Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Utabirifu wa Makosa ya Utenganishaji na Uunganishaji wa Maneno katika Kiswahili

View through CrossRef
Uandishi ni mchakato unaohitaji umakini ili kinachoandikwa kieleweke kwa msomaji kwa namna iliyokusudiwa na mwandishi. Ikiwa kueleweka kutazingatiwa, basi, kutakuwa na mawasiliano madhubuti. Hata hivyo, matini mbalimbali zimekuwa na makosa mengi kiasi cha kukwamisha mawasiliano baina ya mwandishi na msomaji wake. Lengo la makala haya ni kuchunguza utabirifu wa makosa katika uandishi kwa kumakinikia makosa ya utenganishaji na uunganishaji wa maneno. Nadharia ya Uchanganuzi Makosa ya Corder (1967) imetumika kuchambua na kujadili data za utafiti kwa sababu inahusika na makosa yanayohusiana na lugha na isimu. Data zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa matini na usaili. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba makosa ya kutenganisha na kuunganisha maneno yanatabirika kwa sababu yana uelekeo mmoja. Makosa ya kuunganisha maneno yamegawanyika katika makundi makubwa manne, yaani maneno yenye urejeshi, maneno yenye kiambishi cha umahali na wakati, maneno yanayotokana na uradidi, na maneno ambatani. Makosa ya kuunganisha maneno yamegawanyika katika makundi mawili ambayo ni mwambatano wa vitenzi shirikishi vya “kuwa na” na nomino, na viunganishi tegemezi vinavyoanza na “kwa”. Kwa ujumla, makosa haya yanatokana na uhamishaji wa kanuni moja katika uandishi wa maneno fulani yenye vipashio, hususani viambishi vinavyofanana. Kufuatia matokeo haya, makala haya yanapendekeza waandishi kuzingatia aina na sifa mahususi za maneno na si kujumuisha kanuni zinazotumika kuandika baadhi ya maneno.
University of Dar es Salaam
Title: Utabirifu wa Makosa ya Utenganishaji na Uunganishaji wa Maneno katika Kiswahili
Description:
Uandishi ni mchakato unaohitaji umakini ili kinachoandikwa kieleweke kwa msomaji kwa namna iliyokusudiwa na mwandishi.
Ikiwa kueleweka kutazingatiwa, basi, kutakuwa na mawasiliano madhubuti.
Hata hivyo, matini mbalimbali zimekuwa na makosa mengi kiasi cha kukwamisha mawasiliano baina ya mwandishi na msomaji wake.
Lengo la makala haya ni kuchunguza utabirifu wa makosa katika uandishi kwa kumakinikia makosa ya utenganishaji na uunganishaji wa maneno.
Nadharia ya Uchanganuzi Makosa ya Corder (1967) imetumika kuchambua na kujadili data za utafiti kwa sababu inahusika na makosa yanayohusiana na lugha na isimu.
Data zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa matini na usaili.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba makosa ya kutenganisha na kuunganisha maneno yanatabirika kwa sababu yana uelekeo mmoja.
Makosa ya kuunganisha maneno yamegawanyika katika makundi makubwa manne, yaani maneno yenye urejeshi, maneno yenye kiambishi cha umahali na wakati, maneno yanayotokana na uradidi, na maneno ambatani.
Makosa ya kuunganisha maneno yamegawanyika katika makundi mawili ambayo ni mwambatano wa vitenzi shirikishi vya “kuwa na” na nomino, na viunganishi tegemezi vinavyoanza na “kwa”.
Kwa ujumla, makosa haya yanatokana na uhamishaji wa kanuni moja katika uandishi wa maneno fulani yenye vipashio, hususani viambishi vinavyofanana.
Kufuatia matokeo haya, makala haya yanapendekeza waandishi kuzingatia aina na sifa mahususi za maneno na si kujumuisha kanuni zinazotumika kuandika baadhi ya maneno.

Related Results

Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Lengo la makala haya ni kuonesha utangamano wa lugha ya Kiswahili na lugha ya Kinyambo. Utangamano wa lugha hizo umeoneshwa katika baadhi ya vipengele vya kimofolojia ambavyo ni mb...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...
Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu
Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu
Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ –English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchun...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi...

Back to Top