Javascript must be enabled to continue!
Uongozi na Uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia Teule za Kiswahili
View through CrossRef
Kiswahili
Lengo la makala hii ni kuchunguza uongozi na uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (MME) katika tamthilia teule za Kiswahili. Kazi hii iliongozwa na Nadharia ya Uhistoria Mpya iliyoasisiwa na Stephen Greenblatt mwaka wa 1980. Utafiti huu ni wa kithamano na ulitumia muundo wa kiuchanganuzi. Mbinu ya unukuzi ilitumiwa kukusanya data. Data ilipangwa kisha kuchanganuliwa kupitia Mbinu ya uhakiki wa yaliyomo. Kwa kutumia mbinu ya usampulishaji dhamirifu, tamthilia nne ziliteuliwa. Tamthilia hizi ziliteuliwa kwa msingi kuwa zina maudhui ya uongozi na ziliandikwa kati ya miaka ya 2016 na 2024. Hizi ni: Shamba la Halaiki, Mwinyi na Manyani ya Adili, Kifunganjia na Kodi. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo ya kazi hii ni kuwa kuna aina mbili kuu za uongozi zinazojitokeza katika tamthilia teule za Kiswahili: uongozi wa kidemokrasia na wa kidikteta. Demokrasia iliendeleza uafikiaji wa MME kinyume na udikteta uliodumaza uafikiaji wa MME. Makala haya yanapendekeza kuwa wananchi katika mataifa mbalimbali ya ulimwengu wachangie uongozi bora katika jamii zao ili kufanikisha uafikiaji wa MME. Aidha, watafiti wa baadaye walinganishe na kulinganua aina mbalimbali za uongozi katika kazi mbalimbali za fasihi kando na uongozi wa kidemokrasia na kidiktea ulioshughuliwa katika makala haya.
English
This paper investigated leadership and the realisation of SDGs in selected Swahili plays. This study was guided by the New Historicism Theory that was propounded by Stephen Greenblatt in 1980. This is qualitative research that employed an analytical research design. The transcriptional method was used to collect data. Data was organised and analysed through content analysis. Through the purposive sampling technique, four plays were selected. These plays were selected on the basis that they have a leadership theme and were written between the years 2016 and 2024. These are: Shamba la Halaiki, Mwinyi na Manyani ya Adili, Kifunganjia and Kodi. The findings of this study are that there are two distinct leadership styles in selected Swahili plays: democratic and dictatorial leadership styles. Democracy led to the realisation of the Sustainable Development Goals (SDGs). However, dictatorship derailed the achievement of the SDGs. This paper recommends that citizens in their respective countries should contribute to good leadership in order to achieve the SDGs. Further studies should be carried out by comparing and contrasting different types of leadership in different literary genres other than democratic and dictatorial types of government, as examined by this paper.
Keywords: Democracy, dictatorship, leadership, Sustainable Development Goals (SDGs), swahili plays
Editon Consortium Publishing
Title: Uongozi na Uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Description:
Kiswahili
Lengo la makala hii ni kuchunguza uongozi na uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (MME) katika tamthilia teule za Kiswahili.
Kazi hii iliongozwa na Nadharia ya Uhistoria Mpya iliyoasisiwa na Stephen Greenblatt mwaka wa 1980.
Utafiti huu ni wa kithamano na ulitumia muundo wa kiuchanganuzi.
Mbinu ya unukuzi ilitumiwa kukusanya data.
Data ilipangwa kisha kuchanganuliwa kupitia Mbinu ya uhakiki wa yaliyomo.
Kwa kutumia mbinu ya usampulishaji dhamirifu, tamthilia nne ziliteuliwa.
Tamthilia hizi ziliteuliwa kwa msingi kuwa zina maudhui ya uongozi na ziliandikwa kati ya miaka ya 2016 na 2024.
Hizi ni: Shamba la Halaiki, Mwinyi na Manyani ya Adili, Kifunganjia na Kodi.
Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo.
Matokeo ya kazi hii ni kuwa kuna aina mbili kuu za uongozi zinazojitokeza katika tamthilia teule za Kiswahili: uongozi wa kidemokrasia na wa kidikteta.
Demokrasia iliendeleza uafikiaji wa MME kinyume na udikteta uliodumaza uafikiaji wa MME.
Makala haya yanapendekeza kuwa wananchi katika mataifa mbalimbali ya ulimwengu wachangie uongozi bora katika jamii zao ili kufanikisha uafikiaji wa MME.
Aidha, watafiti wa baadaye walinganishe na kulinganua aina mbalimbali za uongozi katika kazi mbalimbali za fasihi kando na uongozi wa kidemokrasia na kidiktea ulioshughuliwa katika makala haya.
English
This paper investigated leadership and the realisation of SDGs in selected Swahili plays.
This study was guided by the New Historicism Theory that was propounded by Stephen Greenblatt in 1980.
This is qualitative research that employed an analytical research design.
The transcriptional method was used to collect data.
Data was organised and analysed through content analysis.
Through the purposive sampling technique, four plays were selected.
These plays were selected on the basis that they have a leadership theme and were written between the years 2016 and 2024.
These are: Shamba la Halaiki, Mwinyi na Manyani ya Adili, Kifunganjia and Kodi.
The findings of this study are that there are two distinct leadership styles in selected Swahili plays: democratic and dictatorial leadership styles.
Democracy led to the realisation of the Sustainable Development Goals (SDGs).
However, dictatorship derailed the achievement of the SDGs.
This paper recommends that citizens in their respective countries should contribute to good leadership in order to achieve the SDGs.
Further studies should be carried out by comparing and contrasting different types of leadership in different literary genres other than democratic and dictatorial types of government, as examined by this paper.
Keywords: Democracy, dictatorship, leadership, Sustainable Development Goals (SDGs), swahili plays.
Related Results
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jami...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili
Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Udhihirikaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia ya Shamba la Halaiki (Okello, 2016)
Udhihirikaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia ya Shamba la Halaiki (Okello, 2016)
Lengo la makala hii ni kuchunguza udhihirikaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (MME) katika tamthilia ya Shamba la Halaiki (Okello, 2016). Mpango wa MME umekumbatiwa na wasomi, wa...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Kiswahili na Wadau: Fursa na Changamoto kwa Maendeleo Endelevu
Kiswahili na Wadau: Fursa na Changamoto kwa Maendeleo Endelevu
Lengo la makala hii ni kujadili fursa na changamoto kwa maendeleo endelevu ya lugha ya Kiswahili, hususan baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na U...

