Javascript must be enabled to continue!
Mikinzano ya Kimtazamo baina ya Wahusika Inavyobainisha Falsafa ya Kiafrika: Mifano kutoka Riwaya ya <i>Dunia Uwanja wa Fujo</i> (2007)
View through CrossRef
Tofauti za kimtazamo baina ya wahusika zimekuwa zikijitokeza katika kazi mbalimbali za riwaya. Watunzi wa kazi hizo wamekuwa na kawaida ya kuwavisha wahusika uhusika unaopambanua mawazo, imani, itikadi na falsafa mbalimbali zinazoongoza maisha yao. Kuwapo kwa mitazamo hiyo, kumechochea tafiti nyingi kuchunguza falsafa ya waandishi wa kazi hizo, mitazamo ya wahusika na uhusika wao na Uafrikanishaji wa kazi hizo, hususani za riwaya. Makala hii inalenga kuchunguza mikinzano ya kimtazamo baina ya wahusika na namna inavyobainisha falsafa ya Kiafrika. Data za utafiti zimepatikana uwandani kupitia njia ya usomaji na uchambuzi matini. Mchakato wa uchambuzi umeongozwa na Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa mikinzano ya kimtazamo baina ya wahusika katika riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo (2007) imejitokeza katika masuala ya ndoa, uzazi, malezi, utamaduni na ujamaa. Vipengele hivyo ndivyo vimeibua mikinzano ya kimtazamo baina ya wahusika na kubainisha falsafa ya Kiafrika kwamba maisha ya Mwafrika yamejengwa katika kuthamini uzazi kama mhimili wa kuwapo na mwendelezo hai wa vizazi.
Title: Mikinzano ya Kimtazamo baina ya Wahusika Inavyobainisha Falsafa ya Kiafrika: Mifano kutoka Riwaya ya <i>Dunia Uwanja wa Fujo</i> (2007)
Description:
Tofauti za kimtazamo baina ya wahusika zimekuwa zikijitokeza katika kazi mbalimbali za riwaya.
Watunzi wa kazi hizo wamekuwa na kawaida ya kuwavisha wahusika uhusika unaopambanua mawazo, imani, itikadi na falsafa mbalimbali zinazoongoza maisha yao.
Kuwapo kwa mitazamo hiyo, kumechochea tafiti nyingi kuchunguza falsafa ya waandishi wa kazi hizo, mitazamo ya wahusika na uhusika wao na Uafrikanishaji wa kazi hizo, hususani za riwaya.
Makala hii inalenga kuchunguza mikinzano ya kimtazamo baina ya wahusika na namna inavyobainisha falsafa ya Kiafrika.
Data za utafiti zimepatikana uwandani kupitia njia ya usomaji na uchambuzi matini.
Mchakato wa uchambuzi umeongozwa na Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa mikinzano ya kimtazamo baina ya wahusika katika riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo (2007) imejitokeza katika masuala ya ndoa, uzazi, malezi, utamaduni na ujamaa.
Vipengele hivyo ndivyo vimeibua mikinzano ya kimtazamo baina ya wahusika na kubainisha falsafa ya Kiafrika kwamba maisha ya Mwafrika yamejengwa katika kuthamini uzazi kama mhimili wa kuwapo na mwendelezo hai wa vizazi.
Related Results
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Wahusika wa Kivisasili na Athari yake katika Riwaya ya Kiswahili
Wahusika wa Kivisasili na Athari yake katika Riwaya ya Kiswahili
Wahusika ni kipengele muhimu cha kazi yoyote ya fasihi. Umuhimu wake unatokana na ukweli kwamba ujitokezaji wa vipengele vingine vya msingi vya fani na maudhui katika fasihi hutege...
Mitindo ya Lugha Inayowabainisha Wahusika Wazimu katika Riwaya za Habwe
Mitindo ya Lugha Inayowabainisha Wahusika Wazimu katika Riwaya za Habwe
Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni zinaonyesha ongezeko la idadi ya wazimu katika jamii duniani kote (Kovacevic, 2021). Waandishi wa fasihi wamewaumba wahusika wazimu wakiakisi...
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Makala haya yalichunguza ujitokezaji wa ujumi wa Kiafrika katika ushairi wa Kiswahili wa Bongo Fleva pamoja na athari yake katika ushairi huo. Tafiti kuhusu vipengele vya ujumi wa ...
Kuchunguza Sababu Zinazowalazimu Wahusika Kufanya Ukahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema Na Ndoto ya Almasi
Kuchunguza Sababu Zinazowalazimu Wahusika Kufanya Ukahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema Na Ndoto ya Almasi
Utafiti huu ulichunguza suala la ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema (Mohamed S.Mohamed) na Ndoto ya Almasi (Ken Walibora). Kitendo cha ukahaba kimesababisha mashaka mengi san...
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Hulka za wahusika katika tungo za sanaa aghalabu husukwa kutokana na matendo yanayoathiriwa na matukio katika mazingira wanamokulia. Hulka hizi hudhihirika kupitia matamko yanayoba...
Muainisho wa matamko tendi katika riwaya za Ken Walibora
Muainisho wa matamko tendi katika riwaya za Ken Walibora
Ikisiri
Makala hii inanuia kuchunguza matamko tendi yanayopatikana katika dayolojia baina ya wahusika katika riwaya za Walibora. Madhumuni mahsusi ni kuainisha MT yaliyotumiwa kati...
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Makala hii inalinganisha dhamira zilizowasilishwa kupitia wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili zilizoandikwa na wanawake wa Kenya na Tanzania. Tumaini (2006) ya Clara...

