Javascript must be enabled to continue!
Kubainisha Kanuni na Sheria Zinazotawala Muundo wa Maneno katika Sentensi Sahili ya Ekegusii.
View through CrossRef
Utafiti huu unalenga kubainisha kanuni na sheria zinazotawala muundo wa maneno katika sentensi sahili ya Ekegusii. Utafiti huu ulihasisiwa na nadharia ya Sintaksia Finyizi. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani, vitabu teule vya Ekegusii kwa kutumia kifaa cha kudondoa data ulitumika katika kusanya data. Mbinu ya usampulishaji kwa lengo maalum ilitumika kwa lengo la kupata sentensi ambazo hudhihirisha mageuzi. Data iliwasilishwa kwa njia za maelezo. Utafiti huu ulidhihirisha kuwa muundo wa sentensi unahusu mpangilio wa viambajengo katika sentensi. Muundo wa virai ya sentensi sahili ya Ekegusii unategemea majopo ya maneno kisarufi. Majopo ya maneno yaliyotumika katika utafiti huu yanaweza kuainishwa katika makundi wawili: Jopo la leksia na jopo amilifu. Kuna categoria tano za maneno zilizoainishwa katika jopo leksia nazo ni nomino, kitenzi, kielezi, kivumishi na kihusishi. Jopo amilifu hutawaliwa na virai vibainishi, virai vipatanishi na virai shamirisho. Utafiti huu unapendekeza kuwa tafiti zaidi zinaweza kufanywa kuhusu sentensi ambatano au changamano. Isitoshe, utafiti wa mageuzi unaweza kufanywa kwa lugha nyingine ili kueleza iwapo kuna matokeo tofauti.
Title: Kubainisha Kanuni na Sheria Zinazotawala Muundo wa Maneno katika Sentensi Sahili ya Ekegusii.
Description:
Utafiti huu unalenga kubainisha kanuni na sheria zinazotawala muundo wa maneno katika sentensi sahili ya Ekegusii.
Utafiti huu ulihasisiwa na nadharia ya Sintaksia Finyizi.
Utafiti huu ulikuwa wa maktabani, vitabu teule vya Ekegusii kwa kutumia kifaa cha kudondoa data ulitumika katika kusanya data.
Mbinu ya usampulishaji kwa lengo maalum ilitumika kwa lengo la kupata sentensi ambazo hudhihirisha mageuzi.
Data iliwasilishwa kwa njia za maelezo.
Utafiti huu ulidhihirisha kuwa muundo wa sentensi unahusu mpangilio wa viambajengo katika sentensi.
Muundo wa virai ya sentensi sahili ya Ekegusii unategemea majopo ya maneno kisarufi.
Majopo ya maneno yaliyotumika katika utafiti huu yanaweza kuainishwa katika makundi wawili: Jopo la leksia na jopo amilifu.
Kuna categoria tano za maneno zilizoainishwa katika jopo leksia nazo ni nomino, kitenzi, kielezi, kivumishi na kihusishi.
Jopo amilifu hutawaliwa na virai vibainishi, virai vipatanishi na virai shamirisho.
Utafiti huu unapendekeza kuwa tafiti zaidi zinaweza kufanywa kuhusu sentensi ambatano au changamano.
Isitoshe, utafiti wa mageuzi unaweza kufanywa kwa lugha nyingine ili kueleza iwapo kuna matokeo tofauti.
Related Results
Kupambanua Kanuni Zinazotawala Mageuzi katika Sentensi Sahili ya Ekegusii Language in Kenya.
Kupambanua Kanuni Zinazotawala Mageuzi katika Sentensi Sahili ya Ekegusii Language in Kenya.
Utafiti huu unalenga kupambanua kanuni zinazotawala mageuzi katika sentensi sahili ya Ekegusii language in Kenya. Nadharia ya Sintaksia Finyizi na Sarufi Geuza Maumbo uliongoza uta...
Kuchanganua Aina za Mageuzi katika Maneno ya Sentensi Sahili ya Ekegusii.
Kuchanganua Aina za Mageuzi katika Maneno ya Sentensi Sahili ya Ekegusii.
Utafiti huu unachanganua aina za mageuzi zinazojitokeza katika sentensi sahili ya Ekegusii. Utafiti huu ulihasisiwa na nadharia za Sintaksia Finyizi na Sarufi Geuza Maumbo. Data il...
Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo
Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo
Makala haya yanahusu uchanganuzi wa ruwaza za Toni katika Vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo. Lengo kuu la makala haya ni kuchunguza ruwaza ya ujitokezaji wa toni katika vite...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Utabirifu wa Makosa ya Utenganishaji na Uunganishaji wa Maneno katika Kiswahili
Utabirifu wa Makosa ya Utenganishaji na Uunganishaji wa Maneno katika Kiswahili
Uandishi ni mchakato unaohitaji umakini ili kinachoandikwa kieleweke kwa msomaji kwa namna iliyokusudiwa na mwandishi. Ikiwa kueleweka kutazingatiwa, basi, kutakuwa na mawasiliano ...
Mikabala Mbalimbali ya Uchanganuzi wa Sentensi Changamano za Kiswahili katika Vitabu vya Kiada vya Shule za Sekondari
Mikabala Mbalimbali ya Uchanganuzi wa Sentensi Changamano za Kiswahili katika Vitabu vya Kiada vya Shule za Sekondari
Rasimu ya mtalaa mpya wa elimu nchini Kenya imebaini vipengele anavyopaswa kuzingatishwa mwanafunzi ili kuimarisha uwezo na maarifa yake katika ujifunzaji wa Kiswahili. Hali hii im...
Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu
Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu
Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ –English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchun...
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Nomino sahili ni maneno ambayo kimofolojia yameundwa na mofu huru moja. Pia, kisematiki, maneno haya yana maana zake katika kamusi. Licha ya kuwa na sifa hizi, uambikaji wa viambis...

