifa walihitajika kuvitamka kwa Kirombo huku mtafiti akirekodi na kualamisha toni katika vitenzi hivyo.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kuna ruwaza mbalimbali za kitoni zinazoleteleza utokeaji wa kanuni za kitoni ambazo hutofautiana kutegemeana na idadi ya silabi na uwapo au kutowapo kwa yambwa.
Aidha, vitenzi visoukomo changamani vya silabi moja hutawaliwa na kanuni ya uhusishaji wa toni chini na vitamkwa na sharti la ukubalifu, wakati vitenzi visoukomo changamani vya silabi mbili hadi ama tano au sita za shina hutawaliwa na kanuni ya udondoshaji wa TJM pamoja na kanuni nyingine kitoni kama vile: kanuni ya msambao wa tonijuu kuelekea kulia mwa shina, uhamaji wa TJM kutoka silabi ya kwanza kwenda katika silabi ya pili ya shina, unakiliji wa TJM katika silabi ya mwisho kasoro moja.
Aidha, TJM hupachikwa katika mofimu ya yambwa kwa vitenzi visoukomo changamani vya silabi moja ya shina.
Pia, matokeo yanaonesha kwamba kuna TJM mbili, yaani, ya kwanza ni ya yambwa na ya pili ikiwa ya shina, ambapo katika mchakato wa ukokotozi wa uibuzi wa toni, TJM ya shina hudondoshwa kwa kuwa yambwa ina nguvu zaidi.
  Makala haya yamesaidia kujua namna toni zinavyojitokeza katika vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo kwa ujumla.

Related Results

Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Fonolojia ni taaluma iliyosheheni viarudhi au vipambasauti kama ambavyo wataalamu wengine huviita. Miongoni mwake ni toni, lafudhi, mkazo, nguvumsikiko, usilabi, kiimbo, unguvunguv...
Mnyambuliko wa Vitenzi Katika Lugha za Kiafrika: Mfano katika Lugha ya Kimasaaba Nchini Uganda
Mnyambuliko wa Vitenzi Katika Lugha za Kiafrika: Mfano katika Lugha ya Kimasaaba Nchini Uganda
Katika makala hii, mtafiti anaeleza jinsi vitenzi vya lugha za Kiafrika vinavyonyambuliwa na kuleta maana tofauti tofauti. Anafanya hivyo kwa kurejelea Kimasaaba ambayo ni lugha in...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulid...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...

Back to Top