Javascript must be enabled to continue!
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
View through CrossRef
Nyanja mbalimbali katika jamii hutegemea matumizi ya lugha. Hali hii huzua changamoto ya namna ya kutumia raslimali za lugha zinazopatikana katika jamiilugha fulani. Juhudi ya kufahamu na kutagusana na ulimwengu huhitaji matumizi ya kiisimu ya kipekee. Katika muktadha wa kidini kuna changamoto ya asili ya maneno, mamlaka, utambulisho na ushirikiano wa wahusika. Aidha, miktadha mbalimbali ya kidini hutumia lugha kutimiza mahitaji yake maalum. Lugha hutenda matendo, huomba maombi ya kukemea, husimulia hali za kijamii na hata huonekana kudhibiti matendo ya Maulana. Ni kwa misingi hii ndipo kazi hii inajukumika kutalii jinsi lugha ya Kiswahili na Kibukusu zinavyotagusana katika mawanda haya ya dini, hasa Dini ya Musambwa (DYM) ambayo inaaminika kuwa ya kiasili katika jamii hii ya Wabukusu katika Kaunti ya Bungoma. Kazi hii inazingatia misingi ya Spolsky (2004, 2006, 2009) ambaye anajadili kuwa sera ya lugha halisi ya jamii hupatikana kwenye matumizi yake. Anazingatia Mwelekeo wa ikolojia ya lugha uliozinduliwa na Haugen (1972) unaochunguza mwingiliano baina ya lugha na mazingira. Muundo wa kiuchanganuzi ulitumiwa. Kupitia uchunzaji wa kutoshiriki moja kwa moja mtafiti alihudhuria ibada na kunasa mazungumzo yao kwenye kanda ya kunasia sauti. Mazungumzo hayo yalinakiliwa na orodha ya uchunzaji ilitumiwa kubainisha na kueleza namna lugha ya Kibukusu na Kiswahili zilivyotumiwa katika shughuli za kanisa hilo. Hali ya kuchanganya na kubadili msimbo, utohozi na hata matumizi ya Kiswahili kwa Kibukusu haikuweza kuepukika. Utafiti huu unadhihirisha kuwa raslimali za lugha zilizopo katika ikolojia fulani huchagizana katika kukamilisha majukumu ya mawasiliano katika muktadha husika.
East African Nature and Science Organization
Title: Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Description:
Nyanja mbalimbali katika jamii hutegemea matumizi ya lugha.
Hali hii huzua changamoto ya namna ya kutumia raslimali za lugha zinazopatikana katika jamiilugha fulani.
Juhudi ya kufahamu na kutagusana na ulimwengu huhitaji matumizi ya kiisimu ya kipekee.
Katika muktadha wa kidini kuna changamoto ya asili ya maneno, mamlaka, utambulisho na ushirikiano wa wahusika.
Aidha, miktadha mbalimbali ya kidini hutumia lugha kutimiza mahitaji yake maalum.
Lugha hutenda matendo, huomba maombi ya kukemea, husimulia hali za kijamii na hata huonekana kudhibiti matendo ya Maulana.
Ni kwa misingi hii ndipo kazi hii inajukumika kutalii jinsi lugha ya Kiswahili na Kibukusu zinavyotagusana katika mawanda haya ya dini, hasa Dini ya Musambwa (DYM) ambayo inaaminika kuwa ya kiasili katika jamii hii ya Wabukusu katika Kaunti ya Bungoma.
Kazi hii inazingatia misingi ya Spolsky (2004, 2006, 2009) ambaye anajadili kuwa sera ya lugha halisi ya jamii hupatikana kwenye matumizi yake.
Anazingatia Mwelekeo wa ikolojia ya lugha uliozinduliwa na Haugen (1972) unaochunguza mwingiliano baina ya lugha na mazingira.
Muundo wa kiuchanganuzi ulitumiwa.
Kupitia uchunzaji wa kutoshiriki moja kwa moja mtafiti alihudhuria ibada na kunasa mazungumzo yao kwenye kanda ya kunasia sauti.
Mazungumzo hayo yalinakiliwa na orodha ya uchunzaji ilitumiwa kubainisha na kueleza namna lugha ya Kibukusu na Kiswahili zilivyotumiwa katika shughuli za kanisa hilo.
Hali ya kuchanganya na kubadili msimbo, utohozi na hata matumizi ya Kiswahili kwa Kibukusu haikuweza kuepukika.
Utafiti huu unadhihirisha kuwa raslimali za lugha zilizopo katika ikolojia fulani huchagizana katika kukamilisha majukumu ya mawasiliano katika muktadha husika.
Related Results
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi...
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Lengo la makala haya ni kuonesha utangamano wa lugha ya Kiswahili na lugha ya Kinyambo. Utangamano wa lugha hizo umeoneshwa katika baadhi ya vipengele vya kimofolojia ambavyo ni mb...
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika ...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili
Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli ya kuelekeza mabinti zao katika maisha ya ndoa. Anafanya hivyo kwa kurejelea ndoa za kijadi ...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...

