Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Mkakati wa Tafsiri Mkopo wa Istilahi za Kiingereza katika Kiswahili na Athari zake: Uchanganuzi wa Vidahizo Teule vya Kamusi ya Biolojia, Fizikia na Kemia

View through CrossRef
Makala hii inachunguza mkakati wa tafsiri mkopo wa istilahi za Kiingereza katika Kiswahili na athari zake kwa kuangazia uga wa biolojia, fizikia na kemia kupitia vidahizo teule vya Kamusi ya Biolojia, Fizikia na kemia (2012). Azma kuu ya uchunguzi huu ni kutathmini mchango wa tafsiri mkopo wa msamiati wa Kiingereza katika suala zima la kukuza lugha ya Kiswahili. Kwa mujibu wa makala hii eneo hili halijapewa aula miongoni mwa mada mbalimbali za tafsiri zilizokwishachunguzwa. Hii imemuhamasisha mtafiti kulishughulikia eneo hili. Data ya makala hii ilikusanywa uwandani katika idara na taasisi zilizo katika jiji la Dar es Salaam kwa njia ya usaili, hojaji na chanzo cha data cha maktabani. Idara na taasisi zilizohusishwa katika ukusanyaji wa data ni: Idara ya Lugha za Kigeni na Isimu, TATAKI kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na BAKIZA. Idara na taasisi hizi zinapatikana mkoani Dar es Salaam Wilaya ya Ubungo ambapo mtafiti alifanikiwa kudodosa na kufanya mahojiano ya ana kwa ana kwa wataalamu wa tafsiri. Aidha, data ilikusanywa kutoka katika matini mbalimbali kutoka chanzo cha data cha maktabani. Mathalani, kamusi, tasinifu, majarida na vitabu kadhaa kulingana na mada ya makala hii. Malengo ya makala hii yametimizwa kwa kuongozwa na Nadharia ya Istilahi za Kisayansi iliyoasisiwa na Kiingi (1989) na kuendelezwa na Kiingi (1992) na Kiingi (1998) na Mwaro-Were (2000, 2001). Halikadhalika, data ya makala hii imechambuliwa kwa kutumia mkabala wa maelezo. Aidha, matokeo yameonesha kuwa Kiswahili kimejipatia istilahi lukuki katika tasnia ya biolojia, fizikia pamoja na kemia kupitia mkakati wa tafsiri mkopo. Makala hii ni muhimu kwa wanaisimu kwani inabainisha istilahi mbalimbali za lugha ya Kiingereza katika uwanja wa biolojia, fizikia pamoja na kemia zilizoingizwa katika Kiswahili kupitia tafsiri mkopo. Inapendekezwa kuwa watafiti wa lugha wachunguze njia nyinginezo za ukopaji zinazokiendeleza Kiswahili kama vile utohozi na uasilishaji.
Title: Mkakati wa Tafsiri Mkopo wa Istilahi za Kiingereza katika Kiswahili na Athari zake: Uchanganuzi wa Vidahizo Teule vya Kamusi ya Biolojia, Fizikia na Kemia
Description:
Makala hii inachunguza mkakati wa tafsiri mkopo wa istilahi za Kiingereza katika Kiswahili na athari zake kwa kuangazia uga wa biolojia, fizikia na kemia kupitia vidahizo teule vya Kamusi ya Biolojia, Fizikia na kemia (2012).
Azma kuu ya uchunguzi huu ni kutathmini mchango wa tafsiri mkopo wa msamiati wa Kiingereza katika suala zima la kukuza lugha ya Kiswahili.
Kwa mujibu wa makala hii eneo hili halijapewa aula miongoni mwa mada mbalimbali za tafsiri zilizokwishachunguzwa.
Hii imemuhamasisha mtafiti kulishughulikia eneo hili.
Data ya makala hii ilikusanywa uwandani katika idara na taasisi zilizo katika jiji la Dar es Salaam kwa njia ya usaili, hojaji na chanzo cha data cha maktabani.
Idara na taasisi zilizohusishwa katika ukusanyaji wa data ni: Idara ya Lugha za Kigeni na Isimu, TATAKI kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na BAKIZA.
Idara na taasisi hizi zinapatikana mkoani Dar es Salaam Wilaya ya Ubungo ambapo mtafiti alifanikiwa kudodosa na kufanya mahojiano ya ana kwa ana kwa wataalamu wa tafsiri.
Aidha, data ilikusanywa kutoka katika matini mbalimbali kutoka chanzo cha data cha maktabani.
Mathalani, kamusi, tasinifu, majarida na vitabu kadhaa kulingana na mada ya makala hii.
Malengo ya makala hii yametimizwa kwa kuongozwa na Nadharia ya Istilahi za Kisayansi iliyoasisiwa na Kiingi (1989) na kuendelezwa na Kiingi (1992) na Kiingi (1998) na Mwaro-Were (2000, 2001).
Halikadhalika, data ya makala hii imechambuliwa kwa kutumia mkabala wa maelezo.
Aidha, matokeo yameonesha kuwa Kiswahili kimejipatia istilahi lukuki katika tasnia ya biolojia, fizikia pamoja na kemia kupitia mkakati wa tafsiri mkopo.
Makala hii ni muhimu kwa wanaisimu kwani inabainisha istilahi mbalimbali za lugha ya Kiingereza katika uwanja wa biolojia, fizikia pamoja na kemia zilizoingizwa katika Kiswahili kupitia tafsiri mkopo.
Inapendekezwa kuwa watafiti wa lugha wachunguze njia nyinginezo za ukopaji zinazokiendeleza Kiswahili kama vile utohozi na uasilishaji.

Related Results

Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulid...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Ulinganisho wa Uingizaji wa Vidahizo Homonimu katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la Nne na Kamusi la Kiswahili Fasaha Toleo la Kwanza
Ulinganisho wa Uingizaji wa Vidahizo Homonimu katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la Nne na Kamusi la Kiswahili Fasaha Toleo la Kwanza
Makala haya yanalinganisha uingizaji wa vidahizo homonimu katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu toleo la nne (KKS4) (2004) na Kamusi la Kiswahili Fasaha toleo la kwanza (KKF1) (2010). ...
Mtunzi kama Mtafsiri Anayeingilia Kati ya Tafsiri: Kifo Kisimani (1999) na Natala (2005)
Mtunzi kama Mtafsiri Anayeingilia Kati ya Tafsiri: Kifo Kisimani (1999) na Natala (2005)
Utafiti huu unalenga kuchunguza kwa kina nafasi na athari za mwandishi anaposhiriki moja kwa moja katika mchakato wa kutafsiri kazi yake ya kifasihi, kwa kuzingatia tamthilia mbili...
Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu
Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu
Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ –English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchun...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...

Back to Top