Javascript must be enabled to continue!
Uchambuzi wa Miktadha ya Kijamii na Mchango Wake katika Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili Nchini Burundi
View through CrossRef
Makala hii inahusu miktadha ya kijamii na mchango wake katika kujifunza Kiswahili kama lugha ya pili nchini Burundi. Muktadha wa kijamii huathiri ujifunzaji wa lugha ya pili kwa kuchochea mawasiliano ya kuongea, kukuza, na kuboresha matumizi halisi ya lugha katika mazingira ya kawaida (Ellis R., 2008). Hali hii ilimchochea mtafiti kufanya utafiti huu ili kubainisha miktadha ya kijamii iliyopo jijini Bujumbura na kuonesha mchango wake katika kujifunza Kiswahili kama lugha ya pili. Mbinu ya hojaji ilitumiwa kukusanya data. Aidha, mbinu ya usampulishaji tajwa ilitumika kuteua watoataarifa. Watoataarifa hao walikuwa wanafunzi 20 kutoka Chuo Kikuu cha Burundi, kiwango cha shahada ya awali. Nadharia ya Utamaduni Jamii iliyoasisiwa na Mwanasaikolojia Vygotsky (1978) iliongoza utafiti huu.
Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa miktadha ya kijamii ya kujifunza Kiswahili jijini Bujumbura ni soko, hospitali, zahanati, nyumbani, na kadhalika. Matokeo pia yalionesha kuwa miktadha hiyo inawawezesha wanafunzi kuingiza msamiati mpya, kukuza stadi za kusikiliza na kuzungumza. Inawawezesha pia, kuimarisha umilisi wa utamaduni na maarifa kuhusu fasihi. Serikali ya Burundi inaombwa kuchukua miktadha ya kijamii kama mikakati rasmi inayochangia kujifunza Kiswahili nchini. Mwisho, makala hii inapendekeza serikali ya Burundi iwezeshe walimu wa Kiswahili kufuatilia ujifunzaji wa Kiswahili wa wanafunzi nje ya darasa.
Title: Uchambuzi wa Miktadha ya Kijamii na Mchango Wake katika Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili Nchini Burundi
Description:
Makala hii inahusu miktadha ya kijamii na mchango wake katika kujifunza Kiswahili kama lugha ya pili nchini Burundi.
Muktadha wa kijamii huathiri ujifunzaji wa lugha ya pili kwa kuchochea mawasiliano ya kuongea, kukuza, na kuboresha matumizi halisi ya lugha katika mazingira ya kawaida (Ellis R.
, 2008).
Hali hii ilimchochea mtafiti kufanya utafiti huu ili kubainisha miktadha ya kijamii iliyopo jijini Bujumbura na kuonesha mchango wake katika kujifunza Kiswahili kama lugha ya pili.
Mbinu ya hojaji ilitumiwa kukusanya data.
Aidha, mbinu ya usampulishaji tajwa ilitumika kuteua watoataarifa.
Watoataarifa hao walikuwa wanafunzi 20 kutoka Chuo Kikuu cha Burundi, kiwango cha shahada ya awali.
Nadharia ya Utamaduni Jamii iliyoasisiwa na Mwanasaikolojia Vygotsky (1978) iliongoza utafiti huu.
Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa miktadha ya kijamii ya kujifunza Kiswahili jijini Bujumbura ni soko, hospitali, zahanati, nyumbani, na kadhalika.
Matokeo pia yalionesha kuwa miktadha hiyo inawawezesha wanafunzi kuingiza msamiati mpya, kukuza stadi za kusikiliza na kuzungumza.
Inawawezesha pia, kuimarisha umilisi wa utamaduni na maarifa kuhusu fasihi.
Serikali ya Burundi inaombwa kuchukua miktadha ya kijamii kama mikakati rasmi inayochangia kujifunza Kiswahili nchini.
Mwisho, makala hii inapendekeza serikali ya Burundi iwezeshe walimu wa Kiswahili kufuatilia ujifunzaji wa Kiswahili wa wanafunzi nje ya darasa.
Related Results
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi...
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Lengo la makala haya ni kuonesha utangamano wa lugha ya Kiswahili na lugha ya Kinyambo. Utangamano wa lugha hizo umeoneshwa katika baadhi ya vipengele vya kimofolojia ambavyo ni mb...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli ya kuelekeza mabinti zao katika maisha ya ndoa. Anafanya hivyo kwa kurejelea ndoa za kijadi ...

