Javascript must be enabled to continue!
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
View through CrossRef
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni kitabu mojawapo kikongwe cha fasihi ambacho huwasilisha taswira changamano kuhusu binadamu. Katika kitabu cha Mwanzo 1:26-27, lugha inayotumiwa katika Biblia Takatifu inatuchorea taswira kuhusu hadhi ya mwanamke na mwanamume kuinuliwa kwa pamoja kulingana na mpango asili uliopendekezwa na Mungu. Hata hivyo, kupitia hiyo Biblia Takatifu, tunakumbana na taswira changamano zinazowasilishwa kuhusu mwanamke. Hili huwezeshwa kupitia lugha. Ikumbukwe kuwa lugha inayotumika katika Biblia Takatifu ina athari kubwa katika uhalisia wa kijamii, ikizingatiwa kuwa idadi ya wakristo wanaozingatia mafunzo ya Biblia Takatifu ni wengi (bilioni 2.4). Utafiti huu unachanganua vipengele vya sanaa vinavyojenga taswira ya mwanamke katika vitabu teule vya Biblia Takatifu. Madhumuni yaliyoshughulikiwa ni Kwanza, kuchanganua maumbo ya fasihi yanayojenga taswira ya mwanamke katika vitabu teule vya Biblia Takatifu na pili, kudhihirisha maudhui yanayojitokeza katika maumbo yanayojenga taswira ya mwanamke katika vitabu teule vya Biblia Takatifu. Utafiti huu ulijikita tu kwa maumbo ya fasihi na maudhui yanayowasilishwa katika taswira ya mwanamke katika vitabu teule vya Biblia Takatifu, toleo la 2013. Utafiti ulizingatia mseto wa nadharia; nadharia ya Umuundo mpya iliyorejelewa na Crick (2016), nadharia ya Umaumbo ambayo ilirejelewa na MaryAnne (1999), na kiunzi cha nadharia ya Ufeministi kwa mujibu wa Wamitila (2003). Muundo wa kiuchanganuzi ulizingatiwa. Mbinu ya uchunzaji ilitumiwa kuufanikisha huu utafiti. Makala yanayodhihirisha taswira ya mwanamke katika Biblia Takatifu ndiyo yaliyodondolewa. Orodhahakiki ilitumiwa kudondoa data kutoka kwenye Biblia Takatifu ili kupata sampuli zifaazo za maumbo na maudhui. Usampulishaji dhamirifu ulitumiwa kwa kuongozwa na madhumuni ya utafiti huu. Utafiti umebaini kuwa maumbo ya fasihi yanayojenga taswira ya mwanamke katika Biblia Takatifu yanaibua maudhui hai, aidha yanayoishi katika jamii, hivyo, kuna uwezekano kuwa lugha katika Biblia Takatifu imeathiri jamii halisi kwa namna hasi na chanya. Utafiti unatarajiwa kuwafahamisha wanajamii na umma kwa jumla kuwa nafasi ya mwanamke ni muhimu katika kuendeleza jamii na utaweka wazi namna lugha katika Biblia Takatifu inavyoathiri mtazamo wa jamii halisi kumhusu mwanamke
East African Nature and Science Organization
Title: Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Description:
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii.
Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii.
Biblia Takatifu ni kitabu mojawapo kikongwe cha fasihi ambacho huwasilisha taswira changamano kuhusu binadamu.
Katika kitabu cha Mwanzo 1:26-27, lugha inayotumiwa katika Biblia Takatifu inatuchorea taswira kuhusu hadhi ya mwanamke na mwanamume kuinuliwa kwa pamoja kulingana na mpango asili uliopendekezwa na Mungu.
Hata hivyo, kupitia hiyo Biblia Takatifu, tunakumbana na taswira changamano zinazowasilishwa kuhusu mwanamke.
Hili huwezeshwa kupitia lugha.
Ikumbukwe kuwa lugha inayotumika katika Biblia Takatifu ina athari kubwa katika uhalisia wa kijamii, ikizingatiwa kuwa idadi ya wakristo wanaozingatia mafunzo ya Biblia Takatifu ni wengi (bilioni 2.
4).
Utafiti huu unachanganua vipengele vya sanaa vinavyojenga taswira ya mwanamke katika vitabu teule vya Biblia Takatifu.
Madhumuni yaliyoshughulikiwa ni Kwanza, kuchanganua maumbo ya fasihi yanayojenga taswira ya mwanamke katika vitabu teule vya Biblia Takatifu na pili, kudhihirisha maudhui yanayojitokeza katika maumbo yanayojenga taswira ya mwanamke katika vitabu teule vya Biblia Takatifu.
