Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Kuchunguza Sababu Zinazowalazimu Wahusika Kufanya Ukahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema Na Ndoto ya Almasi

View through CrossRef
Utafiti huu ulichunguza suala la ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema (Mohamed S.Mohamed) na Ndoto ya Almasi (Ken Walibora). Kitendo cha ukahaba kimesababisha mashaka mengi sana katika maisha ya mwanadamu kama vile kupoteza ujira, uharibikaji wa ndoa, maradhi ya zinaa, vifo, kukata tamaa na utengano miongoni mwa wanajamii. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni: kubainisha usawiri wa ukahaba na wahusika makahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi; kuchunguza sababu zinazowalazimu wahusika kufanya ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi; na kudhihirisha athari za ukahaba kwa wahusika waliomo katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi.  Mtafiti alitumia nadharia ya utekelezi ambayo ni miongoni mwa nadharia nyingi zenye mtazamo wa kisosholojia. Nadharia ya utekelezi imeendelezwa na wanasosholojia kama vile Talcort Parsons na Emile Durkheim kama wanavyonukuliwa na Worsely Introducing Sociology (1970), huku akisema kwamba ukahaba husababishwa na mambo mawili yaani haja ya kutekeleza mahitaji ya kiuchumi na kwa kukidhi matashi ya nafsi zao kiashki.  Mtafiti pia alitumia nadharia ya umaksi iliyoanzishwa na Karl Marx (1818-1863) na Fredrich Engles(1820-1895).  Nadharia hii hufaa utafiti huu kwa kudhihirisha wahusika wanaoshiriki katika vitendo vya ukahaba kwa ajili ya kupata fedha au zawadi. Mabepari au walionacho huwa na lengo la kuridhisha miili yao tu na wanyonge huwa na lengo la kupata pesa ili kutimiza mahitaji yao, pengine, mnyonge hutolea mwili wake kwa ajili ya kupewa kazi au kupandishwa cheo kazini au kama njia ya kuilinda kazi yake ili asipigwe kalamu. Utafiti huu ni wa maktabani kwa hivyo, maktaba yaliyotumika ni yale ya Chuo Kikuu cha uislamu kilichopo nchini Uganda, Chuo kikuu cha Bishop Stuart Mbarara, na maktabani ya shule ya upili Heritage. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na uchunguzaji wa riwaya teule yaani: ile ya Nyota ya Rehema na ya Ndoto ya Almasi kwa kuzisoma na kuzichambua kwa kina na kuiwasilishwa data kwa mbinu ya kiuthamano. Utafiti huu umebainisha kuwa wahusika hufanya ukahaba ili kupata pesa au kuridhisha matashi ya nafsi zao kiashiki. Utafiti huu utakuwa wa muhimu sana kwa kufunza jamii kwamba kahaba si mwanamke peke yake kama inavyochukuliwa katika baadhi ya jamii bali kahaba ni mtu yeyote awe mwanamume au mwanamke anayeshiririki vitendo vya uzinzi.
Title: Kuchunguza Sababu Zinazowalazimu Wahusika Kufanya Ukahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema Na Ndoto ya Almasi
Description:
Utafiti huu ulichunguza suala la ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema (Mohamed S.
Mohamed) na Ndoto ya Almasi (Ken Walibora).
Kitendo cha ukahaba kimesababisha mashaka mengi sana katika maisha ya mwanadamu kama vile kupoteza ujira, uharibikaji wa ndoa, maradhi ya zinaa, vifo, kukata tamaa na utengano miongoni mwa wanajamii.
Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni: kubainisha usawiri wa ukahaba na wahusika makahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi; kuchunguza sababu zinazowalazimu wahusika kufanya ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi; na kudhihirisha athari za ukahaba kwa wahusika waliomo katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi.
  Mtafiti alitumia nadharia ya utekelezi ambayo ni miongoni mwa nadharia nyingi zenye mtazamo wa kisosholojia.
Nadharia ya utekelezi imeendelezwa na wanasosholojia kama vile Talcort Parsons na Emile Durkheim kama wanavyonukuliwa na Worsely Introducing Sociology (1970), huku akisema kwamba ukahaba husababishwa na mambo mawili yaani haja ya kutekeleza mahitaji ya kiuchumi na kwa kukidhi matashi ya nafsi zao kiashki.
  Mtafiti pia alitumia nadharia ya umaksi iliyoanzishwa na Karl Marx (1818-1863) na Fredrich Engles(1820-1895).
  Nadharia hii hufaa utafiti huu kwa kudhihirisha wahusika wanaoshiriki katika vitendo vya ukahaba kwa ajili ya kupata fedha au zawadi.
Mabepari au walionacho huwa na lengo la kuridhisha miili yao tu na wanyonge huwa na lengo la kupata pesa ili kutimiza mahitaji yao, pengine, mnyonge hutolea mwili wake kwa ajili ya kupewa kazi au kupandishwa cheo kazini au kama njia ya kuilinda kazi yake ili asipigwe kalamu.
Utafiti huu ni wa maktabani kwa hivyo, maktaba yaliyotumika ni yale ya Chuo Kikuu cha uislamu kilichopo nchini Uganda, Chuo kikuu cha Bishop Stuart Mbarara, na maktabani ya shule ya upili Heritage.
Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na uchunguzaji wa riwaya teule yaani: ile ya Nyota ya Rehema na ya Ndoto ya Almasi kwa kuzisoma na kuzichambua kwa kina na kuiwasilishwa data kwa mbinu ya kiuthamano.
Utafiti huu umebainisha kuwa wahusika hufanya ukahaba ili kupata pesa au kuridhisha matashi ya nafsi zao kiashiki.
Utafiti huu utakuwa wa muhimu sana kwa kufunza jamii kwamba kahaba si mwanamke peke yake kama inavyochukuliwa katika baadhi ya jamii bali kahaba ni mtu yeyote awe mwanamume au mwanamke anayeshiririki vitendo vya uzinzi.

Related Results

Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Mitindo ya Lugha Inayowabainisha Wahusika Wazimu katika Riwaya za Habwe
Mitindo ya Lugha Inayowabainisha Wahusika Wazimu katika Riwaya za Habwe
Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni zinaonyesha ongezeko la idadi ya wazimu katika jamii duniani kote (Kovacevic, 2021). Waandishi wa fasihi wamewaumba wahusika wazimu wakiakisi...
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Hulka za wahusika katika tungo za sanaa aghalabu husukwa kutokana na matendo yanayoathiriwa na matukio katika mazingira wanamokulia. Hulka hizi hudhihirika kupitia matamko yanayoba...
Wahusika wa Kivisasili na Athari yake katika Riwaya ya Kiswahili
Wahusika wa Kivisasili na Athari yake katika Riwaya ya Kiswahili
Wahusika ni kipengele muhimu cha kazi yoyote ya fasihi. Umuhimu wake unatokana na ukweli kwamba ujitokezaji wa vipengele vingine vya msingi vya fani na maudhui katika fasihi hutege...
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Makala hii inalinganisha dhamira zilizowasilishwa kupitia wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili zilizoandikwa na wanawake wa Kenya na Tanzania. Tumaini (2006) ya Clara...
Muainisho wa matamko tendi katika riwaya za Ken Walibora
Muainisho wa matamko tendi katika riwaya za Ken Walibora
Ikisiri Makala hii inanuia kuchunguza matamko tendi yanayopatikana katika dayolojia baina ya wahusika katika riwaya za Walibora. Madhumuni mahsusi ni kuainisha MT yaliyotumiwa kati...

Back to Top