Javascript must be enabled to continue!
Kuchambua Athari ya Vivumishi vya Runyakitara Katika Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili Nchini Uganda
View through CrossRef
Katika mfumo wa elimu nchini Uganda, Kiswahili ni lugha muhimu kwa mawasiliano na maendeleo ya kijamii. Hata hivyo, wanafunzi wanaozungumza Runyakitara wanakumbana na changamoto katika kujifunza Kiswahili, hasa kwenye matumizi ya vivumishi. Tofauti za kimuundo kati ya vivumishi vya Runyakitara na Kiswahili huathiri uelewa sahihi wa Kiswahili, na mara nyingi uhamishaji wa vivumishi kutoka Runyakitara huleta makosa ya kiisimu. Wanafunzi ambao lugha yao ya kwanza ni Runyakitara hukumbana na matatizo wanapojifunza Kiswahili kama lugha ya pili. Utafiti huu ulilenga kuchunguza athari za vivumishi vya Runyakitara katika ujifunzaji wa Kiswahili kwa kubainisha tofauti za kimuundo, kuchunguza athari zake, na kutathmini makosa ya kiisimu yanayotokana na uhamishaji wa vivumishi hivyo. Utafiti huu uliendeshwa kwa mujibu wa nadharia ya uchanganuzi linganuzi, inayozingatia uingiliaji wa lugha ya kwanza, uhamishaji chanya na hasi, pamoja na utambulisho wa makosa. Utafiti ulifanyika Mbarara, Uganda, ukitumia mbinu ya usampulishaji nasibu na kimaksudi katika shule 10 na wanafunzi 100 wa Kiswahili wenye Runyakitara kama lugha ya kwanza. Data ilikusanywa kupitia mjarabu wa kimaandishi na kimazungumzo, na kuchanganuliwa kimaelezo kwa kutumia majedwali na michoro. Matokeo yalionyesha kuwa, ingawa Runyakitara na Kiswahili zinatoka nasaba moja, zina tofauti na mfanano katika matumizi ya vivumishi. Utafiti huu utakuwa na mchango mkubwa kwa wataalamu wa isimu, ukisaidia kuboresha matumizi sahihi ya Kiswahili sanifu na Runyakitara bila kusababisha mwingiliano hasi au kuibuka kwa lugha mseto
East African Nature and Science Organization
Title: Kuchambua Athari ya Vivumishi vya Runyakitara Katika Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili Nchini Uganda
Description:
Katika mfumo wa elimu nchini Uganda, Kiswahili ni lugha muhimu kwa mawasiliano na maendeleo ya kijamii.
Hata hivyo, wanafunzi wanaozungumza Runyakitara wanakumbana na changamoto katika kujifunza Kiswahili, hasa kwenye matumizi ya vivumishi.
Tofauti za kimuundo kati ya vivumishi vya Runyakitara na Kiswahili huathiri uelewa sahihi wa Kiswahili, na mara nyingi uhamishaji wa vivumishi kutoka Runyakitara huleta makosa ya kiisimu.
Wanafunzi ambao lugha yao ya kwanza ni Runyakitara hukumbana na matatizo wanapojifunza Kiswahili kama lugha ya pili.
Utafiti huu ulilenga kuchunguza athari za vivumishi vya Runyakitara katika ujifunzaji wa Kiswahili kwa kubainisha tofauti za kimuundo, kuchunguza athari zake, na kutathmini makosa ya kiisimu yanayotokana na uhamishaji wa vivumishi hivyo.
Utafiti huu uliendeshwa kwa mujibu wa nadharia ya uchanganuzi linganuzi, inayozingatia uingiliaji wa lugha ya kwanza, uhamishaji chanya na hasi, pamoja na utambulisho wa makosa.
Utafiti ulifanyika Mbarara, Uganda, ukitumia mbinu ya usampulishaji nasibu na kimaksudi katika shule 10 na wanafunzi 100 wa Kiswahili wenye Runyakitara kama lugha ya kwanza.
Data ilikusanywa kupitia mjarabu wa kimaandishi na kimazungumzo, na kuchanganuliwa kimaelezo kwa kutumia majedwali na michoro.
Matokeo yalionyesha kuwa, ingawa Runyakitara na Kiswahili zinatoka nasaba moja, zina tofauti na mfanano katika matumizi ya vivumishi.
Utafiti huu utakuwa na mchango mkubwa kwa wataalamu wa isimu, ukisaidia kuboresha matumizi sahihi ya Kiswahili sanifu na Runyakitara bila kusababisha mwingiliano hasi au kuibuka kwa lugha mseto.
Related Results
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Lengo la makala haya ni kuonesha utangamano wa lugha ya Kiswahili na lugha ya Kinyambo. Utangamano wa lugha hizo umeoneshwa katika baadhi ya vipengele vya kimofolojia ambavyo ni mb...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...

