Javascript must be enabled to continue!
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
View through CrossRef
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jamii nyingi za Kiafrika humfungamanisha na jinsia ya kiume au kike kama ilivyo katika tamthilia ya Bembea ya Maisha iliyoandikwa na Timothy Arege mwaka wa 2020. Malengo ya Makala haya ni kutathmini jinsi masuala haya ya kijinsia yalivyo shughulikiwa na mwandishi huyu katika tamthilia hii. Nadharia itakayotumiwa kuendeleza kazi hii ni nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika iliyoasisiwa na Chioma (1980) na kuendelezwa na watafiti wengine kama Ogundipe (1994), Wamitila (2003), Nnaemeka (2003) miongoni mwa wengine. Nadharia hii inalenga kutoa mwelekeo wa jinsi ya kumnasua mwanamke katika nafasi finyu aliyopewa katika jamii na nyanja tofauti. Data iliyotumika kuendeleza utafiti huu ilitoka maktabani kwa kusoma makala, vitabu, majarida na mambo mengine katika mtandao yanayohusiana na mada hii. Data inayohusiana na jinsia ya wahusika ilitoka katika tamthilia ya Bembea ya Maisha. Tamthilia ya Bembea ya Maisha iliteuliwa kimaksudi kwani mwandishi amewapa nafasi tosha wahusika wa jinsia ya kike na kiume. Wahusika hawa pia ni wa miaka tofauti kuanzia watoto hadi watu wazima. Mtafiti alisoma tamthilia husika na kuchambua wahusika kwa undani ili kupata data. Data iliyohitajika ilikusanywa na matokeo kuwasilishwa kwa njia ya maelezo na jedwali. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kuwa, licha ya juhudi nyingi zilizofanywa ili kumpa mwanamke nafasi katika jamii, bado kuna baadhi ya waandishi ambao wamempa nafasi finyu au ya chini katika kazi zao za fasihi. Usampulishaji dhamirifu ulitumika kuteua tamthilia ya Bembea ya Maisha. Data iliteuliwa kimakusudi. Mtafiti alizingatia nidhamu katika utafiti huu. Utafiti huu utakuwa wa manufaa kwa waandishi wa kazi za kifasihi ambao wanadhamiria kuandika kwani watajua namna ya kumsawiri mwanamke kama kiungo muhimu katika maendeleo ya jamii. Aidha, wasomi wa fasihi za Kiafrika watapa taswira ya nafasi za kila jinsia katika jamii za Kiafrika
East African Nature and Science Organization
Title: Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Description:
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke.
Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili.
Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jamii nyingi za Kiafrika humfungamanisha na jinsia ya kiume au kike kama ilivyo katika tamthilia ya Bembea ya Maisha iliyoandikwa na Timothy Arege mwaka wa 2020.
Malengo ya Makala haya ni kutathmini jinsi masuala haya ya kijinsia yalivyo shughulikiwa na mwandishi huyu katika tamthilia hii.
Nadharia itakayotumiwa kuendeleza kazi hii ni nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika iliyoasisiwa na Chioma (1980) na kuendelezwa na watafiti wengine kama Ogundipe (1994), Wamitila (2003), Nnaemeka (2003) miongoni mwa wengine.
Nadharia hii inalenga kutoa mwelekeo wa jinsi ya kumnasua mwanamke katika nafasi finyu aliyopewa katika jamii na nyanja tofauti.
Data iliyotumika kuendeleza utafiti huu ilitoka maktabani kwa kusoma makala, vitabu, majarida na mambo mengine katika mtandao yanayohusiana na mada hii.
Data inayohusiana na jinsia ya wahusika ilitoka katika tamthilia ya Bembea ya Maisha.
Tamthilia ya Bembea ya Maisha iliteuliwa kimaksudi kwani mwandishi amewapa nafasi tosha wahusika wa jinsia ya kike na kiume.
Wahusika hawa pia ni wa miaka tofauti kuanzia watoto hadi watu wazima.
Mtafiti alisoma tamthilia husika na kuchambua wahusika kwa undani ili kupata data.
Data iliyohitajika ilikusanywa na matokeo kuwasilishwa kwa njia ya maelezo na jedwali.
Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kuwa, licha ya juhudi nyingi zilizofanywa ili kumpa mwanamke nafasi katika jamii, bado kuna baadhi ya waandishi ambao wamempa nafasi finyu au ya chini katika kazi zao za fasihi.
Usampulishaji dhamirifu ulitumika kuteua tamthilia ya Bembea ya Maisha.
Data iliteuliwa kimakusudi.
Mtafiti alizingatia nidhamu katika utafiti huu.
Utafiti huu utakuwa wa manufaa kwa waandishi wa kazi za kifasihi ambao wanadhamiria kuandika kwani watajua namna ya kumsawiri mwanamke kama kiungo muhimu katika maendeleo ya jamii.
Aidha, wasomi wa fasihi za Kiafrika watapa taswira ya nafasi za kila jinsia katika jamii za Kiafrika.
Related Results
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jami...
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulid...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Maudhui katika Nyimbo za Tohara za Wamasaaba Nchini Uganda
Maudhui katika Nyimbo za Tohara za Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala hii, mwandishi anaeleza maudhui mbalimbali yanayopatikana katika nyimbo za tohara za Wamasaaba nchini Uganda. Alifanya hivyo kwa kurejelea angalau mfano mmoja wa nyim...
Kupambanua Mbinu za Uwakilishi wa Uhalisia-Ajabu Katika Mustakabali wa Uongozi Barani Afrika Katika Karne ya 21 Katika Riwaya ya Babu Alipofufuka.
Kupambanua Mbinu za Uwakilishi wa Uhalisia-Ajabu Katika Mustakabali wa Uongozi Barani Afrika Katika Karne ya 21 Katika Riwaya ya Babu Alipofufuka.
Sanaa za kihalisia-ajabu husheheni usimulizi wa matukio yasiyotafsirika wala kufikirika kuwa na uyakinifu katika maisha ya mwanadamu. Fasihi za aina hii hutilia nguvu umazingaombwe...
Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
Utafiti huu unahusu maudhui katika nyimbo teule kwenye vyombo vya habari, mfano ni nyimbo katika kipindi cha Rauka katika runinga ya Citizen. Utafiti ulichochewa na haja ya kutaka ...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Fonolojia ni taaluma iliyosheheni viarudhi au vipambasauti kama ambavyo wataalamu wengine huviita. Miongoni mwake ni toni, lafudhi, mkazo, nguvumsikiko, usilabi, kiimbo, unguvunguv...

