Javascript must be enabled to continue!
Mikabala Mbalimbali ya Uchanganuzi wa Sentensi Changamano za Kiswahili katika Vitabu vya Kiada vya Shule za Sekondari
View through CrossRef
Rasimu ya mtalaa mpya wa elimu nchini Kenya imebaini vipengele anavyopaswa kuzingatishwa mwanafunzi ili kuimarisha uwezo na maarifa yake katika ujifunzaji wa Kiswahili. Hali hii imetokana na mpango wa kufanyia mtaala wa elimu mabadiliko ili kumudu mahitaji ya jamii katika karne ya ishirini na moja. Silabasi ya sasa ya Kiswahili kwa shule za upili inaeleza kwa wazi vipengele vya kufundishwa katika sarufi na matumizi ya lugha. Sentensi ni mojawapo ya vipengele vya sarufi vinavyofundishwa katika shule za upili kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Kuna aina tatu kuu za sentensi kimuundo; miongoni mwazo ikiwa ni sentensi changamano Makala haya itaangazia aina hii ya sentensi kwa msingi wa uchanganuzi wake kutumia mikabala mbalimbali. Pengo lililopo ni kwamba vitabu vya kiada vilivyopendekezwa na Taasisi ya Ukuzaji wa Mtaala kisha kuidhinishwa na wizara ya elimu nchini; vimerejelea mada hii kwa mtazamo tofauti tofauti. Hali ambayo inazua mkanganyo na kuathiri mchakato wa ufunzaji na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi. Mada ya uchanganuzi wa sentensi inapasa kutiliwa msingi katika kidato cha kwanza na pili kisha kusisitizwa katika kidato cha tatu na nne. Kinyume na inavyojitokeza katika vitabu hivi vya kiada ambapo ufundishaji wa mada hii unaanzia kidato ha tatu na kukamilishwa katika kidato cha nne. Masebo (2002), anasema uchanganuzi wa sentensi ni kipengele cha sarufi miundo ambacho ni utanzu unaoshughulikia maneno katika tungo na uhusiano wa vipashio vyake. Ni muhimu mwanafunzi kupata mwelekeo faafu wa mada hii kwa kuelekezwa kwa njia na namna moja sio kwa kuhitilafiana. Lugha kando na kuwa ni chombo muhimu cha kujieleza, pia ina jukumu la kupitisha elimu faafu
East African Nature and Science Organization
Title: Mikabala Mbalimbali ya Uchanganuzi wa Sentensi Changamano za Kiswahili katika Vitabu vya Kiada vya Shule za Sekondari
Description:
Rasimu ya mtalaa mpya wa elimu nchini Kenya imebaini vipengele anavyopaswa kuzingatishwa mwanafunzi ili kuimarisha uwezo na maarifa yake katika ujifunzaji wa Kiswahili.
Hali hii imetokana na mpango wa kufanyia mtaala wa elimu mabadiliko ili kumudu mahitaji ya jamii katika karne ya ishirini na moja.
Silabasi ya sasa ya Kiswahili kwa shule za upili inaeleza kwa wazi vipengele vya kufundishwa katika sarufi na matumizi ya lugha.
Sentensi ni mojawapo ya vipengele vya sarufi vinavyofundishwa katika shule za upili kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.
Kuna aina tatu kuu za sentensi kimuundo; miongoni mwazo ikiwa ni sentensi changamano Makala haya itaangazia aina hii ya sentensi kwa msingi wa uchanganuzi wake kutumia mikabala mbalimbali.
Pengo lililopo ni kwamba vitabu vya kiada vilivyopendekezwa na Taasisi ya Ukuzaji wa Mtaala kisha kuidhinishwa na wizara ya elimu nchini; vimerejelea mada hii kwa mtazamo tofauti tofauti.
Hali ambayo inazua mkanganyo na kuathiri mchakato wa ufunzaji na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi.
Mada ya uchanganuzi wa sentensi inapasa kutiliwa msingi katika kidato cha kwanza na pili kisha kusisitizwa katika kidato cha tatu na nne.
Kinyume na inavyojitokeza katika vitabu hivi vya kiada ambapo ufundishaji wa mada hii unaanzia kidato ha tatu na kukamilishwa katika kidato cha nne.
Masebo (2002), anasema uchanganuzi wa sentensi ni kipengele cha sarufi miundo ambacho ni utanzu unaoshughulikia maneno katika tungo na uhusiano wa vipashio vyake.
Ni muhimu mwanafunzi kupata mwelekeo faafu wa mada hii kwa kuelekezwa kwa njia na namna moja sio kwa kuhitilafiana.
Lugha kando na kuwa ni chombo muhimu cha kujieleza, pia ina jukumu la kupitisha elimu faafu.
Related Results
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili
Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Utata wa Maudhui ya Kisarufi katika Vitabu vya Kiada vya Kiswahili Kidato cha Kwanza na cha Tatu Nchini Tanzania
Utata wa Maudhui ya Kisarufi katika Vitabu vya Kiada vya Kiswahili Kidato cha Kwanza na cha Tatu Nchini Tanzania
Vitabu vya kiada ni nyenzo muhimu katika ufundishaji wa somo la Kiswahili nchini Tanzania. Hutumika kama mwongozo wa ufundishaji wa mada zilizoteuliwa kwa kiwango husika cha elimu....
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulid...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...

