Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu

View through CrossRef
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika ngazi ya kitaifa nchini Kenya ambapo mfumo wa elimu wa 8-4-4 unaondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na mtaala wa umilisi (CBC). Mabadiliko haya yamejikita katika elimu ya msingi, kuanzia kiwango cha chekechea, shule za upili hadi kwenye vyuo vinavyotoa elimu ya kiufundi kote nchini. Kwa sasa, mabadiliko katika mtaala wa kitaifa hayajaathiri vyuo vikuu kunakotolewa elimu ya juu. Hata hivyo, wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu huandaliwa kupitia kwa mafunzo ya shule za upili. Hivyo basi mabadiliko yoyote yanayotokea katika elimu ya msingi lazima yataathiri programu za mafunzo yanayotolewa katika vyuo vikuu. Makala haya yataangazia kipengele cha tathmini katika vyuo vikuu kwa kuzingatia mabadiliko katika mfumo wa elimu uliopo na vigezo vinavyoelekeza tathmini katika mfumo wa elimu wa umilisi. Mabadiliko katika tathmini katika mfumo wa elimu wa umilisi yanaashiria kuwepo haja ya kufanya mabadiliko sawia ya tathmini katika mafunzo ya elimu ya juu katika vyuo vikuu. Hali hii inatokea kuwa hivi kwa kuwa wanafunzi wanapojiunga na vyuo vikuu watakuwa wamezoeshwa tathmini ya shule za upili ambayo hufanyika katika kila hatua ya ujifunzaji mafunzo yanapoendelea tofauti na illivyokuwa awali ambapo tathmini ilifanyika mara moja mwishoni baada ya kipindi maalumu cha mafunzo (mwishoni mwa miaka minane katika shule za msingi na miaka minne katika shule za upili). Swali hapa ni je, tathmini ya awali iliyozoeleka na ambayo ilifanyika baada ya kipindi maalumu bado itafaa? Bado itafikia malengo yaliyopo ya elimu? Kufikia sasa, hakuna mwelekeo wowote ambao umetolewa kuhusiana na hili. Hali hii inapelekea kuwepo haja ya kubuni sera itakayotoa mwelekeo kuhusu vigezo vinavyofaa kuzingatiwa katika kubadili tathmini katika vyuo vikuu ili iendane na mabadiliko yanayoendelea kutokea katika mfumo wa elimu uliopo. Mabadiliko katika tathmini vyuoni yanaweza kufanyika kwa kulinganisha na kulinganua tathmini iliyokuwepo awali na iliyopo hivi sasa katika elimu ya msingi na vyuo vikuu. Makala haya yamechanganua changamoto zinazotokana na hiyo mifumo miwili ya tathmini na kuangazia namna ambavyo aina zote mbili za tathmini humwathiri mwanafunzi ambaye ndiye mwathiriwa mkuu. Makala haya yamelenga kuwezesha vyuo vikuu kutambua mielekeo na mitazamo ambayo wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga navyo huingia nayo vyuoni kutokana na namna wanavyotathminiwa wanapopokea elimu ya msingi. Makala haya yametokana na uchambuzi na mapitio ya maandishi yaliyopo tayari kuhusu mifumo hii miwili ya elimu pamoja na maoni ya wataalamu wa masuala ya mitaala. Maandishi haya yalipatikana maktabani na mitandaoni.
East African Nature and Science Organization
Title: Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Description:
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu.
Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika ngazi ya kitaifa nchini Kenya ambapo mfumo wa elimu wa 8-4-4 unaondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na mtaala wa umilisi (CBC).
Mabadiliko haya yamejikita katika elimu ya msingi, kuanzia kiwango cha chekechea, shule za upili hadi kwenye vyuo vinavyotoa elimu ya kiufundi kote nchini.
Kwa sasa, mabadiliko katika mtaala wa kitaifa hayajaathiri vyuo vikuu kunakotolewa elimu ya juu.
Hata hivyo, wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu huandaliwa kupitia kwa mafunzo ya shule za upili.
Hivyo basi mabadiliko yoyote yanayotokea katika elimu ya msingi lazima yataathiri programu za mafunzo yanayotolewa katika vyuo vikuu.
Makala haya yataangazia kipengele cha tathmini katika vyuo vikuu kwa kuzingatia mabadiliko katika mfumo wa elimu uliopo na vigezo vinavyoelekeza tathmini katika mfumo wa elimu wa umilisi.
Mabadiliko katika tathmini katika mfumo wa elimu wa umilisi yanaashiria kuwepo haja ya kufanya mabadiliko sawia ya tathmini katika mafunzo ya elimu ya juu katika vyuo vikuu.
Hali hii inatokea kuwa hivi kwa kuwa wanafunzi wanapojiunga na vyuo vikuu watakuwa wamezoeshwa tathmini ya shule za upili ambayo hufanyika katika kila hatua ya ujifunzaji mafunzo yanapoendelea tofauti na illivyokuwa awali ambapo tathmini ilifanyika mara moja mwishoni baada ya kipindi maalumu cha mafunzo (mwishoni mwa miaka minane katika shule za msingi na miaka minne katika shule za upili).
Swali hapa ni je, tathmini ya awali iliyozoeleka na ambayo ilifanyika baada ya kipindi maalumu bado itafaa? Bado itafikia malengo yaliyopo ya elimu? Kufikia sasa, hakuna mwelekeo wowote ambao umetolewa kuhusiana na hili.
Hali hii inapelekea kuwepo haja ya kubuni sera itakayotoa mwelekeo kuhusu vigezo vinavyofaa kuzingatiwa katika kubadili tathmini katika vyuo vikuu ili iendane na mabadiliko yanayoendelea kutokea katika mfumo wa elimu uliopo.
Mabadiliko katika tathmini vyuoni yanaweza kufanyika kwa kulinganisha na kulinganua tathmini iliyokuwepo awali na iliyopo hivi sasa katika elimu ya msingi na vyuo vikuu.
Makala haya yamechanganua changamoto zinazotokana na hiyo mifumo miwili ya tathmini na kuangazia namna ambavyo aina zote mbili za tathmini humwathiri mwanafunzi ambaye ndiye mwathiriwa mkuu.
Makala haya yamelenga kuwezesha vyuo vikuu kutambua mielekeo na mitazamo ambayo wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga navyo huingia nayo vyuoni kutokana na namna wanavyotathminiwa wanapopokea elimu ya msingi.
Makala haya yametokana na uchambuzi na mapitio ya maandishi yaliyopo tayari kuhusu mifumo hii miwili ya elimu pamoja na maoni ya wataalamu wa masuala ya mitaala.
Maandishi haya yalipatikana maktabani na mitandaoni.

