Javascript must be enabled to continue!
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
View through CrossRef
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidijitali hutumia maneno ya Kiingereza – hata bila utohozi – wanapozungumzia haki za kiteknolojia. Hali hii ya mambo inachangia udhoofu fulani katika utetezi wa haki za kidijitali kwani wanaojaribu kueleza jamii umuhimu wa haki hizi hulazimishwa kutegemea msamiati wa Kiingereza usiyo na msingi au viungo na lugha ya Kiswahili Katika makala hii, tutazungumzia umuhimu wa kukaribisha watu kutumia lugha za Kiafrika kwenye mtandao.
Design/methodology/approach
Kiswahili ni lugha ya Kiafrika inayozungumzwa katika eneo zaidi sana duniani. Karibu watu milioni mia moja na arobaini Afrika mashariki wanazungumza Kiswahili kama lugha yao ya kwanza au ya pili, miongoni mwao Wakenya na Watanzania, wenyeji wa nchi ambamo Kiswahili ni lugha ya kitaifa. Tena kuna historia ndefu ya kutumiwa kwa lugha ya Kiswahili katika uandishi, uchapishaji na ubunifu wa utamaduni wa kisasa. Kiswahili pekee yake ndiyo lugha ya asili ya Kiafrika inayotumika kama lugha ya maalum ya Umoja wa Mataifa za Kiafrika. Hata hivyo, kwa upande wa matumizi ya Kiswahili, hasa kwenye mada ya teknolojia, Kiswahili imewachwa nyuma.
Findings
Zaidi ya maneno rasmi, uwepo wa lugha za Kiafrika ni muhimu kuimarisha jumuiya za Kiafrika mtandaoni kwani lugha inalenga sana haki na utambulisho wa watu. Miradi za kutafsiri maneno za kiteknolojia katika lugha ya Kiswahili inahimiza jumuiya za Afrika Mashariki kuunda jamii inayosimamia matakwa yao vyema. Makala hii basi inazingatia umuhimu wa lugha kwenye kuunda jamii na katika hatua za kuondoa mbinu za kikoloni mtandaoni ili wenyeji wa Afrika Mashariki wajione mtandaoni kwa ujumla wao wote. Makala pia itazingatia semiotiki ya lugha katika ubunifu wa teknolojia, na umuhimu wa kutafsiri jamii ya lugha ya Kiswahili katika harakati za kuondoa ukoloni katika ubunifu huu. Lakini sio tu kwamba lugha ya Kiswahili ndio pekee inayoweza kuondoa mbinu za kikoloni mtandaoni, kwani pia lugha hiyo ina ishara za kutawalwa kwa jamii fulani. Bali makala hii inatumia mfano wa Kiswahili kuhimiza utumiaji wa lugha za kiasili au za kimama mtandaoni ili kulinda mustakabali wa kidijitali wa umma.
Originality/value
Umuhimu wa makala hii ni kuashiria jipya umuhimu wa lugha katika harakati za kuendeleza haki za kidijitali na hasa kuondoa mbinu za kikoloni kwenye teknolojia, swala lisilowahijadiliwa katika lugha ya Kiswahili.
Title: Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Description:
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili.
Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidijitali hutumia maneno ya Kiingereza – hata bila utohozi – wanapozungumzia haki za kiteknolojia.
Hali hii ya mambo inachangia udhoofu fulani katika utetezi wa haki za kidijitali kwani wanaojaribu kueleza jamii umuhimu wa haki hizi hulazimishwa kutegemea msamiati wa Kiingereza usiyo na msingi au viungo na lugha ya Kiswahili Katika makala hii, tutazungumzia umuhimu wa kukaribisha watu kutumia lugha za Kiafrika kwenye mtandao.
Design/methodology/approach
Kiswahili ni lugha ya Kiafrika inayozungumzwa katika eneo zaidi sana duniani.
Karibu watu milioni mia moja na arobaini Afrika mashariki wanazungumza Kiswahili kama lugha yao ya kwanza au ya pili, miongoni mwao Wakenya na Watanzania, wenyeji wa nchi ambamo Kiswahili ni lugha ya kitaifa.
Tena kuna historia ndefu ya kutumiwa kwa lugha ya Kiswahili katika uandishi, uchapishaji na ubunifu wa utamaduni wa kisasa.
Kiswahili pekee yake ndiyo lugha ya asili ya Kiafrika inayotumika kama lugha ya maalum ya Umoja wa Mataifa za Kiafrika.
Hata hivyo, kwa upande wa matumizi ya Kiswahili, hasa kwenye mada ya teknolojia, Kiswahili imewachwa nyuma.
Findings
Zaidi ya maneno rasmi, uwepo wa lugha za Kiafrika ni muhimu kuimarisha jumuiya za Kiafrika mtandaoni kwani lugha inalenga sana haki na utambulisho wa watu.
Miradi za kutafsiri maneno za kiteknolojia katika lugha ya Kiswahili inahimiza jumuiya za Afrika Mashariki kuunda jamii inayosimamia matakwa yao vyema.
Makala hii basi inazingatia umuhimu wa lugha kwenye kuunda jamii na katika hatua za kuondoa mbinu za kikoloni mtandaoni ili wenyeji wa Afrika Mashariki wajione mtandaoni kwa ujumla wao wote.
Makala pia itazingatia semiotiki ya lugha katika ubunifu wa teknolojia, na umuhimu wa kutafsiri jamii ya lugha ya Kiswahili katika harakati za kuondoa ukoloni katika ubunifu huu.
Lakini sio tu kwamba lugha ya Kiswahili ndio pekee inayoweza kuondoa mbinu za kikoloni mtandaoni, kwani pia lugha hiyo ina ishara za kutawalwa kwa jamii fulani.
Bali makala hii inatumia mfano wa Kiswahili kuhimiza utumiaji wa lugha za kiasili au za kimama mtandaoni ili kulinda mustakabali wa kidijitali wa umma.
Originality/value
Umuhimu wa makala hii ni kuashiria jipya umuhimu wa lugha katika harakati za kuendeleza haki za kidijitali na hasa kuondoa mbinu za kikoloni kwenye teknolojia, swala lisilowahijadiliwa katika lugha ya Kiswahili.
Related Results
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza namna ambavyo Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa kwa nchi ya Uganda. Ni kweli kwamba nchini Uganda, watu kadhaa wakiwemo baadhi ya wanasiasa ha...
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika ...
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nyanja mbalimbali katika jamii hutegemea matumizi ya lugha. Hali hii huzua changamoto ya namna ya kutumia raslimali za lugha zinazopatikana katika jamiilugha fulani. Juhudi ya kufa...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Teknolojia ibuka na ufundishaji wa somo la Kiswahili
Teknolojia ibuka na ufundishaji wa somo la Kiswahili
Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuchanganua teknolojia ibuka na ufundishaji wa somo la Kiswahili. Katika sekta mbalimbali kama vile afya, benki, biashara, usafiri, utawala, ki...
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba...

