Javascript must be enabled to continue!
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
View through CrossRef
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo kwa kila mwanafunzi unapofika, wanafunzi huwa na sababu za kimsingi zinazowafanya wapendelee masomo fulani na kuyakataa mengine. Kwa kawaida wanafunzi huwa hawalazimishwi kuchukua masomo fulani. Kila mwanafunzi huwa na uhuru wa kuchagua masomo anayoyapenda. Imebainika wazi kuwa nchini Uganda, wakati wa wanafunzi kupunguza idadi ya masomo unapofika, wengi wao huwa wanaacha somo la Kiswahili. Katika darasa la wanafunzi mia moja, ni wanafunzi kumi au kumi na watano tu ndio wanachukua Kiswahili. Hali hii inatisha sana hasa kwa wapenzi wa Kiswahili. Hivyo basi, mtafiti aliendeleza utafiti huu ili kueleza sababu zinazopelekea wanafunzi kufanya hivyo. Dhamira ya utafiti ni kueleza bayana kwa nini wanafunzi wengi nchini Uganda huwa hawachukui somo la Kiswahili. Madhumuni ya utafiti huu ni kueleza mielekeo ya wanafunzi wa shule za sekondari nchini Uganda dhidi ya ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili na kufafanua hatua ambazo zinastahili kuchukuliwa ili kufanya idadi ya wanafunzi wa Kiswahili iongezeke. Katika kazi hii, mkabala wa utafiti ulikuwa wa nyanjani. Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alizuru nyanjani na kuendeleza mahojiano na wahojiwa wake. Utafiti huu umeonyesha kuwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini Uganda huwa hawapendelei somo la Kiswahili kwa sababu zifuatazo: kuwepo na sera mbovu nchini kuhusu lugha ya Kiswahili; wanafunzi kutokuwa na msingi wa lugha ya Kiswahili; wanafunzi kuwa na fikra potovu kuwa Kiswahili ni lugha ya wezi; wanafunzi kufikiria kuwa Kiswahili ni somo linalofaa wenzao kutoka Kenya na Tanzania; wanafunzi kufikiria kuwa lugha ya Kiswahili ni ngumu; watu wa nchi ya Uganda kuchukulia Kiswahili kuwa lugha ya kawaida na isiyofaa kufundishwa shuleni; wananchi wa Uganda kupendelea Kiganda na Kiingereza na kupiga vita lugha ya Kiswahili.
East African Nature and Science Organization
Title: Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Description:
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili.
Wakati wa kupunguza idadi ya masomo kwa kila mwanafunzi unapofika, wanafunzi huwa na sababu za kimsingi zinazowafanya wapendelee masomo fulani na kuyakataa mengine.
Kwa kawaida wanafunzi huwa hawalazimishwi kuchukua masomo fulani.
Kila mwanafunzi huwa na uhuru wa kuchagua masomo anayoyapenda.
Imebainika wazi kuwa nchini Uganda, wakati wa wanafunzi kupunguza idadi ya masomo unapofika, wengi wao huwa wanaacha somo la Kiswahili.
Katika darasa la wanafunzi mia moja, ni wanafunzi kumi au kumi na watano tu ndio wanachukua Kiswahili.
Hali hii inatisha sana hasa kwa wapenzi wa Kiswahili.
Hivyo basi, mtafiti aliendeleza utafiti huu ili kueleza sababu zinazopelekea wanafunzi kufanya hivyo.
Dhamira ya utafiti ni kueleza bayana kwa nini wanafunzi wengi nchini Uganda huwa hawachukui somo la Kiswahili.
Madhumuni ya utafiti huu ni kueleza mielekeo ya wanafunzi wa shule za sekondari nchini Uganda dhidi ya ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili na kufafanua hatua ambazo zinastahili kuchukuliwa ili kufanya idadi ya wanafunzi wa Kiswahili iongezeke.
Katika kazi hii, mkabala wa utafiti ulikuwa wa nyanjani.
Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alizuru nyanjani na kuendeleza mahojiano na wahojiwa wake.
Utafiti huu umeonyesha kuwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini Uganda huwa hawapendelei somo la Kiswahili kwa sababu zifuatazo: kuwepo na sera mbovu nchini kuhusu lugha ya Kiswahili; wanafunzi kutokuwa na msingi wa lugha ya Kiswahili; wanafunzi kuwa na fikra potovu kuwa Kiswahili ni lugha ya wezi; wanafunzi kufikiria kuwa Kiswahili ni somo linalofaa wenzao kutoka Kenya na Tanzania; wanafunzi kufikiria kuwa lugha ya Kiswahili ni ngumu; watu wa nchi ya Uganda kuchukulia Kiswahili kuwa lugha ya kawaida na isiyofaa kufundishwa shuleni; wananchi wa Uganda kupendelea Kiganda na Kiingereza na kupiga vita lugha ya Kiswahili.
Related Results
Changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika shule za sekondari za umma Tanzania: mfano wa shule teule za sekondari Wilaya ya Kwimba
Changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika shule za sekondari za umma Tanzania: mfano wa shule teule za sekondari Wilaya ya Kwimba
Ufaulu wa somo la Kiswahili kwa shule za sekondari za umma za Wilaya ya Kwimba ni hafifu ukilinganishwa na ufaulu wa somo hilo kitaifa. Hali hii ilibua mabunio ya kuwa huenda kuna ...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili
Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda
Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda
Umahiri wa kuzungumza lugha ni miongoni mwa matokeo yanayotarajiwa kutoka kwa mtu yeyote anayejifunza lugha ya kigeni au lugha ya pili. Mathalani nchini Uganda imebainika kuwa kiwa...
Teknolojia ibuka na ufundishaji wa somo la Kiswahili
Teknolojia ibuka na ufundishaji wa somo la Kiswahili
Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuchanganua teknolojia ibuka na ufundishaji wa somo la Kiswahili. Katika sekta mbalimbali kama vile afya, benki, biashara, usafiri, utawala, ki...
Maoni ya wanafunzi wa taasisi za kiufundi za kitaifa kuhusu nafasi ya Kiswahili katika elimu ya ufundi nchini Kenya
Maoni ya wanafunzi wa taasisi za kiufundi za kitaifa kuhusu nafasi ya Kiswahili katika elimu ya ufundi nchini Kenya
Utafiti huu ulinuia kutafuta maoni ya wanafunzi wa taasisi za kiufundi za kitaifa kuhusu nafasi ya lugha ya Kiswahili katika elimu ya kiufundi. Muundo wa Uchunguzi Kimaelezo ulitum...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza namna ambavyo Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa kwa nchi ya Uganda. Ni kweli kwamba nchini Uganda, watu kadhaa wakiwemo baadhi ya wanasiasa ha...

