Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Muundo wa Kifonolojia wa Maneno ya Sheng’

View through CrossRef
Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ – English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchunguzi huu kwa sababu ndio kamusi ya kwanza ya Sheng’ kuwahi kuchapishwa. Licha ya kamusi hii kuchapishwa katika lugha ya Kiingereza ina leksimu za Sheng’ ambazo yafaa kuchunguzwa namna zinavyoathiri Kiswahili sanifu. Lengo la utafiti huu lilikuwa kueleza muundo wa kifonolojia wa maneno ya Sheng’ na jinsi yanavyotofautiana na Kiswahili sanifu. Nadharia ya utafiti ilikuwa Nadharia ya Fonolojia Boreshi ambayo inapatikana katika mtazamo mpana wa Nadharia Boreshi iliyoasisiwa na Alan Prince na Paul Smolensky (2003). Hii ni nadharia inayochunguza hatua za ukuaji wa msamiati kutoka hali ghafi hadi ukubalifu wake kupitia kwa vizuizi tofauti. Mahali pa utafiti palikuwa maktabani na mtandaoni. Mbinu ya uchunguzi ikawa kupitia kusikiliza na kusoma makala mbalimbali kuhusu mada hii. Data ilikusanywa kupitia kwa kuchunguza maneno na vidahizo vya maneno kutoka kamusi ya Sheng’ – English Dictionary (2003). Iliaminika kuwa kamusi hii ingetupa sampuli ya maneno mahsusi ya Sheng’ ambayo muundo wake huathiri matumizi katika Kiswahili sanifu kwenye jamii ya kisasa. Uchanganuzi wa maelezo ulitegemea mtazamo wa Fonolojia Boreshi katika nadharia ya fonolojia inayoangazia sarufi zalishi. Katika mtazamo huu, uambishaji wa maneno uliangaziwa na jinsi uundaji huo hutawaliwa na vizuizi mbalimbali na sheria za fonolojia. Uwasilishaji wa data ulikuwa kupitia kwa maelezo ya kina, michoro na jedwali. Uchunguzi huu ulidhamiria kuchangia usomi wa Kiswahili kwa kuweka wazi athari za Sheng’ katika ukuaji wa lugha ya Kiswahili kimsamiati. Kadhalika, utafiti huu utawasaidia wanafunzi kuweka mipaka bayana kati ya msimbo wa Sheng’ na lugha ya Kiswahili sanifu
Title: Muundo wa Kifonolojia wa Maneno ya Sheng’
Description:
Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu.
Kamusi ya Sheng’ – English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchunguzi huu kwa sababu ndio kamusi ya kwanza ya Sheng’ kuwahi kuchapishwa.
Licha ya kamusi hii kuchapishwa katika lugha ya Kiingereza ina leksimu za Sheng’ ambazo yafaa kuchunguzwa namna zinavyoathiri Kiswahili sanifu.
Lengo la utafiti huu lilikuwa kueleza muundo wa kifonolojia wa maneno ya Sheng’ na jinsi yanavyotofautiana na Kiswahili sanifu.
Nadharia ya utafiti ilikuwa Nadharia ya Fonolojia Boreshi ambayo inapatikana katika mtazamo mpana wa Nadharia Boreshi iliyoasisiwa na Alan Prince na Paul Smolensky (2003).
Hii ni nadharia inayochunguza hatua za ukuaji wa msamiati kutoka hali ghafi hadi ukubalifu wake kupitia kwa vizuizi tofauti.
Mahali pa utafiti palikuwa maktabani na mtandaoni.
Mbinu ya uchunguzi ikawa kupitia kusikiliza na kusoma makala mbalimbali kuhusu mada hii.
Data ilikusanywa kupitia kwa kuchunguza maneno na vidahizo vya maneno kutoka kamusi ya Sheng’ – English Dictionary (2003).
Iliaminika kuwa kamusi hii ingetupa sampuli ya maneno mahsusi ya Sheng’ ambayo muundo wake huathiri matumizi katika Kiswahili sanifu kwenye jamii ya kisasa.
Uchanganuzi wa maelezo ulitegemea mtazamo wa Fonolojia Boreshi katika nadharia ya fonolojia inayoangazia sarufi zalishi.
Katika mtazamo huu, uambishaji wa maneno uliangaziwa na jinsi uundaji huo hutawaliwa na vizuizi mbalimbali na sheria za fonolojia.
Uwasilishaji wa data ulikuwa kupitia kwa maelezo ya kina, michoro na jedwali.
Uchunguzi huu ulidhamiria kuchangia usomi wa Kiswahili kwa kuweka wazi athari za Sheng’ katika ukuaji wa lugha ya Kiswahili kimsamiati.
Kadhalika, utafiti huu utawasaidia wanafunzi kuweka mipaka bayana kati ya msimbo wa Sheng’ na lugha ya Kiswahili sanifu.

