Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Vipengele Vya Ontolojia Katika Tamthiliya Za Kiswahili: Mashetani (1971) Na Kivuli Kinaishi (1990).

View through CrossRef
Makala haya yalilenga kuchambua vipengele vya Ontolojia ya Kiafrika katika tamthiliya za Kiswahili: mfano wa Mashetani (1971) na Kivuli Kinaishi (1990). Mbinu iliyotumika katika kukusanya data hii ni mbinu ya kitaamuli. Sampuli iliyotumika katika makala haya ni vitabu viwili vya tamthiliya ambavyo ni Mashetani (1971) na Kivuli Kinaishi (1990). Tamthiliya hizi zitawakilisha zingine nyingi ambazo zimeandikwa na Ibrahimu Hussein na Said Mohamed. Mtafiti atajikita katika tamthiliya hizo mbili ili kuchambua vipengele vya ontolojia. Utafiti huu ulifanywa maktabani ambapo data ziliweza kukusanywa kwa kutumia mbinu ya udurusu maktaba. Mtafiti alipitia maandishi mbalimbali kutoka katika vitabu vilivyopo katika maktaba pamoja na wavuti ili kupata maelezo yaliyotosha kukidhi haja ya makala haya. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Ontolojia ambapo mtafiti aliitumia katika kuchambua vipengele vya ontolojia ya Kiafrika katika tamthiliya teule. Makala haya yatasaidia kuongeza uelewa kwa wanajamii hasa kwa wale wasiofahamu kuchambua masuala ya kiontolojia katika fasihi andishi. Kutokana na matokeo ya utafiti huu tumefikia mahitimisho kuwa vipengele vya ontolojia ya Kiafrika vilivyobainishwa kutoka katika tamthiliya ya Mashetani na Kivuli Kinaishi vimeweza kusawiri ontolojia ya Kiafrika na nafasi yake kwa jamii.
Title: Vipengele Vya Ontolojia Katika Tamthiliya Za Kiswahili: Mashetani (1971) Na Kivuli Kinaishi (1990).
Description:
Makala haya yalilenga kuchambua vipengele vya Ontolojia ya Kiafrika katika tamthiliya za Kiswahili: mfano wa Mashetani (1971) na Kivuli Kinaishi (1990).
Mbinu iliyotumika katika kukusanya data hii ni mbinu ya kitaamuli.
Sampuli iliyotumika katika makala haya ni vitabu viwili vya tamthiliya ambavyo ni Mashetani (1971) na Kivuli Kinaishi (1990).
Tamthiliya hizi zitawakilisha zingine nyingi ambazo zimeandikwa na Ibrahimu Hussein na Said Mohamed.
Mtafiti atajikita katika tamthiliya hizo mbili ili kuchambua vipengele vya ontolojia.
Utafiti huu ulifanywa maktabani ambapo data ziliweza kukusanywa kwa kutumia mbinu ya udurusu maktaba.
Mtafiti alipitia maandishi mbalimbali kutoka katika vitabu vilivyopo katika maktaba pamoja na wavuti ili kupata maelezo yaliyotosha kukidhi haja ya makala haya.
Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Ontolojia ambapo mtafiti aliitumia katika kuchambua vipengele vya ontolojia ya Kiafrika katika tamthiliya teule.
Makala haya yatasaidia kuongeza uelewa kwa wanajamii hasa kwa wale wasiofahamu kuchambua masuala ya kiontolojia katika fasihi andishi.
Kutokana na matokeo ya utafiti huu tumefikia mahitimisho kuwa vipengele vya ontolojia ya Kiafrika vilivyobainishwa kutoka katika tamthiliya ya Mashetani na Kivuli Kinaishi vimeweza kusawiri ontolojia ya Kiafrika na nafasi yake kwa jamii.

Related Results

Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu

Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Uchunguzi wa Dhamira Zinazojengwa na Vipengele vya Sanaa katikaVisasuli vya Wahaya
Uchunguzi wa Dhamira Zinazojengwa na Vipengele vya Sanaa katikaVisasuli vya Wahaya
Sanaa ni sehemu muhimu ya maisha ya kila siku katika kabila la Wahaya. Umuhimu wa sanaa katika kabila la Wahaya unatokana na utajiri mkubwa walionao katika fasihi simulizi hususani...
Usawiri wa Nafasi ya Mwanamke katika Tamthiliya ya Kiswahili "Tamthiliya ya Alikiona kama mfano"
Usawiri wa Nafasi ya Mwanamke katika Tamthiliya ya Kiswahili "Tamthiliya ya Alikiona kama mfano"
Makala hii inalenga kuchunguza usawiri wa nafasi ya mwanamke  katika tamthiliya ya Kiswahili "Tamthiliya ya Alikiona kama mfano" Katika kufanikisha lengo hili, tulichambua usawiri ...
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulid...

Back to Top