Javascript must be enabled to continue!
Maoni ya wanafunzi wa taasisi za kiufundi za kitaifa kuhusu nafasi ya Kiswahili katika elimu ya ufundi nchini Kenya
View through CrossRef
Utafiti huu ulinuia kutafuta maoni ya wanafunzi wa taasisi za kiufundi za kitaifa kuhusu nafasi ya lugha ya Kiswahili katika elimu ya kiufundi. Muundo wa Uchunguzi Kimaelezo ulitumiwa, huku taasisi 5 za kiufundi za kitaifa na sampuli ya wanafunzi 148 na wakufunzi 20 wakishirikishwa katika utafiti. Aidha, utafiti huu ulitumia hojaji na mahojiano kukusanya data. Mbinu ya Yaliyomo Mchanganuo ilitumiwa kuchanganua data. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha kuwa lugha ya Kiswahili huchukua nafasi kuu katika mtaala wa elimu ya ufundi katika taasisi za kiufundi za kitaifa nchini. Kwa sasa, Kiswahili sio lugha ya ufundishaji katika taasisi hizi, ila hutumiwa na wakufunzi wa kozi mbalimbali kudadavua dhana tata, hasa miongoni mwa wanafunzi wa astashahada. Pia, utafiti huu zaidi uligundua kuwa Kiswahili ni lugha ya mawasiliano kwa wanafunzi wengi. Kutokana na majukumu haya yaliyodokezwa na wasailiwa, utafiti unapendekeza kwa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayanzi na Teknolojia (MOHEST), ikishirikiana Taasisi ya Ukuzaji Mitaala (KICD) kubuni mkakati wa kuanzisha ufundishaji wa lugha ya Kiswahili kama somo katika taasisi za ufundi nchini. Kwa kufanya hivyo, taasisi tajwa zitakuwa zikihimilisha dhima za kiakademia na kijamii ambazo hutekelezwa na Kiswahili katika mtaala wa elimu ya ufundi. Utafiti zaidi unaweza kulinganisha na kulinganua mielekeo ya wanafunzi wa taasisi za ufundi kuhusu Kiswahili na Kiingereza kama lugha ya kutoa mafunzo miongoni mwa wanafunzi wa astashahada.
Title: Maoni ya wanafunzi wa taasisi za kiufundi za kitaifa kuhusu nafasi ya Kiswahili katika elimu ya ufundi nchini Kenya
Description:
Utafiti huu ulinuia kutafuta maoni ya wanafunzi wa taasisi za kiufundi za kitaifa kuhusu nafasi ya lugha ya Kiswahili katika elimu ya kiufundi.
Muundo wa Uchunguzi Kimaelezo ulitumiwa, huku taasisi 5 za kiufundi za kitaifa na sampuli ya wanafunzi 148 na wakufunzi 20 wakishirikishwa katika utafiti.
Aidha, utafiti huu ulitumia hojaji na mahojiano kukusanya data.
Mbinu ya Yaliyomo Mchanganuo ilitumiwa kuchanganua data.
Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha kuwa lugha ya Kiswahili huchukua nafasi kuu katika mtaala wa elimu ya ufundi katika taasisi za kiufundi za kitaifa nchini.
Kwa sasa, Kiswahili sio lugha ya ufundishaji katika taasisi hizi, ila hutumiwa na wakufunzi wa kozi mbalimbali kudadavua dhana tata, hasa miongoni mwa wanafunzi wa astashahada.
Pia, utafiti huu zaidi uligundua kuwa Kiswahili ni lugha ya mawasiliano kwa wanafunzi wengi.
Kutokana na majukumu haya yaliyodokezwa na wasailiwa, utafiti unapendekeza kwa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayanzi na Teknolojia (MOHEST), ikishirikiana Taasisi ya Ukuzaji Mitaala (KICD) kubuni mkakati wa kuanzisha ufundishaji wa lugha ya Kiswahili kama somo katika taasisi za ufundi nchini.
Kwa kufanya hivyo, taasisi tajwa zitakuwa zikihimilisha dhima za kiakademia na kijamii ambazo hutekelezwa na Kiswahili katika mtaala wa elimu ya ufundi.
Utafiti zaidi unaweza kulinganisha na kulinganua mielekeo ya wanafunzi wa taasisi za ufundi kuhusu Kiswahili na Kiingereza kama lugha ya kutoa mafunzo miongoni mwa wanafunzi wa astashahada.
Related Results
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili
Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika ...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili

Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...