Javascript must be enabled to continue!
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
View through CrossRef
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi kwa wanafunzi wanaojifunza lugha Kiswahili katika Idara ya lugha na Taaluma za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Sebha kwa muda mrefu, mtafiti aliona kuwa kuna wanafunzi wengi wanakumbana na matatizo mengi na ugumu wa kuelewa jinsi na kanuni za uundaji wa vitenzi katika lugha ya Kiswahili. Kwa kuwa mtafiti anaelekea kwenye dhana kwamba tofauti kati ya lugha hizo mbili katika jinsi na kanuni za uundaji wa kauli ya kutendwa ni sababu mojawapo ya kuwepo kwa baadhi ya matatizo na ugumu. Kwa hivyo, mtafiti alichunguza jinsi ya kubadilisha vitenzi kuwa katika kauli ya kutendwa kisha kuvitumia katika sentensi ili mwanafunzi ajue jinsi na kanuni za uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha zote mbili Kiswahili na Kiarabu. Ifahamike hapa kuwa utafiti huu unachukuliwa kuwa wa kwanza wa aina yake kwa kuwa ulishughulikia maelezo ya jinsi ya kuunda kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiarabu kwa lugha ya Kiswahili, pamoja na kwamba unachanganya katika kueleza uundaji wa kauli ya kutendwa katika Kiswahili na Kiarabu katika utafiti huo huo. Mwenyezi Mungu akipenda, utafiti huu utakuwa wa thamani si tu kwa wanafunzi wa Kiarabu wanaojifunza lugha ya Kiswahili, bali pia kwa wanafunzi wa Kiswahili wanaojifunza Kiarabu. Pia, utafiti huu utawasaidia katika kujua jinsi ya kuunda kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiarabu na tofauti na lugha ya Kiswahili. Isitoshe, bali faida itakuwa hata kwa walimu na watafiti wa lugha zote mbili.
Title: Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Description:
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi kwa wanafunzi wanaojifunza lugha Kiswahili katika Idara ya lugha na Taaluma za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Sebha kwa muda mrefu, mtafiti aliona kuwa kuna wanafunzi wengi wanakumbana na matatizo mengi na ugumu wa kuelewa jinsi na kanuni za uundaji wa vitenzi katika lugha ya Kiswahili.
Kwa kuwa mtafiti anaelekea kwenye dhana kwamba tofauti kati ya lugha hizo mbili katika jinsi na kanuni za uundaji wa kauli ya kutendwa ni sababu mojawapo ya kuwepo kwa baadhi ya matatizo na ugumu.
Kwa hivyo, mtafiti alichunguza jinsi ya kubadilisha vitenzi kuwa katika kauli ya kutendwa kisha kuvitumia katika sentensi ili mwanafunzi ajue jinsi na kanuni za uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha zote mbili Kiswahili na Kiarabu.
Ifahamike hapa kuwa utafiti huu unachukuliwa kuwa wa kwanza wa aina yake kwa kuwa ulishughulikia maelezo ya jinsi ya kuunda kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiarabu kwa lugha ya Kiswahili, pamoja na kwamba unachanganya katika kueleza uundaji wa kauli ya kutendwa katika Kiswahili na Kiarabu katika utafiti huo huo.
Mwenyezi Mungu akipenda, utafiti huu utakuwa wa thamani si tu kwa wanafunzi wa Kiarabu wanaojifunza lugha ya Kiswahili, bali pia kwa wanafunzi wa Kiswahili wanaojifunza Kiarabu.
Pia, utafiti huu utawasaidia katika kujua jinsi ya kuunda kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiarabu na tofauti na lugha ya Kiswahili.
Isitoshe, bali faida itakuwa hata kwa walimu na watafiti wa lugha zote mbili.
Related Results
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Lengo la makala haya ni kuonesha utangamano wa lugha ya Kiswahili na lugha ya Kinyambo. Utangamano wa lugha hizo umeoneshwa katika baadhi ya vipengele vya kimofolojia ambavyo ni mb...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika ...
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli ya kuelekeza mabinti zao katika maisha ya ndoa. Anafanya hivyo kwa kurejelea ndoa za kijadi ...
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nyanja mbalimbali katika jamii hutegemea matumizi ya lugha. Hali hii huzua changamoto ya namna ya kutumia raslimali za lugha zinazopatikana katika jamiilugha fulani. Juhudi ya kufa...
Ulinganishi Wa Uundaji Wa Maneno Ya Kiswahili Na Ya Kiarabu
Ulinganishi Wa Uundaji Wa Maneno Ya Kiswahili Na Ya Kiarabu
Makala hii imejadili suala la ulinganishi wa uundaji wa maneno ya Kiswahili na Kiarabu. Katika makala hii tumetoa taarifa kuhusu umuhimu na njia za uundaji wa maneno kwa jumla, aid...

