Javascript must be enabled to continue!
Kupambanua Mbinu za Uwakilishi wa Uhalisia-Ajabu Katika Mustakabali wa Uongozi Barani Afrika Katika Karne ya 21 Katika Riwaya ya Babu Alipofufuka.
View through CrossRef
Sanaa za kihalisia-ajabu husheheni usimulizi wa matukio yasiyotafsirika wala kufikirika kuwa na uyakinifu katika maisha ya mwanadamu. Fasihi za aina hii hutilia nguvu umazingaombwe na kukiuka uhalisia. Riwaya ya Babu Alipofufuka ya Mohamed ni mfano mojawapo wa fasihi yenye uhalisia-mazingaombwe. Utafiti huu unapambanua mkabala huo kwa kusimikwa kwenye mada Mustakabali wa Uongozi katika bara la Afrika katika karne ya 21: Tathmini ya Uhalisia-ajabu katika Riwaya ya Babu Alipofufuka na Said Ahmed Mohamed. Malengo ya utafiti huu ni; Kupambanua uhalisia-ajabu na uozo wa uongozi na hatimaye kutambua suluhu kwa matatizo ya uongozi barani Afrika kwa mujibu wa riwaya ya Babu Alipofufuka. Uchunguzi katika kazi hii uliongozwa na nadharia ya uhalisia-ajabu kwa kujifunga kwa mihimili yake mitano: kinaya, uandishi ndani ya uandishi, umazingaombwe katika mukhtadha halisi, vurugu la kiwakati na muingilano wa matini. Utafiti wenyewe uliendeshwa kwa mtindo wa kimakusudi ambapo matini maalum zilichanganuliwa maktabani na vile vile mtandaoni. Mbinu ya uchanganuzi ilihusu yaliyomo katika riwaya ya Babu Alipofufuka. Mhakiki pia alilenga kuchanganua kazi nyingine za fasihi kwa misingi ya malengo ya utafiti huu. Matokeo ya uchunguzi huu yana umuhimu mkubwa kwani yatasaidia kuchunguza suala la uongozi katika kutatua matatizo ya ndani kwa ndani kwa mustakabali wa itikadi za Kiafrika. Uchunguzi huu unashikilia kuwa utandawazi ni nduli ambalo limechangia kuwepo kwa matatizo humu barani na kuzidi kuifanya Afrika kunyongeka katika minyororo ya utumwa mpya. Taswira hii ni dhahiri katika riwaya mpya za Kiswahili. Matokeo yake bila shaka yatapevua ufahamu kuwa Afrika ina itikadi za kijadi ambazo zilizingatiwa katika kutafuta suluhu kwa matatizo ya ndani kwa ndani hasa za kisiasa. Wanafunzi wa shule za upili na vyuo vikuu pia watanufaika na matokeo ya uchunguzi huu kwa kupata mwelekeo wa uhakiki wa kazi za fasihi mintarafu zenye uhalisia-ajabu.
East African Nature and Science Organization
Title: Kupambanua Mbinu za Uwakilishi wa Uhalisia-Ajabu Katika Mustakabali wa Uongozi Barani Afrika Katika Karne ya 21 Katika Riwaya ya Babu Alipofufuka.
Description:
Sanaa za kihalisia-ajabu husheheni usimulizi wa matukio yasiyotafsirika wala kufikirika kuwa na uyakinifu katika maisha ya mwanadamu.
Fasihi za aina hii hutilia nguvu umazingaombwe na kukiuka uhalisia.
Riwaya ya Babu Alipofufuka ya Mohamed ni mfano mojawapo wa fasihi yenye uhalisia-mazingaombwe.
Utafiti huu unapambanua mkabala huo kwa kusimikwa kwenye mada Mustakabali wa Uongozi katika bara la Afrika katika karne ya 21: Tathmini ya Uhalisia-ajabu katika Riwaya ya Babu Alipofufuka na Said Ahmed Mohamed.
Malengo ya utafiti huu ni; Kupambanua uhalisia-ajabu na uozo wa uongozi na hatimaye kutambua suluhu kwa matatizo ya uongozi barani Afrika kwa mujibu wa riwaya ya Babu Alipofufuka.
Uchunguzi katika kazi hii uliongozwa na nadharia ya uhalisia-ajabu kwa kujifunga kwa mihimili yake mitano: kinaya, uandishi ndani ya uandishi, umazingaombwe katika mukhtadha halisi, vurugu la kiwakati na muingilano wa matini.
Utafiti wenyewe uliendeshwa kwa mtindo wa kimakusudi ambapo matini maalum zilichanganuliwa maktabani na vile vile mtandaoni.
Mbinu ya uchanganuzi ilihusu yaliyomo katika riwaya ya Babu Alipofufuka.
Mhakiki pia alilenga kuchanganua kazi nyingine za fasihi kwa misingi ya malengo ya utafiti huu.
Matokeo ya uchunguzi huu yana umuhimu mkubwa kwani yatasaidia kuchunguza suala la uongozi katika kutatua matatizo ya ndani kwa ndani kwa mustakabali wa itikadi za Kiafrika.
Uchunguzi huu unashikilia kuwa utandawazi ni nduli ambalo limechangia kuwepo kwa matatizo humu barani na kuzidi kuifanya Afrika kunyongeka katika minyororo ya utumwa mpya.
Taswira hii ni dhahiri katika riwaya mpya za Kiswahili.
Matokeo yake bila shaka yatapevua ufahamu kuwa Afrika ina itikadi za kijadi ambazo zilizingatiwa katika kutafuta suluhu kwa matatizo ya ndani kwa ndani hasa za kisiasa.
Wanafunzi wa shule za upili na vyuo vikuu pia watanufaika na matokeo ya uchunguzi huu kwa kupata mwelekeo wa uhakiki wa kazi za fasihi mintarafu zenye uhalisia-ajabu.
Related Results
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili
Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Hulka za wahusika katika tungo za sanaa aghalabu husukwa kutokana na matendo yanayoathiriwa na matukio katika mazingira wanamokulia. Hulka hizi hudhihirika kupitia matamko yanayoba...
Uongozi na Uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Uongozi na Uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Kiswahili
Lengo la makala hii ni kuchunguza uongozi na uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (MME) katika tamthilia teule za Kiswahili. Kazi hii iliongozwa na Nadharia ya Uhis...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Tathmini ya Anthropomofiki katika Riwaya ya Shamba la Wanyama
Tathmini ya Anthropomofiki katika Riwaya ya Shamba la Wanyama
Makala haya yanatathmini namna anthropomofiki ilivyotumika katika riwaya ya Shamba la Wanyama ya George Orwell. Orwell ni miongoni mwa waandishi maarufu na waliosifika katika fani ...
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Makala hii inalinganisha dhamira zilizowasilishwa kupitia wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili zilizoandikwa na wanawake wa Kenya na Tanzania. Tumaini (2006) ya Clara...

