Javascript must be enabled to continue!
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
View through CrossRef
Makala hii inalinganisha dhamira zilizowasilishwa kupitia wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili zilizoandikwa na wanawake wa Kenya na Tanzania. Tumaini (2006) ya Clara Momanyi, Dago wa Munje (2008) ya Sheila Ryanga, Kipimo cha Mizani (2004) ya Zainabu Burhani, Hiba ya Wivu (1997) ya Zainabu Mwanga. Kuna dhamira za uchapakazi, ndoa, maadili, umuhimu wa elimu, malezi na migogoro ingawa makala hii imejikita katika dhamira mbili ambazo zinalinganishwa katika riwaya teule. Riwaya hizi nne zimeteuliwa kimakusudi kulingana na maudhui mazito yaliyomo katika riwaya hizo kuhusu wanaume. Makala hii imeonesha kuwa nadharia ya ujifunzaji wa kijamii (imejikita kwenye uana) na mwanaume mpya zimekuwa nadharia faafu katika makala hii. Nadharia ya ujifunzaji wa kijamii huona tabia kama kitendo ambacho mtu hujifunza kutoka katika mazingira ambayo ndiyo hupelekea umuhimu wa majukumu ya kiana. Mwisho, makala hii imetumia nadharia ya mwanaume mpya, nadharia inayojaribu kuelezea kwanini baadhi ya wanaume hukaa na wake zao kwa usawa bila tabia za mfumo dume ambazo huashiria kuwepo kwa taasubi ya kiume. Mbinu ya Fasihi Linganishi imetumika kulinganisha usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya teule kupitia dhamira wanazowasilisha. Data iliyotumika katika Makala hii ilitolewa maktabani kwa kusoma tasnifu, makala na vitabu vinavyohusiana na mada. Uwasilishaji wa matokeo umefanyika kwa njia ya maelezo. Matokeo yameonesha kuwa waandishi wa kike wamemsawiri mwanamume kwa mtazamo chanya zaidi kuliko hasi. Kwa hiyo, kulingana na waandishi wa kike wa Tanzania na Kenya wameonesha kuwa mwanamume ni mpya kulingana na mpito wa wakati ambapo mambo mbalimbali ya ugandamizaji wa kijinsia yametupiliwa mbali ili kuleta uwiano wa kiana.
Title: Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Description:
Makala hii inalinganisha dhamira zilizowasilishwa kupitia wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili zilizoandikwa na wanawake wa Kenya na Tanzania.
Tumaini (2006) ya Clara Momanyi, Dago wa Munje (2008) ya Sheila Ryanga, Kipimo cha Mizani (2004) ya Zainabu Burhani, Hiba ya Wivu (1997) ya Zainabu Mwanga.
Kuna dhamira za uchapakazi, ndoa, maadili, umuhimu wa elimu, malezi na migogoro ingawa makala hii imejikita katika dhamira mbili ambazo zinalinganishwa katika riwaya teule.
Riwaya hizi nne zimeteuliwa kimakusudi kulingana na maudhui mazito yaliyomo katika riwaya hizo kuhusu wanaume.
Makala hii imeonesha kuwa nadharia ya ujifunzaji wa kijamii (imejikita kwenye uana) na mwanaume mpya zimekuwa nadharia faafu katika makala hii.
Nadharia ya ujifunzaji wa kijamii huona tabia kama kitendo ambacho mtu hujifunza kutoka katika mazingira ambayo ndiyo hupelekea umuhimu wa majukumu ya kiana.
Mwisho, makala hii imetumia nadharia ya mwanaume mpya, nadharia inayojaribu kuelezea kwanini baadhi ya wanaume hukaa na wake zao kwa usawa bila tabia za mfumo dume ambazo huashiria kuwepo kwa taasubi ya kiume.
Mbinu ya Fasihi Linganishi imetumika kulinganisha usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya teule kupitia dhamira wanazowasilisha.
Data iliyotumika katika Makala hii ilitolewa maktabani kwa kusoma tasnifu, makala na vitabu vinavyohusiana na mada.
Uwasilishaji wa matokeo umefanyika kwa njia ya maelezo.
Matokeo yameonesha kuwa waandishi wa kike wamemsawiri mwanamume kwa mtazamo chanya zaidi kuliko hasi.
Kwa hiyo, kulingana na waandishi wa kike wa Tanzania na Kenya wameonesha kuwa mwanamume ni mpya kulingana na mpito wa wakati ambapo mambo mbalimbali ya ugandamizaji wa kijinsia yametupiliwa mbali ili kuleta uwiano wa kiana.
Related Results
Uchanganuzi Linganishi wa Usawiri wa Wahusika wa Kiume Katika Riwaya ya Kiswahili
Uchanganuzi Linganishi wa Usawiri wa Wahusika wa Kiume Katika Riwaya ya Kiswahili
Makala haya yanakusudia kuchanganua na kulinganisha wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili ambazo ni: Mwisho wa Kosa, (1987) iliyoandikwa na Zainabu Burhani, Siku Njema...
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jami...
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Hulka za wahusika katika tungo za sanaa aghalabu husukwa kutokana na matendo yanayoathiriwa na matukio katika mazingira wanamokulia. Hulka hizi hudhihirika kupitia matamko yanayoba...
Mitindo ya Lugha Inayowabainisha Wahusika Wazimu katika Riwaya za Habwe
Mitindo ya Lugha Inayowabainisha Wahusika Wazimu katika Riwaya za Habwe
Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni zinaonyesha ongezeko la idadi ya wazimu katika jamii duniani kote (Kovacevic, 2021). Waandishi wa fasihi wamewaumba wahusika wazimu wakiakisi...
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...
Kupambanua Mbinu za Uwakilishi wa Uhalisia-Ajabu Katika Mustakabali wa Uongozi Barani Afrika Katika Karne ya 21 Katika Riwaya ya Babu Alipofufuka.
Kupambanua Mbinu za Uwakilishi wa Uhalisia-Ajabu Katika Mustakabali wa Uongozi Barani Afrika Katika Karne ya 21 Katika Riwaya ya Babu Alipofufuka.
Sanaa za kihalisia-ajabu husheheni usimulizi wa matukio yasiyotafsirika wala kufikirika kuwa na uyakinifu katika maisha ya mwanadamu. Fasihi za aina hii hutilia nguvu umazingaombwe...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...

