Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Kiswahili na Wadau: Fursa na Changamoto kwa Maendeleo Endelevu

View through CrossRef
Lengo la makala hii ni kujadili fursa na changamoto kwa maendeleo endelevu ya lugha ya Kiswahili, hususan baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni - UNESCO kutangaza Siku ya Maalumu ya Kiswahili duniani. Kutangazwa kwa siku hii kunatoa fursa kwa wadau wa Kiswahili katika ngazi zote za kitaifa na kimataifa kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na maendeleo ya Kiswahili. Katika makala hii, pamoja na masuala yaliyolengwa, mwandishi anatoa shukurani zake kwa asasi mbalimbali za kimataifa ambazo zimeshiriki kwa namna tofauti katika mchakato wa kufanikisha hatua ya kutangazwa tarehe 7 Julai kuwa siku maalumu ya Kiswahili duniani. Makala hii inajadili kwa ujumla, majukumu na mchango wa wadau mbalimbali katika maendeleo ya Kiswahili kwa kudokeza fursa na changamoto katika maendeleo hayo. Mtafiti anahitimisha kwa kusisitiza kuwa jukumu la kuendeleza lugha ni la taasisi zote za elimu, hususan vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi. Kutokana na changamoto kubwa ya kifedha, uzalendo uwekwe mbele ili kufanikisha malengo ya kukuza Kiswahili.
University of Dar es Salaam
Title: Kiswahili na Wadau: Fursa na Changamoto kwa Maendeleo Endelevu
Description:
Lengo la makala hii ni kujadili fursa na changamoto kwa maendeleo endelevu ya lugha ya Kiswahili, hususan baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni - UNESCO kutangaza Siku ya Maalumu ya Kiswahili duniani.
Kutangazwa kwa siku hii kunatoa fursa kwa wadau wa Kiswahili katika ngazi zote za kitaifa na kimataifa kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na maendeleo ya Kiswahili.
Katika makala hii, pamoja na masuala yaliyolengwa, mwandishi anatoa shukurani zake kwa asasi mbalimbali za kimataifa ambazo zimeshiriki kwa namna tofauti katika mchakato wa kufanikisha hatua ya kutangazwa tarehe 7 Julai kuwa siku maalumu ya Kiswahili duniani.
Makala hii inajadili kwa ujumla, majukumu na mchango wa wadau mbalimbali katika maendeleo ya Kiswahili kwa kudokeza fursa na changamoto katika maendeleo hayo.
Mtafiti anahitimisha kwa kusisitiza kuwa jukumu la kuendeleza lugha ni la taasisi zote za elimu, hususan vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.
Kutokana na changamoto kubwa ya kifedha, uzalendo uwekwe mbele ili kufanikisha malengo ya kukuza Kiswahili.

Related Results

Mtunzi kama Mtafsiri Anayeingilia Kati ya Tafsiri: Kifo Kisimani (1999) na Natala (2005)
Mtunzi kama Mtafsiri Anayeingilia Kati ya Tafsiri: Kifo Kisimani (1999) na Natala (2005)
Utafiti huu unalenga kuchunguza kwa kina nafasi na athari za mwandishi anaposhiriki moja kwa moja katika mchakato wa kutafsiri kazi yake ya kifasihi, kwa kuzingatia tamthilia mbili...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
MASIKIDU kama Miviga ya Kuchochea Maendeleo ya Kiswahili
MASIKIDU kama Miviga ya Kuchochea Maendeleo ya Kiswahili
Makala hii inachunguza namna Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani – MASIKIDU yanavyoweza kutumiwa kama nyenzo ya kukuza maarifa ya Kiswahili ndani na nje ya Ukanda wa Afrika Ma...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza namna ambavyo Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa kwa nchi ya Uganda. Ni kweli kwamba nchini Uganda, watu kadhaa wakiwemo baadhi ya wanasiasa ha...
Udhihirikaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia ya Shamba la Halaiki (Okello, 2016)
Udhihirikaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia ya Shamba la Halaiki (Okello, 2016)
Lengo la makala hii ni kuchunguza udhihirikaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (MME) katika tamthilia ya Shamba la Halaiki (Okello, 2016). Mpango wa MME umekumbatiwa na wasomi, wa...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili

Back to Top