Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi

View through CrossRef
Lengo la makala haya ni kuonesha utangamano wa lugha ya Kiswahili na lugha ya Kinyambo. Utangamano wa lugha hizo umeoneshwa katika baadhi ya vipengele vya kimofolojia ambavyo ni mbinu za uundaji na katika utumizi wa baadhi ya viambishi. Data ya makala haya imepatikana kwa namna tofauti ambazo ni: mosi, katika orodha ya msamiati wa Kinyambo ili kupata maneno ya mkopo ya Kiswahili yanayotumika katika Kinyambo. Pili, maandiko ya wataalamu mbalimbali yamehusishwa ili kupata mifano ya maneno yenye viambishi maalumu vinavyoonesha utangamano katika lugha hizo. Tatu, ujuzi wa lugha hizi mbili alionao mwandishi wa makala haya umesaidia kupata na kuielewa data. Uchanganuzi wa data hizo umeongozwa na Nadharia ya Mofolojia Lekisika ili kuonesha mipaka ya viambishi katika maneno. Uchanguzi wa data hizo umedhihirisha masuala yafuatayo: kwanza, katika uundaji wa maneno, maneno yenye vibadala vyake katika lugha ya Kinyambo yanakopwa tena kutoka Kiswahili. Hali hii imeonesha utangamano wa wazi kwa kuwa hakuna hitaji la msingi la ukopaji wa namna hiyo kutokana na kuwapo kwa vibadala vya maneno hayo katika lugha hiyo. Pili, pamoja na kwamba kuna viambishi ambavyo havikubaliki katika Kiswahili rasmi, watumiaji wa lugha ya Kiswahili wanavitumia katika mawasiliano ya kawaida. Hali hii inadhihirisha utangamano wa lugha hizo mbili kwa sababu viambishi hivyo vinatumika katika lugha zinazoingiliana sana na Kiswahili. Hivyo, kwa kuwa lugha hutangamana na kubadilika, uchambuzi wa maneno kimofolojia haupaswi kwenda mbali na mabadiliko hayo ili kuona namna maumbo ya maneno yanavyobadilika na yanavyotumika katika lugha husika ili kwenda na uhalisia ulivyo.
University of Dar es Salaam
Title: Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Description:
Lengo la makala haya ni kuonesha utangamano wa lugha ya Kiswahili na lugha ya Kinyambo.
Utangamano wa lugha hizo umeoneshwa katika baadhi ya vipengele vya kimofolojia ambavyo ni mbinu za uundaji na katika utumizi wa baadhi ya viambishi.
Data ya makala haya imepatikana kwa namna tofauti ambazo ni: mosi, katika orodha ya msamiati wa Kinyambo ili kupata maneno ya mkopo ya Kiswahili yanayotumika katika Kinyambo.
Pili, maandiko ya wataalamu mbalimbali yamehusishwa ili kupata mifano ya maneno yenye viambishi maalumu vinavyoonesha utangamano katika lugha hizo.
Tatu, ujuzi wa lugha hizi mbili alionao mwandishi wa makala haya umesaidia kupata na kuielewa data.
Uchanganuzi wa data hizo umeongozwa na Nadharia ya Mofolojia Lekisika ili kuonesha mipaka ya viambishi katika maneno.
Uchanguzi wa data hizo umedhihirisha masuala yafuatayo: kwanza, katika uundaji wa maneno, maneno yenye vibadala vyake katika lugha ya Kinyambo yanakopwa tena kutoka Kiswahili.
Hali hii imeonesha utangamano wa wazi kwa kuwa hakuna hitaji la msingi la ukopaji wa namna hiyo kutokana na kuwapo kwa vibadala vya maneno hayo katika lugha hiyo.
Pili, pamoja na kwamba kuna viambishi ambavyo havikubaliki katika Kiswahili rasmi, watumiaji wa lugha ya Kiswahili wanavitumia katika mawasiliano ya kawaida.
Hali hii inadhihirisha utangamano wa lugha hizo mbili kwa sababu viambishi hivyo vinatumika katika lugha zinazoingiliana sana na Kiswahili.
Hivyo, kwa kuwa lugha hutangamana na kubadilika, uchambuzi wa maneno kimofolojia haupaswi kwenda mbali na mabadiliko hayo ili kuona namna maumbo ya maneno yanavyobadilika na yanavyotumika katika lugha husika ili kwenda na uhalisia ulivyo.

Related Results

Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Msingi wa makala haya ni “Sera ya Elimu na Mafunzo” (SEM, 2014). Makala yanahakiki nafasi ya lugha ya Kiswahili kwenye Sera ya Elimu na Mafunzo nchini Tanzania na mustakabali wake ...
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Tofauti za Kifonolojia na Kimsamiati baina ya Kiswahili cha Kigoma, Ujiji na Kiswahili Sanifu
Tofauti za Kifonolojia na Kimsamiati baina ya Kiswahili cha Kigoma, Ujiji na Kiswahili Sanifu
Watanzania wengi, hususani waishio vijijini, wana lugha zao za asili ambapo hujifunza Kiswahili na kukitumia kama lugha ya pili. Watanzania hao, wanapotumia Kiswahili huonekana wak...
Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania
Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania
Makala haya yanaeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ujumuishaji wa kidemokrasia nchini Tanzania kwa kuzingatia matumizi ya lugha hiyo kwenye michakato ya uchaguzi. Lengo la...
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika ...

Back to Top