Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili

View through CrossRef
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jamii. Tafiti nyingi zilizofanywa zinahusu vipengele vya fasihi kama vile maudhui, matumizi ya lugha, wahusika na mandhari katika fasihi. Katika tafiti hizo, watafiti hawajaonyesha mifumo jamii inayojitokeza kutokana na vipengele hivi. Utafiti huu umezama na kiutathimini mifumo hii kupitia kwa tamthilia teule za Kiswahili ambazo ni: tamthilia ya Pango (2003) kilichoandikwa na Wamitila, Kifo Kisimani (2008) kilichoandikwa na Kithaka Wa Mberia na Mstahiki Meya (2009) kilichoandikwa na Timothy Arege. Mifumo iliyotafitiwa katika utafiti huu ni: mfumo wa utawala na siasa, wa uchumi katika jamii, wa utamaduni, wa imani na dini, ule wa tabaka za jamii na ule wa elimu ya jamii. Utafiti huu umeongozwa na madhumuni mahsusi yafutayo: kujadili maudhui yanayodhihirisha mifumo ya jamii katika tamthilia teule; kuchanganua mitindo ya lugha inavyodhihirisha mifumo ya kijamii kutoka tamthilia teule; na kuchunguza wahusika katika uhusika wao kwenye mandhari maalumu wanavyojenga ploti inayochangia kuweka wazi mifumo ya kijamii kutoka tamthilia teule. Kiunzi cha nadharia ya uchunguzi kimejengwa na nadharia za uhalisia na nadharia ya umtindo. Mihimili ya nadharia ya uhalisia ikiwemo masuala ya utawala na uongozi, yale ya vijana, udhanifu, ukosefu wa ajira na masuala ya jinsia imebainishwa kadri ilivyojitokeza kupitia tamthilia teule. Mbali na nadharia za uhalisia na umtindo nadharia ya ukoloni mamboleo imetumika kuelezea hali katika tamthilia hasa utambuzi wa mifumo jamii inayotokana na matokeo ya baada ya uhuru. Utafiti umeongozwa na tamthilia 26 zilizoandikwa nchini Kenya na Tanzania tangu mwaka wa 2000. Tamthilia 26 zilizotumika ni zile zilizoandikwa na wazawa asilia wa Afrika Mashariki na kati kufikia mwaka wa 2014. Asilimia kumi ya idadi hiyo ilipeana sampuli ya mbili nukta sita (2.6) ambacho ni kifani tosha cha tamthilia tatu. Utafiti huu umejikita Kenya na Tanzania kwa kigezo kuwa mbali na Kiswahili kuchimbukia na kuenea zaidi katika janibu hizi, imebainika pia kuwa sera na sheria za kikatiba za nchi hizi zimekipa Kiswahili kipao mbele. Orodha ya uchuzaji imetumika kukusanya data. Uchanganuzi wa data ulitumia yaliyomo. Utafiti huu unatarajiwa kuibua mawazo mapya kuhusu mifumo ya kijamii inayotokana na fasihi na hivyo kuchangia katika ukuaji wa elimu.
Title: Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Description:
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili.
Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jamii.
Tafiti nyingi zilizofanywa zinahusu vipengele vya fasihi kama vile maudhui, matumizi ya lugha, wahusika na mandhari katika fasihi.
Katika tafiti hizo, watafiti hawajaonyesha mifumo jamii inayojitokeza kutokana na vipengele hivi.
Utafiti huu umezama na kiutathimini mifumo hii kupitia kwa tamthilia teule za Kiswahili ambazo ni: tamthilia ya Pango (2003) kilichoandikwa na Wamitila, Kifo Kisimani (2008) kilichoandikwa na Kithaka Wa Mberia na Mstahiki Meya (2009) kilichoandikwa na Timothy Arege.
Mifumo iliyotafitiwa katika utafiti huu ni: mfumo wa utawala na siasa, wa uchumi katika jamii, wa utamaduni, wa imani na dini, ule wa tabaka za jamii na ule wa elimu ya jamii.
Utafiti huu umeongozwa na madhumuni mahsusi yafutayo: kujadili maudhui yanayodhihirisha mifumo ya jamii katika tamthilia teule; kuchanganua mitindo ya lugha inavyodhihirisha mifumo ya kijamii kutoka tamthilia teule; na kuchunguza wahusika katika uhusika wao kwenye mandhari maalumu wanavyojenga ploti inayochangia kuweka wazi mifumo ya kijamii kutoka tamthilia teule.
Kiunzi cha nadharia ya uchunguzi kimejengwa na nadharia za uhalisia na nadharia ya umtindo.
Mihimili ya nadharia ya uhalisia ikiwemo masuala ya utawala na uongozi, yale ya vijana, udhanifu, ukosefu wa ajira na masuala ya jinsia imebainishwa kadri ilivyojitokeza kupitia tamthilia teule.
Mbali na nadharia za uhalisia na umtindo nadharia ya ukoloni mamboleo imetumika kuelezea hali katika tamthilia hasa utambuzi wa mifumo jamii inayotokana na matokeo ya baada ya uhuru.
Utafiti umeongozwa na tamthilia 26 zilizoandikwa nchini Kenya na Tanzania tangu mwaka wa 2000.
Tamthilia 26 zilizotumika ni zile zilizoandikwa na wazawa asilia wa Afrika Mashariki na kati kufikia mwaka wa 2014.
Asilimia kumi ya idadi hiyo ilipeana sampuli ya mbili nukta sita (2.
6) ambacho ni kifani tosha cha tamthilia tatu.
Utafiti huu umejikita Kenya na Tanzania kwa kigezo kuwa mbali na Kiswahili kuchimbukia na kuenea zaidi katika janibu hizi, imebainika pia kuwa sera na sheria za kikatiba za nchi hizi zimekipa Kiswahili kipao mbele.
Orodha ya uchuzaji imetumika kukusanya data.
Uchanganuzi wa data ulitumia yaliyomo.
Utafiti huu unatarajiwa kuibua mawazo mapya kuhusu mifumo ya kijamii inayotokana na fasihi na hivyo kuchangia katika ukuaji wa elimu.

Related Results

Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Uongozi na Uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Uongozi na Uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Kiswahili Lengo la makala hii ni kuchunguza uongozi na uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (MME) katika tamthilia teule za Kiswahili. Kazi hii iliongozwa na Nadharia ya Uhis...

Back to Top