Javascript must be enabled to continue!
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
View through CrossRef
Hulka za wahusika katika tungo za sanaa aghalabu husukwa kutokana na matendo yanayoathiriwa na matukio katika mazingira wanamokulia. Hulka hizi hudhihirika kupitia matamko yanayobainisha mtagusano wa wahusika hao. Katika hali ya kawaida, matamko ya wahusika huongozwa, kuelekezwa na kudhibitiwa na uhalisia wa kaida tagusani yanayotokana na mazoea ya jamii husika katika miktadha maalum. Hivyo, kwa kuzingatia uyakinifu wa kaida hizi, kuna mipaka inayotarajiwa kudumishwa katika mtagusano wa wahusika mbalimbali. Hata hivyo, uhalisia wa kaida hizi unaonekana kukiukwa katika mtagusano wa wahusika wa umri na jinsia tofauti katika baadhi ya tungo za Ken Walibora. Mkabala wa makala hii ni kuwa ukiushi wa uhalisia huu umetumiwa kama njia ya kusawiri na kusuta upotovu wa maadili katika jamii. Utafiti huu ulioangikiwa nadharia ya Kitendo Neni cha Austin (1962) umejikita katika riwaya mbili za Ken Walibora: Siku Njema (1996) na Kidagaa Kimemwozea (2012). Riwaya hizi ziliteuliwa kimaksudi kutokana na uwezo wake wa kutoa data yakini zilizohitajika kutimiza mahitaji ya utafiti huu. Data za utafiti huu uliokitwa katika muundo elezi zilidondolewa na kunukuliwa kupitia usomaji wa kina wa riwaya husika kisha zikachanganuliwa kwa kupambanua yaliyomo. Matokeo ya utafiti huu yamewasilishwa kinathari. Pamedhihirika ukiushi wa kaida za kijinsia kuhusu maadili ya mapenzi, ukiushi wa kaida kuhusu maadili ya malezi, ukiushi wa kaida kuhusu maadili ya uaminifu na utu na ukiushi wa kaida katika mahusiano ya wanandoa kuhusu maadili ya ukweli.
East African Nature and Science Organization
Title: Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Description:
Hulka za wahusika katika tungo za sanaa aghalabu husukwa kutokana na matendo yanayoathiriwa na matukio katika mazingira wanamokulia.
Hulka hizi hudhihirika kupitia matamko yanayobainisha mtagusano wa wahusika hao.
Katika hali ya kawaida, matamko ya wahusika huongozwa, kuelekezwa na kudhibitiwa na uhalisia wa kaida tagusani yanayotokana na mazoea ya jamii husika katika miktadha maalum.
Hivyo, kwa kuzingatia uyakinifu wa kaida hizi, kuna mipaka inayotarajiwa kudumishwa katika mtagusano wa wahusika mbalimbali.
Hata hivyo, uhalisia wa kaida hizi unaonekana kukiukwa katika mtagusano wa wahusika wa umri na jinsia tofauti katika baadhi ya tungo za Ken Walibora.
Mkabala wa makala hii ni kuwa ukiushi wa uhalisia huu umetumiwa kama njia ya kusawiri na kusuta upotovu wa maadili katika jamii.
Utafiti huu ulioangikiwa nadharia ya Kitendo Neni cha Austin (1962) umejikita katika riwaya mbili za Ken Walibora: Siku Njema (1996) na Kidagaa Kimemwozea (2012).
Riwaya hizi ziliteuliwa kimaksudi kutokana na uwezo wake wa kutoa data yakini zilizohitajika kutimiza mahitaji ya utafiti huu.
Data za utafiti huu uliokitwa katika muundo elezi zilidondolewa na kunukuliwa kupitia usomaji wa kina wa riwaya husika kisha zikachanganuliwa kwa kupambanua yaliyomo.
Matokeo ya utafiti huu yamewasilishwa kinathari.
Pamedhihirika ukiushi wa kaida za kijinsia kuhusu maadili ya mapenzi, ukiushi wa kaida kuhusu maadili ya malezi, ukiushi wa kaida kuhusu maadili ya uaminifu na utu na ukiushi wa kaida katika mahusiano ya wanandoa kuhusu maadili ya ukweli.
Related Results
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jami...
Muainisho wa matamko tendi katika riwaya za Ken Walibora
Muainisho wa matamko tendi katika riwaya za Ken Walibora
Ikisiri
Makala hii inanuia kuchunguza matamko tendi yanayopatikana katika dayolojia baina ya wahusika katika riwaya za Walibora. Madhumuni mahsusi ni kuainisha MT yaliyotumiwa kati...
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Makala hii inalinganisha dhamira zilizowasilishwa kupitia wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili zilizoandikwa na wanawake wa Kenya na Tanzania. Tumaini (2006) ya Clara...
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Makala haya yalichunguza ujitokezaji wa ujumi wa Kiafrika katika ushairi wa Kiswahili wa Bongo Fleva pamoja na athari yake katika ushairi huo. Tafiti kuhusu vipengele vya ujumi wa ...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Kupambanua Mbinu za Uwakilishi wa Uhalisia-Ajabu Katika Mustakabali wa Uongozi Barani Afrika Katika Karne ya 21 Katika Riwaya ya Babu Alipofufuka.
Kupambanua Mbinu za Uwakilishi wa Uhalisia-Ajabu Katika Mustakabali wa Uongozi Barani Afrika Katika Karne ya 21 Katika Riwaya ya Babu Alipofufuka.
Sanaa za kihalisia-ajabu husheheni usimulizi wa matukio yasiyotafsirika wala kufikirika kuwa na uyakinifu katika maisha ya mwanadamu. Fasihi za aina hii hutilia nguvu umazingaombwe...

