Javascript must be enabled to continue!
Uundaji wa Maneno ya Kiswahili katika Mawasiliano Mahalia: Utafiti wa Lugha za Kundi F30
View through CrossRef
Uundaji wa maneno hulenga kukidhi mawasiliano kufuatia kujitokeza kwa mapengo ya mawasiliano, aghalabu, yanayosababishwa na kuzuka kwa vitu vipya au kukutana kwa makundi lugha mawili au zaidi yanayohitaji kuwasiliana na kuelewana. Makala hii inahusu uundaji wa maneno ya Kiswahili pale jamiilugha za Kundi F30, ambazo ni Wanyiramba (F31), Wanyaturu (F32) na Warangi (F33), zinapowasiliana kwa Kiswahili kwa lengo la kukidhi mawasiliano. Makala hii imeshughulikia malengo mawili ambayo ni kubainisha maneno ya Kiswahili yanayoundwa katika jamiilugha za Kundi F30 na kufafanua mbinu zinazotumika kuunda maneno hayo. Nadharia ya Usilimishaji ilitumika katika uchambuzi na mjadala wa matokeo. Mbinu zilizotumika kukusanya data ni usaili na uchambuzi matini. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, pale wazungumzaji wa lugha mahususi za Kundi F30 wanapowasiliana wao kwa wao, hutumia maneno ya asili kutaja majina hayo, lakini wanapowasiliana kwa Kiswahili, hutumia maneno ya Kiswahili yanayofahamika ndani ya kundi hilo pana. Imeonekana zaidi kuwa maneno hayo huundwa kwa kutumia kanuni nne ambazo ni unasibu, utohoaji, uhamishaji na ukarabati-maana. Kufuatia matokeo hayo, makala hii inapendekeza kwamba maneno ya Kiswahili mahalia yakusanywe na kutambuliwa kwa kuingizwa katika kamusi mahususi za Kiswahili ili jamii pana ya Waswahili iweze kunufaika nayo.
Title: Uundaji wa Maneno ya Kiswahili katika Mawasiliano Mahalia: Utafiti wa Lugha za Kundi F30
Description:
Uundaji wa maneno hulenga kukidhi mawasiliano kufuatia kujitokeza kwa mapengo ya mawasiliano, aghalabu, yanayosababishwa na kuzuka kwa vitu vipya au kukutana kwa makundi lugha mawili au zaidi yanayohitaji kuwasiliana na kuelewana.
Makala hii inahusu uundaji wa maneno ya Kiswahili pale jamiilugha za Kundi F30, ambazo ni Wanyiramba (F31), Wanyaturu (F32) na Warangi (F33), zinapowasiliana kwa Kiswahili kwa lengo la kukidhi mawasiliano.
Makala hii imeshughulikia malengo mawili ambayo ni kubainisha maneno ya Kiswahili yanayoundwa katika jamiilugha za Kundi F30 na kufafanua mbinu zinazotumika kuunda maneno hayo.
Nadharia ya Usilimishaji ilitumika katika uchambuzi na mjadala wa matokeo.
Mbinu zilizotumika kukusanya data ni usaili na uchambuzi matini.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, pale wazungumzaji wa lugha mahususi za Kundi F30 wanapowasiliana wao kwa wao, hutumia maneno ya asili kutaja majina hayo, lakini wanapowasiliana kwa Kiswahili, hutumia maneno ya Kiswahili yanayofahamika ndani ya kundi hilo pana.
Imeonekana zaidi kuwa maneno hayo huundwa kwa kutumia kanuni nne ambazo ni unasibu, utohoaji, uhamishaji na ukarabati-maana.
Kufuatia matokeo hayo, makala hii inapendekeza kwamba maneno ya Kiswahili mahalia yakusanywe na kutambuliwa kwa kuingizwa katika kamusi mahususi za Kiswahili ili jamii pana ya Waswahili iweze kunufaika nayo.
Related Results
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi...
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Lengo la makala haya ni kuonesha utangamano wa lugha ya Kiswahili na lugha ya Kinyambo. Utangamano wa lugha hizo umeoneshwa katika baadhi ya vipengele vya kimofolojia ambavyo ni mb...
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika ...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu
Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu
Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ –English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchun...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nyanja mbalimbali katika jamii hutegemea matumizi ya lugha. Hali hii huzua changamoto ya namna ya kutumia raslimali za lugha zinazopatikana katika jamiilugha fulani. Juhudi ya kufa...