Related Results

Utabirifu wa Makosa ya Utenganishaji na Uunganishaji wa Maneno katika Kiswahili
Utabirifu wa Makosa ya Utenganishaji na Uunganishaji wa Maneno katika Kiswahili
Uandishi ni mchakato unaohitaji umakini ili kinachoandikwa kieleweke kwa msomaji kwa namna iliyokusudiwa na mwandishi. Ikiwa kueleweka kutazingatiwa, basi, kutakuwa na mawasiliano ...
Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu
Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu
Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ –English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchun...
Kubainisha Kanuni na Sheria Zinazotawala Muundo wa Maneno katika Sentensi Sahili ya Ekegusii.
Kubainisha Kanuni na Sheria Zinazotawala Muundo wa Maneno katika Sentensi Sahili ya Ekegusii.
Utafiti huu unalenga kubainisha kanuni na sheria zinazotawala muundo wa maneno katika sentensi sahili ya Ekegusii. Utafiti huu ulihasisiwa na nadharia ya Sintaksia Finyizi. Utafiti...
Uundaji wa Maneno ya Kiswahili katika Mawasiliano Mahalia: Utafiti wa Lugha za Kundi F30
Uundaji wa Maneno ya Kiswahili katika Mawasiliano Mahalia: Utafiti wa Lugha za Kundi F30
Uundaji wa maneno hulenga kukidhi mawasiliano kufuatia kujitokeza kwa mapengo ya mawasiliano, aghalabu, yanayosababishwa na kuzuka kwa vitu vipya au kukutana kwa makundi lugha mawi...
Tofauti za Kifonolojia na Kimsamiati baina ya Kiswahili cha Kigoma, Ujiji na Kiswahili Sanifu
Tofauti za Kifonolojia na Kimsamiati baina ya Kiswahili cha Kigoma, Ujiji na Kiswahili Sanifu
Watanzania wengi, hususani waishio vijijini, wana lugha zao za asili ambapo hujifunza Kiswahili na kukitumia kama lugha ya pili. Watanzania hao, wanapotumia Kiswahili huonekana wak...
Ukarabati wa Mfuatano wa Irabu kama Sababu ya Muunganiko wa Maneno katika Gᴉrᴉmi
Ukarabati wa Mfuatano wa Irabu kama Sababu ya Muunganiko wa Maneno katika Gᴉrᴉmi
Mfuatano wa irabu katika lugha nyingi za Kibantu haupendelewi katika mazungumzo. Huepukwa kwa kutumia ukarabati wa namna mbalimbali. Kwa hiyo, makala hii inahusu ukarabati unaofany...
Ulinganishi Wa Uundaji Wa Maneno Ya Kiswahili Na Ya Kiarabu
Ulinganishi Wa Uundaji Wa Maneno Ya Kiswahili Na Ya Kiarabu
Makala hii imejadili suala la ulinganishi wa uundaji wa maneno ya Kiswahili na Kiarabu. Katika makala hii tumetoa taarifa kuhusu umuhimu na njia za uundaji wa maneno kwa jumla, aid...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...

Back to Top