Utafiti huu ulijikita tu kwa maumbo ya fasihi na maudhui yanayowasilishwa katika taswira ya mwanamke katika vitabu teule vya Biblia Takatifu, toleo la 2013.
Utafiti ulizingatia mseto wa nadharia; nadharia ya Umuundo mpya iliyorejelewa na Crick (2016), nadharia ya Umaumbo ambayo ilirejelewa na MaryAnne (1999), na kiunzi cha nadharia ya Ufeministi kwa mujibu wa Wamitila (2003).
Muundo wa kiuchanganuzi ulizingatiwa.
Mbinu ya uchunzaji ilitumiwa kuufanikisha huu utafiti.
Makala yanayodhihirisha taswira ya mwanamke katika Biblia Takatifu ndiyo yaliyodondolewa.
Orodhahakiki ilitumiwa kudondoa data kutoka kwenye Biblia Takatifu ili kupata sampuli zifaazo za maumbo na maudhui.
Usampulishaji dhamirifu ulitumiwa kwa kuongozwa na madhumuni ya utafiti huu.
Utafiti umebaini kuwa maumbo ya fasihi yanayojenga taswira ya mwanamke katika Biblia Takatifu yanaibua maudhui hai, aidha yanayoishi katika jamii, hivyo, kuna uwezekano kuwa lugha katika Biblia Takatifu imeathiri jamii halisi kwa namna hasi na chanya.
Utafiti unatarajiwa kuwafahamisha wanajamii na umma kwa jumla kuwa nafasi ya mwanamke ni muhimu katika kuendeleza jamii na utaweka wazi namna lugha katika Biblia Takatifu inavyoathiri mtazamo wa jamii halisi kumhusu mwanamke.
Related Results
Uchunguzi wa Dhamira Zinazojengwa na Vipengele vya Sanaa katikaVisasuli vya Wahaya
Uchunguzi wa Dhamira Zinazojengwa na Vipengele vya Sanaa katikaVisasuli vya Wahaya
Sanaa ni sehemu muhimu ya maisha ya kila siku katika kabila la Wahaya. Umuhimu wa sanaa katika kabila la Wahaya unatokana na utajiri mkubwa walionao katika fasihi simulizi hususani...
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulid...
Usawiri wa Mwanamke wa Kisasa wa Kiislamu katika Filamu ya Maria.
Usawiri wa Mwanamke wa Kisasa wa Kiislamu katika Filamu ya Maria.
Swahili
Utafiti huu ulilenga kuchunguza usawiri wa mwanamke wa kisasa wa Kiislamu katika filamu ya Maria. Mada ya utafiti ilitokana na utanzu wa fasihi simulizi, ambapo drama, kama...
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jami...
Nafasi ya Riwaya za Kingano za Kiswahili katika Harakati za Kupigania Hadhi-Msingi ya Mwanamke. Mfano Riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba
Nafasi ya Riwaya za Kingano za Kiswahili katika Harakati za Kupigania Hadhi-Msingi ya Mwanamke. Mfano Riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba
Makala haya yanalenga kuonesha namna riwaya za kingano za Kiswahili zinavyoweza kutumika kumpigania na kumkomboa mtu mnyonge hususani mwanamke na mtoto. Baadhi ya watu wanadhani ng...
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Mafumbo ya mwanamke katika mashairi teule ya Muyaka
Mafumbo ya mwanamke katika mashairi teule ya Muyaka
Ikisiri
Azma kuu ya makala hii ni kuchanganua mafumbo ya mwanamke wa Kiswahili wa karne ya kumi na tisa katika ushairi wa Kiswahili wa kipindi hicho. Kwa kutumia mashairi teule ya ...
Nafasi Ya Fasihi Simulizi Katika Kuwasilisha Ujumbe Kisheria: Mfano wa Uendeshaji Kesi Za Kitamaduni Miongoni Mwa Babukusu
Nafasi Ya Fasihi Simulizi Katika Kuwasilisha Ujumbe Kisheria: Mfano wa Uendeshaji Kesi Za Kitamaduni Miongoni Mwa Babukusu
Utafiti uliazimia kubainisha nafasi ya Fasihi Simulizi katika kuwasilisha ujumbe kisheria. Ulionyesha namna vipengele bainifu vya Fasihi Simulizi vinaweza kutumika kuwasilisha ujum...