Related Results

Mikabala Mbalimbali ya Uchanganuzi wa Sentensi Changamano za Kiswahili katika Vitabu vya Kiada vya Shule za Sekondari
Mikabala Mbalimbali ya Uchanganuzi wa Sentensi Changamano za Kiswahili katika Vitabu vya Kiada vya Shule za Sekondari
Rasimu ya mtalaa mpya wa elimu nchini Kenya imebaini vipengele anavyopaswa kuzingatishwa mwanafunzi ili kuimarisha uwezo na maarifa yake katika ujifunzaji wa Kiswahili. Hali hii im...
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Fonolojia ni taaluma iliyosheheni viarudhi au vipambasauti kama ambavyo wataalamu wengine huviita. Miongoni mwake ni toni, lafudhi, mkazo, nguvumsikiko, usilabi, kiimbo, unguvunguv...
Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda
Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda
Umahiri wa kuzungumza lugha ni miongoni mwa matokeo yanayotarajiwa kutoka kwa mtu yeyote anayejifunza lugha ya kigeni au lugha ya pili. Mathalani nchini Uganda imebainika kuwa kiwa...
Maoni ya wanafunzi wa taasisi za kiufundi za kitaifa kuhusu nafasi ya Kiswahili katika elimu ya ufundi nchini Kenya
Maoni ya wanafunzi wa taasisi za kiufundi za kitaifa kuhusu nafasi ya Kiswahili katika elimu ya ufundi nchini Kenya
Utafiti huu ulinuia kutafuta maoni ya wanafunzi wa taasisi za kiufundi za kitaifa kuhusu nafasi ya lugha ya Kiswahili katika elimu ya kiufundi. Muundo wa Uchunguzi Kimaelezo ulitum...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo
Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo
Makala haya yanahusu uchanganuzi wa ruwaza za Toni katika Vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo. Lengo kuu la makala haya ni kuchunguza ruwaza ya ujitokezaji wa toni katika vite...
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Msingi wa makala haya ni “Sera ya Elimu na Mafunzo” (SEM, 2014). Makala yanahakiki nafasi ya lugha ya Kiswahili kwenye Sera ya Elimu na Mafunzo nchini Tanzania na mustakabali wake ...

Back to Top