Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Uchunguzi wa Dhamira Zinazojengwa na Vipengele vya Sanaa katikaVisasuli vya Wahaya

View through CrossRef
Sanaa ni sehemu muhimu ya maisha ya kila siku katika kabila la Wahaya. Umuhimu wa sanaa katika kabila la Wahaya unatokana na utajiri mkubwa walionao katika fasihi simulizi hususani visasuli. Licha ya utajiri huo bado inaonesha kuwa maandiko mengi ya kisanaa na kihistoria hayakuandikwa hali iliyosababisha kutokuwapo kwa tafiti za kutosha kuhusu visasuli vya kabila la Wahaya. Makala hii imechunguza dhamira zinazojengwa na vipengele vya sanaa katika visasuli vya Wahaya. Sababu ya uchunguzi huu ni kwamba vipengele vya sanaa vimekuwa vikichunguzwa kwa ujumla sana katika kazi za fasihi bila ubayana unaoonesha namna vipengele hivyo vinavyojenga dhamira katika visasuli, hususani visasuli vya Wahaya. Data za makala hii zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano. Mjadala wa kimsingi katika Makala hii umekitwa na kuongozwa na Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji iliyoasisiwa na Wolfgang Iser (1978), Stanley Fish (1980) James Tompkins (1980), Haus Robert Jauss (1982) na Robert Holub (1984), katika ukusanyaji na uchambuzi wa data za makala hii. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa vipengele vya sanaa katika visasuli vya Wahaya vinatumika kujenga dhamira. Dhamira hizo ni pamoja na matumizi ya vifaa jadi wakati wa kula, kuonesha thamani ya kitu unachokimiliki, kuharibika kwa maadili, kuendeleza utamaduni, uzazi, mahari, na huruma kwa wahitaji.
Title: Uchunguzi wa Dhamira Zinazojengwa na Vipengele vya Sanaa katikaVisasuli vya Wahaya
Description:
Sanaa ni sehemu muhimu ya maisha ya kila siku katika kabila la Wahaya.
Umuhimu wa sanaa katika kabila la Wahaya unatokana na utajiri mkubwa walionao katika fasihi simulizi hususani visasuli.
Licha ya utajiri huo bado inaonesha kuwa maandiko mengi ya kisanaa na kihistoria hayakuandikwa hali iliyosababisha kutokuwapo kwa tafiti za kutosha kuhusu visasuli vya kabila la Wahaya.
Makala hii imechunguza dhamira zinazojengwa na vipengele vya sanaa katika visasuli vya Wahaya.
Sababu ya uchunguzi huu ni kwamba vipengele vya sanaa vimekuwa vikichunguzwa kwa ujumla sana katika kazi za fasihi bila ubayana unaoonesha namna vipengele hivyo vinavyojenga dhamira katika visasuli, hususani visasuli vya Wahaya.
Data za makala hii zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano.
Mjadala wa kimsingi katika Makala hii umekitwa na kuongozwa na Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji iliyoasisiwa na Wolfgang Iser (1978), Stanley Fish (1980) James Tompkins (1980), Haus Robert Jauss (1982) na Robert Holub (1984), katika ukusanyaji na uchambuzi wa data za makala hii.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa vipengele vya sanaa katika visasuli vya Wahaya vinatumika kujenga dhamira.
Dhamira hizo ni pamoja na matumizi ya vifaa jadi wakati wa kula, kuonesha thamani ya kitu unachokimiliki, kuharibika kwa maadili, kuendeleza utamaduni, uzazi, mahari, na huruma kwa wahitaji.

Related Results

Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulid...
Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.
Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.
Makala hii inaonyesha tofauti iliyopo kati ya majukumu na maumbo ya uhusika katika vichwa vya habari vya siasa kwenye gazeti la Taifa Leo. Nadharia ya uhusika iliyoasisiwa na Charl...
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Makala haya yalichunguza ujitokezaji wa ujumi wa Kiafrika katika ushairi wa Kiswahili wa Bongo Fleva pamoja na athari yake katika ushairi huo. Tafiti kuhusu vipengele vya ujumi wa ...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Mikabala Mbalimbali ya Uchanganuzi wa Sentensi Changamano za Kiswahili katika Vitabu vya Kiada vya Shule za Sekondari
Mikabala Mbalimbali ya Uchanganuzi wa Sentensi Changamano za Kiswahili katika Vitabu vya Kiada vya Shule za Sekondari
Rasimu ya mtalaa mpya wa elimu nchini Kenya imebaini vipengele anavyopaswa kuzingatishwa mwanafunzi ili kuimarisha uwezo na maarifa yake katika ujifunzaji wa Kiswahili. Hali hii im...
Utata wa Maudhui ya Kisarufi katika Vitabu vya Kiada vya Kiswahili Kidato cha Kwanza na cha Tatu Nchini Tanzania
Utata wa Maudhui ya Kisarufi katika Vitabu vya Kiada vya Kiswahili Kidato cha Kwanza na cha Tatu Nchini Tanzania
Vitabu vya kiada ni nyenzo muhimu katika ufundishaji wa somo la Kiswahili nchini Tanzania. Hutumika kama mwongozo wa ufundishaji wa mada zilizoteuliwa kwa kiwango husika cha elimu....
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Makala hii inalinganisha dhamira zilizowasilishwa kupitia wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili zilizoandikwa na wanawake wa Kenya na Tanzania. Tumaini (2006) ya Clara...

Back to Top