Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Utata wa Maudhui ya Kisarufi katika Vitabu vya Kiada vya Kiswahili Kidato cha Kwanza na cha Tatu Nchini Tanzania

View through CrossRef
Vitabu vya kiada ni nyenzo muhimu katika ufundishaji wa somo la Kiswahili nchini Tanzania. Hutumika kama mwongozo wa ufundishaji wa mada zilizoteuliwa kwa kiwango husika cha elimu. Kutokana na umuhimu huo, vitabu hivyo huandikwa vizuri na kwa mpangilio mzuri wenye mantiki na unaoeleweka. Inapotokea kitabu cha kiada kimekuwa na changamoto za maudhui, kuna uwezekano wa maarifa yaliyokusudiwa kutowafikia walengwa kama inavyotakiwa. Hivyo basi, malengo ya makala hii ni kuchambua utata wa kimaudhui unaojitokeza kwenye vipengele vya mada za sarufi katika vitabu vya kiada vya Kiswahili (kidato I na III) na kupendekeza utatuzi wake kwa ajili ya maboresho zaidi. Data za makala hii zimepatikana kwa mbinu ya usomaji makini wa vitabu teule vilivyoandikwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Matokeo ya utafiti yanadhihirisha kuwapo kwa utata kwenye baadhi ya vipengele vya sarufi katika vitabu hivyo. Baadhi ya utata uliobainika unahusu fasili za dhana, mifano iliyotolewa na ufafanuzi wa kushadidia hoja zilizomo vitabuni. Makala inapendekeza kuwa vitabu husika vinapaswa kupitiwa tena ili kurekebisha maudhui yanayoibua utata uliobainishwa.
African Journals Online (AJOL)
Title: Utata wa Maudhui ya Kisarufi katika Vitabu vya Kiada vya Kiswahili Kidato cha Kwanza na cha Tatu Nchini Tanzania
Description:
Vitabu vya kiada ni nyenzo muhimu katika ufundishaji wa somo la Kiswahili nchini Tanzania.
Hutumika kama mwongozo wa ufundishaji wa mada zilizoteuliwa kwa kiwango husika cha elimu.
Kutokana na umuhimu huo, vitabu hivyo huandikwa vizuri na kwa mpangilio mzuri wenye mantiki na unaoeleweka.
Inapotokea kitabu cha kiada kimekuwa na changamoto za maudhui, kuna uwezekano wa maarifa yaliyokusudiwa kutowafikia walengwa kama inavyotakiwa.
Hivyo basi, malengo ya makala hii ni kuchambua utata wa kimaudhui unaojitokeza kwenye vipengele vya mada za sarufi katika vitabu vya kiada vya Kiswahili (kidato I na III) na kupendekeza utatuzi wake kwa ajili ya maboresho zaidi.
Data za makala hii zimepatikana kwa mbinu ya usomaji makini wa vitabu teule vilivyoandikwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).
Matokeo ya utafiti yanadhihirisha kuwapo kwa utata kwenye baadhi ya vipengele vya sarufi katika vitabu hivyo.
Baadhi ya utata uliobainika unahusu fasili za dhana, mifano iliyotolewa na ufafanuzi wa kushadidia hoja zilizomo vitabuni.
Makala inapendekeza kuwa vitabu husika vinapaswa kupitiwa tena ili kurekebisha maudhui yanayoibua utata uliobainishwa.

Related Results

Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili

Mikabala Mbalimbali ya Uchanganuzi wa Sentensi Changamano za Kiswahili katika Vitabu vya Kiada vya Shule za Sekondari
Mikabala Mbalimbali ya Uchanganuzi wa Sentensi Changamano za Kiswahili katika Vitabu vya Kiada vya Shule za Sekondari
Rasimu ya mtalaa mpya wa elimu nchini Kenya imebaini vipengele anavyopaswa kuzingatishwa mwanafunzi ili kuimarisha uwezo na maarifa yake katika ujifunzaji wa Kiswahili. Hali hii im...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulid...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...

Back to Top