Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Udhihirikaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia ya Shamba la Halaiki (Okello, 2016)

View through CrossRef
Lengo la makala hii ni kuchunguza udhihirikaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (MME) katika tamthilia ya Shamba la Halaiki (Okello, 2016). Mpango wa MME umekumbatiwa na wasomi, wataalamu, mashirika na serikali mbalimbali duniani kwa kuwa ni njia ya kuafikia maendeleo. Waandishi wa fasihi wameshughulikia masuala ya maendeleo katika kazi zao. Fasihi kupitia utanzu wa tamthilia ina nafasi muhimu ya kuchangia uafikiaji wa MME kwa kuyaangazia. Utafiti huu ni wa kithamani na uliongozwa na Nadharia ya Uhistoria Mpya iliyoasisiwa na Stephen Greenblatt (1980) na kuendelezwa na Brizee na Tompkins (2012). Muundo wa kiuchanganuzi ulitumiwa. Data ilikusanywa kupitia mbinu ya unukuzi. Data kuhusu namna MME yanavyodhihirika katika tamthilia teule iliibuliwa kupitia wahusika, uumbaji wa mandhari na maudhui. Data hii ilipangwa kisha kuchanganuliwa kwa njia ya uhakiki wa yaliyomo. Kwa kutumia mbinu ya usampulishaji dhamirifu, tamthilia ya Shamba la Halaiki iliyoandikwa na Daniel Okello, 2016 iliteuliwa. Tamthilia hii iliteuliwa kwa msingi kuwa inaangazia MME na imeandikwa kati ya miaka ya 2016 na 2026 ambao ni kipindi cha utekelezaji wa mpango wa MME. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo ya maandishi. Matokeo yanaonyesha kuwa tamthilia teule inadhihirisha MME kupitia vipengele vya kifasihi kama wahusika, mandhari na maudhui, hivyo kujitokeza kama jukwaa muhimu la kujadili maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kimazingira. Hata hivyo, imebainika kuwa baadhi ya malengo hayajaangaziwa ipasavyo, hususan L2, L8, L9, L10, L12 na L14. Makala inapendekeza waandishi wa fasihi kuzingatia zaidi malengo haya ili kuimarisha mchango wa fasihi katika kuendeleza ajenda ya maendeleo endelevu.
Title: Udhihirikaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia ya Shamba la Halaiki (Okello, 2016)
Description:
Lengo la makala hii ni kuchunguza udhihirikaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (MME) katika tamthilia ya Shamba la Halaiki (Okello, 2016).
Mpango wa MME umekumbatiwa na wasomi, wataalamu, mashirika na serikali mbalimbali duniani kwa kuwa ni njia ya kuafikia maendeleo.
Waandishi wa fasihi wameshughulikia masuala ya maendeleo katika kazi zao.
Fasihi kupitia utanzu wa tamthilia ina nafasi muhimu ya kuchangia uafikiaji wa MME kwa kuyaangazia.
Utafiti huu ni wa kithamani na uliongozwa na Nadharia ya Uhistoria Mpya iliyoasisiwa na Stephen Greenblatt (1980) na kuendelezwa na Brizee na Tompkins (2012).
Muundo wa kiuchanganuzi ulitumiwa.
Data ilikusanywa kupitia mbinu ya unukuzi.
Data kuhusu namna MME yanavyodhihirika katika tamthilia teule iliibuliwa kupitia wahusika, uumbaji wa mandhari na maudhui.
Data hii ilipangwa kisha kuchanganuliwa kwa njia ya uhakiki wa yaliyomo.
Kwa kutumia mbinu ya usampulishaji dhamirifu, tamthilia ya Shamba la Halaiki iliyoandikwa na Daniel Okello, 2016 iliteuliwa.
Tamthilia hii iliteuliwa kwa msingi kuwa inaangazia MME na imeandikwa kati ya miaka ya 2016 na 2026 ambao ni kipindi cha utekelezaji wa mpango wa MME.
Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo ya maandishi.
Matokeo yanaonyesha kuwa tamthilia teule inadhihirisha MME kupitia vipengele vya kifasihi kama wahusika, mandhari na maudhui, hivyo kujitokeza kama jukwaa muhimu la kujadili maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kimazingira.
Hata hivyo, imebainika kuwa baadhi ya malengo hayajaangaziwa ipasavyo, hususan L2, L8, L9, L10, L12 na L14.
Makala inapendekeza waandishi wa fasihi kuzingatia zaidi malengo haya ili kuimarisha mchango wa fasihi katika kuendeleza ajenda ya maendeleo endelevu.

Related Results

Uongozi na Uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Uongozi na Uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Kiswahili Lengo la makala hii ni kuchunguza uongozi na uafikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (MME) katika tamthilia teule za Kiswahili. Kazi hii iliongozwa na Nadharia ya Uhis...
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jami...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Kiswahili na Wadau: Fursa na Changamoto kwa Maendeleo Endelevu
Kiswahili na Wadau: Fursa na Changamoto kwa Maendeleo Endelevu
Lengo la makala hii ni kujadili fursa na changamoto kwa maendeleo endelevu ya lugha ya Kiswahili, hususan baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na U...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...

Back to Top