Javascript must be enabled to continue!
Wahusika wa Kivisasili na Athari yake katika Riwaya ya Kiswahili
View through CrossRef
Wahusika ni kipengele muhimu cha kazi yoyote ya fasihi. Umuhimu wake unatokana na ukweli kwamba ujitokezaji wa vipengele vingine vya msingi vya fani na maudhui katika fasihi hutegemea sana namna ambavyo mwanafasihi amewaumba wahusika wake. Makala imetumia riwaya teule tatu ambazo ni Nagona, na Mzingile za Euphrase Kezilahabi na Ziraili na Zirani ya William Mkufya. Kwa hiyo, makala imejikita kuwabainisha wahusika wa kivisasili kwa kuzielezea sifa zao za msingi zinazowatofautisha na wahusika wasio wa kivisasili. Wahusika wa kivisasili waliobainishwa ni pamoja na Kakulu, Mimi, Kizee, Ziraili, Zirani na Kinjeketile Ngwale. Aidha, makala imejadili athari ya wahusika hao katika riwaya teule. Kwa kutumia Nadharia ya Uheminitiki, tumebaini athari anuwai. Mathalani, wahusika wa kivisasili waliotumika katika riwaya wamewezesha urithishaji wa amali za kiutamaduni na uhistorishaji. Pia, wahusika hawa wana athari ya uunganishaji wa ujadi na usasa. Vilevile, wanawezesha utambulishaji wa jamii husika.
Title: Wahusika wa Kivisasili na Athari yake katika Riwaya ya Kiswahili
Description:
Wahusika ni kipengele muhimu cha kazi yoyote ya fasihi.
Umuhimu wake unatokana na ukweli kwamba ujitokezaji wa vipengele vingine vya msingi vya fani na maudhui katika fasihi hutegemea sana namna ambavyo mwanafasihi amewaumba wahusika wake.
Makala imetumia riwaya teule tatu ambazo ni Nagona, na Mzingile za Euphrase Kezilahabi na Ziraili na Zirani ya William Mkufya.
Kwa hiyo, makala imejikita kuwabainisha wahusika wa kivisasili kwa kuzielezea sifa zao za msingi zinazowatofautisha na wahusika wasio wa kivisasili.
Wahusika wa kivisasili waliobainishwa ni pamoja na Kakulu, Mimi, Kizee, Ziraili, Zirani na Kinjeketile Ngwale.
Aidha, makala imejadili athari ya wahusika hao katika riwaya teule.
Kwa kutumia Nadharia ya Uheminitiki, tumebaini athari anuwai.
Mathalani, wahusika wa kivisasili waliotumika katika riwaya wamewezesha urithishaji wa amali za kiutamaduni na uhistorishaji.
Pia, wahusika hawa wana athari ya uunganishaji wa ujadi na usasa.
Vilevile, wanawezesha utambulishaji wa jamii husika.
Related Results
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Makala haya yalichunguza ujitokezaji wa ujumi wa Kiafrika katika ushairi wa Kiswahili wa Bongo Fleva pamoja na athari yake katika ushairi huo. Tafiti kuhusu vipengele vya ujumi wa ...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Kuchunguza Sababu Zinazowalazimu Wahusika Kufanya Ukahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema Na Ndoto ya Almasi
Kuchunguza Sababu Zinazowalazimu Wahusika Kufanya Ukahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema Na Ndoto ya Almasi
Utafiti huu ulichunguza suala la ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema (Mohamed S.Mohamed) na Ndoto ya Almasi (Ken Walibora). Kitendo cha ukahaba kimesababisha mashaka mengi san...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Hulka za wahusika katika tungo za sanaa aghalabu husukwa kutokana na matendo yanayoathiriwa na matukio katika mazingira wanamokulia. Hulka hizi hudhihirika kupitia matamko yanayoba...
Mitindo ya Lugha Inayowabainisha Wahusika Wazimu katika Riwaya za Habwe
Mitindo ya Lugha Inayowabainisha Wahusika Wazimu katika Riwaya za Habwe
Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni zinaonyesha ongezeko la idadi ya wazimu katika jamii duniani kote (Kovacevic, 2021). Waandishi wa fasihi wamewaumba wahusika wazimu wakiakisi...