Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Mitindo ya Lugha Inayowabainisha Wahusika Wazimu katika Riwaya za Habwe

View through CrossRef
Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni zinaonyesha ongezeko la idadi ya wazimu katika jamii duniani kote (Kovacevic, 2021). Waandishi wa fasihi wamewaumba wahusika wazimu wakiakisi mazingira wanamoishi. Tangu jadi wahakiki wamejitahidi kueleza vipi wahusika wazimu wametumika katika fasihi. Tahakiki za tamthilia za Shakespeare na za Kiingereza za karne ya ishirini zimeeleza namna na sababu za uumbaji wao. Katika riwaya za Kiswahili hakuna tahakiki zinazoshughulikia wahusika wazimu wala mitindo ya lugha inayowabainisha. Makala hii ilidhamiria kuchanganua mitindo ya lugha inayowabainisha wahusika wazimu katika kazi teule za Habwe. Uteuzi huu ulitokana na Habwe kusifiwa kuwa mwandishi wa fasihi ya kiongofu aliyetumia motifu ya wazimu katika riwaya zake (Gromov, 2018). Riwaya tano za Habwe:  Paradiso (2005), Cheche za Moto (2008), Fumbo La Maisha (2009), Safari ya Lamu (2011) na Kovu Moyoni (2014) ziliteuliwa kupitia usampulishaji dhamirifu kwa kuwa zilikuwa na wahusika wazimu. Nadharia ya umitindo iliyoasisiwa na Bally (1909) ) na kuendelezwa na Thornborrow na Wareing (1998) iliteuliwa kwa ajili ya kazi hii. Muundo wa kiuchanganuzi umetumiwa. Data zilikusanywa kutumia kifaa cha kudondoa data kilichokuwa na vidokezo vya mitindo ya lugha inayotambulisha wahusika wazimu. Matini ya riwaya teule imesomwa kwa makini na vipengele mbalimbali, kurekodiwa. Kisha data imechanganuliwa, kufasiriwa na kuratibiwa kulingana na madhumuni ya utafiti. Matokeo yamewasillishwa kwa njia ya maelezo. Makala hii imedhihirisha jinsi mitindo ya lugha ilivyotumiwa kuwatambulisha wahusika wazimu.
Title: Mitindo ya Lugha Inayowabainisha Wahusika Wazimu katika Riwaya za Habwe
Description:
Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni zinaonyesha ongezeko la idadi ya wazimu katika jamii duniani kote (Kovacevic, 2021).
Waandishi wa fasihi wamewaumba wahusika wazimu wakiakisi mazingira wanamoishi.
Tangu jadi wahakiki wamejitahidi kueleza vipi wahusika wazimu wametumika katika fasihi.
Tahakiki za tamthilia za Shakespeare na za Kiingereza za karne ya ishirini zimeeleza namna na sababu za uumbaji wao.
Katika riwaya za Kiswahili hakuna tahakiki zinazoshughulikia wahusika wazimu wala mitindo ya lugha inayowabainisha.
Makala hii ilidhamiria kuchanganua mitindo ya lugha inayowabainisha wahusika wazimu katika kazi teule za Habwe.
Uteuzi huu ulitokana na Habwe kusifiwa kuwa mwandishi wa fasihi ya kiongofu aliyetumia motifu ya wazimu katika riwaya zake (Gromov, 2018).
Riwaya tano za Habwe:  Paradiso (2005), Cheche za Moto (2008), Fumbo La Maisha (2009), Safari ya Lamu (2011) na Kovu Moyoni (2014) ziliteuliwa kupitia usampulishaji dhamirifu kwa kuwa zilikuwa na wahusika wazimu.
Nadharia ya umitindo iliyoasisiwa na Bally (1909) ) na kuendelezwa na Thornborrow na Wareing (1998) iliteuliwa kwa ajili ya kazi hii.
Muundo wa kiuchanganuzi umetumiwa.
Data zilikusanywa kutumia kifaa cha kudondoa data kilichokuwa na vidokezo vya mitindo ya lugha inayotambulisha wahusika wazimu.
Matini ya riwaya teule imesomwa kwa makini na vipengele mbalimbali, kurekodiwa.
Kisha data imechanganuliwa, kufasiriwa na kuratibiwa kulingana na madhumuni ya utafiti.
Matokeo yamewasillishwa kwa njia ya maelezo.
Makala hii imedhihirisha jinsi mitindo ya lugha ilivyotumiwa kuwatambulisha wahusika wazimu.

Related Results

Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi...
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Lengo la makala haya ni kuonesha utangamano wa lugha ya Kiswahili na lugha ya Kinyambo. Utangamano wa lugha hizo umeoneshwa katika baadhi ya vipengele vya kimofolojia ambavyo ni mb...
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nyanja mbalimbali katika jamii hutegemea matumizi ya lugha. Hali hii huzua changamoto ya namna ya kutumia raslimali za lugha zinazopatikana katika jamiilugha fulani. Juhudi ya kufa...
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika ...
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Hulka za wahusika katika tungo za sanaa aghalabu husukwa kutokana na matendo yanayoathiriwa na matukio katika mazingira wanamokulia. Hulka hizi hudhihirika kupitia matamko yanayoba...

Back to Top