Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

MASIKIDU kama Miviga ya Kuchochea Maendeleo ya Kiswahili

View through CrossRef
Makala hii inachunguza namna Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani – MASIKIDU yanavyoweza kutumiwa kama nyenzo ya kukuza maarifa ya Kiswahili ndani na nje ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, eneo ambalo sehemu kubwa ya wakazi wake wanaweza kuwasiliana kwa Kiswahili. Maadhimisho haya, yanayoadhimishwa kila mwaka tarehe 7 Julai, huwakutanisha wadau mbalimbali wa Kiswahili ambao hujadiliana masuala kadha wa kadha kuhusu lugha ya Kiswahili na utamaduni wake. Kwa hiyo, katika maadhimisho haya, wadau wanaweza kukumbushana na kupeana majukumu ya kuendeleza Kiswahili. Katika makala hii, MASIKIDU yamejadiliwa kama tukio linalochangia kubadilishana maarifa, fikra na mitazamo kuhusu lugha na fasihi ya Kiswahili. Kwa kutumia kiunzi cha miviga ya mpito chenye hatua tatu, yaani (i) mtengo, (ii) mabadiliko, na (iii) ujumuikaji, makala hii inafafanua namna MASIKIDU yanavyoweza kukuza maarifa ya washiriki na kusambaza maarifa hayo kwa wengine. Kwa ujumla, ikiwa kila mdau atashiriki katika MASIKIDU kwa dhamira ya dhati, kuna uwezekano wa maadhimisho haya kuwa kioo muhimu kwa wanagenzi na wanazuoni wa Kiswahili duniani.
University of Dar es Salaam
Title: MASIKIDU kama Miviga ya Kuchochea Maendeleo ya Kiswahili
Description:
Makala hii inachunguza namna Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani – MASIKIDU yanavyoweza kutumiwa kama nyenzo ya kukuza maarifa ya Kiswahili ndani na nje ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, eneo ambalo sehemu kubwa ya wakazi wake wanaweza kuwasiliana kwa Kiswahili.
Maadhimisho haya, yanayoadhimishwa kila mwaka tarehe 7 Julai, huwakutanisha wadau mbalimbali wa Kiswahili ambao hujadiliana masuala kadha wa kadha kuhusu lugha ya Kiswahili na utamaduni wake.
Kwa hiyo, katika maadhimisho haya, wadau wanaweza kukumbushana na kupeana majukumu ya kuendeleza Kiswahili.
Katika makala hii, MASIKIDU yamejadiliwa kama tukio linalochangia kubadilishana maarifa, fikra na mitazamo kuhusu lugha na fasihi ya Kiswahili.
Kwa kutumia kiunzi cha miviga ya mpito chenye hatua tatu, yaani (i) mtengo, (ii) mabadiliko, na (iii) ujumuikaji, makala hii inafafanua namna MASIKIDU yanavyoweza kukuza maarifa ya washiriki na kusambaza maarifa hayo kwa wengine.
Kwa ujumla, ikiwa kila mdau atashiriki katika MASIKIDU kwa dhamira ya dhati, kuna uwezekano wa maadhimisho haya kuwa kioo muhimu kwa wanagenzi na wanazuoni wa Kiswahili duniani.

Related Results

Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Kiswahili na Wadau: Fursa na Changamoto kwa Maendeleo Endelevu
Kiswahili na Wadau: Fursa na Changamoto kwa Maendeleo Endelevu
Lengo la makala hii ni kujadili fursa na changamoto kwa maendeleo endelevu ya lugha ya Kiswahili, hususan baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na U...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Uchambuzi wa Miktadha ya Kijamii na Mchango Wake katika Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili Nchini Burundi
Uchambuzi wa Miktadha ya Kijamii na Mchango Wake katika Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili Nchini Burundi
Makala hii inahusu miktadha ya kijamii na mchango wake katika kujifunza Kiswahili kama lugha ya pili nchini Burundi. Muktadha wa kijamii huathiri ujifunzaji wa lugha ya pili kwa ku...
Kuchambua Athari ya Vivumishi vya Runyakitara Katika Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili Nchini Uganda
Kuchambua Athari ya Vivumishi vya Runyakitara Katika Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili Nchini Uganda
Katika mfumo wa elimu nchini Uganda, Kiswahili ni lugha muhimu kwa mawasiliano na maendeleo ya kijamii. Hata hivyo, wanafunzi wanaozungumza Runyakitara wanakumbana na changamoto ka...
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza namna ambavyo Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa kwa nchi ya Uganda. Ni kweli kwamba nchini Uganda, watu kadhaa wakiwemo baadhi ya wanasiasa ha...

Back to Top