Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Ulinganisho wa Uingizaji wa Vidahizo Homonimu katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la Nne na Kamusi la Kiswahili Fasaha Toleo la Kwanza

View through CrossRef
Makala haya yanalinganisha uingizaji wa vidahizo homonimu katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu toleo la nne (KKS4) (2004) na Kamusi la Kiswahili Fasaha toleo la kwanza (KKF1) (2010). Malengo mahususi ya makala haya ni kueleza tofauti na ufanano unaojitokeza katika uingizaji wa vidahizo homonimu baina ya kamusi hizo mbili. Mbinu ya uchambuzi matini imetumika kupata data za makala haya. Makala haya yameongozwa na Nadharia ya Metaleksikografia iliyoasisiwa na Weigand (1984). Matokeo yanaonesha kuwa kuna tofauti katika uingizaji wa vidahizo homonimu baina ya KKS4 na KKF1 ambazo zimejidhihirisha katika taarifa za kimatamshi, kietimolojia, uhusika wa vitenzi pamoja na uingizaji wa fasili za maana. Baadhi ya tofauti zinasababishwa na tofauti za kiutamaduni na maeneo ya kijiografia baina ya watumiaji wa kamusi teule ambamo lugha ya Kiswahili inatumika. Hata hivyo, makala haya yamedhihirisha kuwapo kwa ufanano wa uingizaji wa vidahizo homonimu katika KKS4 na KKF1 katika vipengele vya tahajia, matamshi, ubainishaji wa viambishi vya umoja na wingi pamoja na ubainishaji wa viambishi vya upatanisho wa kisarufi. Kwa ujumla, taarifa zilizoingizwa katika KKS4 ni nyingi kuliko taarifa zilizoingizwa katika KKF1. Hivyo, ni vyema kushughulikia katika matoleo yanayofuata ya kamusi hizi teule yale yanayoonekana kuwa ni tofauti zenye changamoto ili kuwa na kamusi zenye utoshelevu zaidi.
Title: Ulinganisho wa Uingizaji wa Vidahizo Homonimu katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la Nne na Kamusi la Kiswahili Fasaha Toleo la Kwanza
Description:
Makala haya yanalinganisha uingizaji wa vidahizo homonimu katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu toleo la nne (KKS4) (2004) na Kamusi la Kiswahili Fasaha toleo la kwanza (KKF1) (2010).
Malengo mahususi ya makala haya ni kueleza tofauti na ufanano unaojitokeza katika uingizaji wa vidahizo homonimu baina ya kamusi hizo mbili.
Mbinu ya uchambuzi matini imetumika kupata data za makala haya.
Makala haya yameongozwa na Nadharia ya Metaleksikografia iliyoasisiwa na Weigand (1984).
Matokeo yanaonesha kuwa kuna tofauti katika uingizaji wa vidahizo homonimu baina ya KKS4 na KKF1 ambazo zimejidhihirisha katika taarifa za kimatamshi, kietimolojia, uhusika wa vitenzi pamoja na uingizaji wa fasili za maana.
Baadhi ya tofauti zinasababishwa na tofauti za kiutamaduni na maeneo ya kijiografia baina ya watumiaji wa kamusi teule ambamo lugha ya Kiswahili inatumika.
Hata hivyo, makala haya yamedhihirisha kuwapo kwa ufanano wa uingizaji wa vidahizo homonimu katika KKS4 na KKF1 katika vipengele vya tahajia, matamshi, ubainishaji wa viambishi vya umoja na wingi pamoja na ubainishaji wa viambishi vya upatanisho wa kisarufi.
Kwa ujumla, taarifa zilizoingizwa katika KKS4 ni nyingi kuliko taarifa zilizoingizwa katika KKF1.
Hivyo, ni vyema kushughulikia katika matoleo yanayofuata ya kamusi hizi teule yale yanayoonekana kuwa ni tofauti zenye changamoto ili kuwa na kamusi zenye utoshelevu zaidi.

Related Results

Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu
Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu
Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ –English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchun...
Muundo wa Kifonolojia wa Maneno ya Sheng’
Muundo wa Kifonolojia wa Maneno ya Sheng’
Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ – English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchu...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi...
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...

Back to Top