Javascript must be enabled to continue!
Tofauti za Kifonolojia na Kimsamiati baina ya Kiswahili cha Kigoma, Ujiji na Kiswahili Sanifu
View through CrossRef
Watanzania wengi, hususani waishio vijijini, wana lugha zao za asili ambapo hujifunza Kiswahili na kukitumia kama lugha ya pili. Watanzania hao, wanapotumia Kiswahili huonekana wakibadili baadhi ya sauti na maneno. Makala hii inalenga kuchunguza tofauti za kifonolojia na kimsamiati baina ya Kiswahili cha Kigoma Ujiji na Kiswahili sanifu ili kubaini tofauti za matumizi ya sauti na maneno kati ya lugha hizo. Data zimekusanywa kwa kutumia ushuhudiaji na majadiliano ya vikundi. Uchambuzi na uwasilishaji wa data umeongozwa na Mkabala wa Mbinu Linganishi (Anttila, 1972). Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kuwa kuna tofauti ya kifonolojia baina Kiswahili cha Kigoma, Ujiji na Kiswahili sanifu katika sauti zenye maneno yenye asili ya kigeni kama vile sauti [h], [bu], [mu]. Pia, kuna tofauti ya mabadiliko ya sauti [a] badala ya sauti [ha], [s] kuwa [sh], [r] badala ya [l], [bh] badala ya [b] na [bu] au [tu] kuwa [wa]. Aidha, kuna tofauti za matumizi ya sauti [-ga], lafudhi na mabadiliko ya kialami [ngo] badala ya sauti [eti] na tofauti za urefushaji irabu. Katika muktadha huo, Kiswahili cha Kigoma, Ujiji kinafanana na kutofautiana na Kiswahili sanifu kifonolojia na kimsamiati. Hata hivyo, tofauti zilizobainika ni zile za ubadilishaji wa sauti na msamiati usio wa msingi katika lugha hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinatokana na athari za lugha mama.
Title: Tofauti za Kifonolojia na Kimsamiati baina ya Kiswahili cha Kigoma, Ujiji na Kiswahili Sanifu
Description:
Watanzania wengi, hususani waishio vijijini, wana lugha zao za asili ambapo hujifunza Kiswahili na kukitumia kama lugha ya pili.
Watanzania hao, wanapotumia Kiswahili huonekana wakibadili baadhi ya sauti na maneno.
Makala hii inalenga kuchunguza tofauti za kifonolojia na kimsamiati baina ya Kiswahili cha Kigoma Ujiji na Kiswahili sanifu ili kubaini tofauti za matumizi ya sauti na maneno kati ya lugha hizo.
Data zimekusanywa kwa kutumia ushuhudiaji na majadiliano ya vikundi.
Uchambuzi na uwasilishaji wa data umeongozwa na Mkabala wa Mbinu Linganishi (Anttila, 1972).
Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kuwa kuna tofauti ya kifonolojia baina Kiswahili cha Kigoma, Ujiji na Kiswahili sanifu katika sauti zenye maneno yenye asili ya kigeni kama vile sauti [h], [bu], [mu].
Pia, kuna tofauti ya mabadiliko ya sauti [a] badala ya sauti [ha], [s] kuwa [sh], [r] badala ya [l], [bh] badala ya [b] na [bu] au [tu] kuwa [wa].
Aidha, kuna tofauti za matumizi ya sauti [-ga], lafudhi na mabadiliko ya kialami [ngo] badala ya sauti [eti] na tofauti za urefushaji irabu.
Katika muktadha huo, Kiswahili cha Kigoma, Ujiji kinafanana na kutofautiana na Kiswahili sanifu kifonolojia na kimsamiati.
Hata hivyo, tofauti zilizobainika ni zile za ubadilishaji wa sauti na msamiati usio wa msingi katika lugha hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinatokana na athari za lugha mama.
.
Related Results
Muundo wa Kifonolojia wa Maneno ya Sheng’
Muundo wa Kifonolojia wa Maneno ya Sheng’
Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ – English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchu...
Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu
Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu
Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ –English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchun...
Ulinganisho wa Uingizaji wa Vidahizo Homonimu katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la Nne na Kamusi la Kiswahili Fasaha Toleo la Kwanza
Ulinganisho wa Uingizaji wa Vidahizo Homonimu katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la Nne na Kamusi la Kiswahili Fasaha Toleo la Kwanza
Makala haya yanalinganisha uingizaji wa vidahizo homonimu katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu toleo la nne (KKS4) (2004) na Kamusi la Kiswahili Fasaha toleo la kwanza (KKF1) (2010). ...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili
Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Kuchambua Athari ya Vivumishi vya Runyakitara Katika Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili Nchini Uganda
Kuchambua Athari ya Vivumishi vya Runyakitara Katika Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili Nchini Uganda
Katika mfumo wa elimu nchini Uganda, Kiswahili ni lugha muhimu kwa mawasiliano na maendeleo ya kijamii. Hata hivyo, wanafunzi wanaozungumza Runyakitara wanakumbana na changamoto ka...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Teknolojia ibuka na ufundishaji wa somo la Kiswahili
Teknolojia ibuka na ufundishaji wa somo la Kiswahili
Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuchanganua teknolojia ibuka na ufundishaji wa somo la Kiswahili. Katika sekta mbalimbali kama vile afya, benki, biashara, usafiri, utawala, ki...

