Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika shule za sekondari za umma Tanzania: mfano wa shule teule za sekondari Wilaya ya Kwimba

View through CrossRef
Ufaulu wa somo la Kiswahili kwa shule za sekondari za umma za Wilaya ya Kwimba ni hafifu ukilinganishwa na ufaulu wa somo hilo kitaifa. Hali hii ilibua mabunio ya kuwa huenda kuna changamoto katika ufundishaji na ujifunzaji zinazosababisha matokeo mabaya ya somo la Kiswahili kwa shule za wilaya hiyo. Hivyo, makala hii inachunguza changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika shule za sekondari za umma zinazoweza kuwa sababu ya ufaulu hafifu wa somo hili. Utafiti ulioibua makala hii ulihusisha shule tatu za sekondari za umma. Kwa kuongozwa na Nadharia ya Utekelezaji Mtaala (Gross, 1971) na mkabala wa kitaamuli, makala inabainisha changamoto zinazokabili ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Kiswahili zinazohusu lugha, miundombinu, taaluma/ujuzi, mtazamo hasi kwa Kiswahili, kimazingira na mamlaka. Aidha, mapendekezo ya kutatua changamoto hizo yametolewa kulingana na tafsiri ya data za makala ili kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika shule za sekondari za umma za Wilaya ya Kwimba.
Title: Changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika shule za sekondari za umma Tanzania: mfano wa shule teule za sekondari Wilaya ya Kwimba
Description:
Ufaulu wa somo la Kiswahili kwa shule za sekondari za umma za Wilaya ya Kwimba ni hafifu ukilinganishwa na ufaulu wa somo hilo kitaifa.
Hali hii ilibua mabunio ya kuwa huenda kuna changamoto katika ufundishaji na ujifunzaji zinazosababisha matokeo mabaya ya somo la Kiswahili kwa shule za wilaya hiyo.
Hivyo, makala hii inachunguza changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika shule za sekondari za umma zinazoweza kuwa sababu ya ufaulu hafifu wa somo hili.
Utafiti ulioibua makala hii ulihusisha shule tatu za sekondari za umma.
Kwa kuongozwa na Nadharia ya Utekelezaji Mtaala (Gross, 1971) na mkabala wa kitaamuli, makala inabainisha changamoto zinazokabili ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Kiswahili zinazohusu lugha, miundombinu, taaluma/ujuzi, mtazamo hasi kwa Kiswahili, kimazingira na mamlaka.
Aidha, mapendekezo ya kutatua changamoto hizo yametolewa kulingana na tafsiri ya data za makala ili kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika shule za sekondari za umma za Wilaya ya Kwimba.

Related Results

Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika ...

Back to Top