Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Maudhui katika Nyimbo za Tohara za Wamasaaba Nchini Uganda

View through CrossRef
Katika makala hii, mwandishi anaeleza maudhui mbalimbali yanayopatikana katika nyimbo za tohara za Wamasaaba nchini Uganda. Alifanya hivyo kwa kurejelea angalau mfano mmoja wa nyimbo hizo kwa kila maudhui. Mwandishi amepanga maudhui hayo kulingana na utaratibu wa utendaji wa matukio ya tohara. Kutokana na jambo hili, mwandishi ameangalia matukio mbalimbali katika utekelezaji wa tohara kwa sababu nyimbo hizo huambatana na matukio fulani. Kwa kufanya hivyo, mwandishi ametaja tukio na kutoa mfano wa wimbo unaoimbwa. Baada ya kutoa mfano wa wimbo, anauchanganua na kubainisha maudhui mbalimbali yaliyomo. Mwandishi anafanya hivyo hatua kwa hatua mpaka mwisho. Dhamira ya utafiti ni kueleza jinsi Wamasaaba walivyobobea katika utanzu huu wa sanaa. Hali kadhalika, madhumuni ya utafiti huu ni kueleza namna nyimbo za kiutamaduni zilivyo muhimu katika maisha ya binadamu, kufafanua athari za nyimbo za tohara kisaikolojia na kuonyesha nguvu za mawasiliano za nyimbo za kiutamaduni. Mkabala wa utafiti huu ulikuwa wa nyanjani. Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alizuru nyanjani na kukusanya nyimbo. Katika kazi yake, mtafiti alitumia mbinu ya uchunguzi shiriki. Kwa kutumia mbinu hii, mtafiti alifuatilia makundi ya watendaji na kushuhudia jinsi matukio ya tohara yanavyotekelezwa. Kulingana na aina ya utafiti, mtafiti hakuuliza watu maswali. Mtafiti alitumia kinasa sauti kurekodi nyimbo. Baada ya mchakato huo kukamilika, mtafiti alizichanganua nyimbo ambazo alizikusanya halafu akawasilisha matokeo ya utafiti wake. Nyimbo zilizokusanywa zilijumlisha zile za kupokea wageni, zile zinazoonyesha huzuni kwa mhusika, zile zinazodhihirisha furaha kwa mhusika, zile za kuonya mhusika nk. Mtafiti alianza uchanganuzi wa nyimbo kwa kuziandika kwenye karatasi. Baada ya kufanya hivyo, alizipanga kulingana na madhumuni ya utafiti. Alipomaliza kufanya hivyo, mtafiti alieleza maudhui mbalimbali kama yalivyojitokeza katika kila wimbo.
East African Nature and Science Organization
Title: Maudhui katika Nyimbo za Tohara za Wamasaaba Nchini Uganda
Description:
Katika makala hii, mwandishi anaeleza maudhui mbalimbali yanayopatikana katika nyimbo za tohara za Wamasaaba nchini Uganda.
Alifanya hivyo kwa kurejelea angalau mfano mmoja wa nyimbo hizo kwa kila maudhui.
Mwandishi amepanga maudhui hayo kulingana na utaratibu wa utendaji wa matukio ya tohara.
Kutokana na jambo hili, mwandishi ameangalia matukio mbalimbali katika utekelezaji wa tohara kwa sababu nyimbo hizo huambatana na matukio fulani.
Kwa kufanya hivyo, mwandishi ametaja tukio na kutoa mfano wa wimbo unaoimbwa.
Baada ya kutoa mfano wa wimbo, anauchanganua na kubainisha maudhui mbalimbali yaliyomo.
Mwandishi anafanya hivyo hatua kwa hatua mpaka mwisho.
Dhamira ya utafiti ni kueleza jinsi Wamasaaba walivyobobea katika utanzu huu wa sanaa.
Hali kadhalika, madhumuni ya utafiti huu ni kueleza namna nyimbo za kiutamaduni zilivyo muhimu katika maisha ya binadamu, kufafanua athari za nyimbo za tohara kisaikolojia na kuonyesha nguvu za mawasiliano za nyimbo za kiutamaduni.
Mkabala wa utafiti huu ulikuwa wa nyanjani.
Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alizuru nyanjani na kukusanya nyimbo.
Katika kazi yake, mtafiti alitumia mbinu ya uchunguzi shiriki.
Kwa kutumia mbinu hii, mtafiti alifuatilia makundi ya watendaji na kushuhudia jinsi matukio ya tohara yanavyotekelezwa.
Kulingana na aina ya utafiti, mtafiti hakuuliza watu maswali.
Mtafiti alitumia kinasa sauti kurekodi nyimbo.
Baada ya mchakato huo kukamilika, mtafiti alizichanganua nyimbo ambazo alizikusanya halafu akawasilisha matokeo ya utafiti wake.
Nyimbo zilizokusanywa zilijumlisha zile za kupokea wageni, zile zinazoonyesha huzuni kwa mhusika, zile zinazodhihirisha furaha kwa mhusika, zile za kuonya mhusika nk.
Mtafiti alianza uchanganuzi wa nyimbo kwa kuziandika kwenye karatasi.
Baada ya kufanya hivyo, alizipanga kulingana na madhumuni ya utafiti.
Alipomaliza kufanya hivyo, mtafiti alieleza maudhui mbalimbali kama yalivyojitokeza katika kila wimbo.

Related Results

Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
Utafiti huu unahusu maudhui katika nyimbo teule kwenye vyombo vya habari, mfano ni nyimbo katika kipindi cha Rauka katika runinga ya Citizen. Utafiti ulichochewa na haja ya kutaka ...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000
Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000
Nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zilianza nchini Tanzania kipindi cha ukoloni. Nyimbo hizi zinasawiri ujumi mweusi kwa kiasi kikubwa, na zina unusura. Ujumi wa kijamii huwa na...
Athari za Usasa kwenye Usimulizi wa Hadithi katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Athari za Usasa kwenye Usimulizi wa Hadithi katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, watafiti anaeleza jinsi usimulizi wa hadithi umeathiriwa na usasa katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda. Anafanya hivyo kwa kulinganisha hali ilivyo sasa na j...
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza namna ambavyo Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa kwa nchi ya Uganda. Ni kweli kwamba nchini Uganda, watu kadhaa wakiwemo baadhi ya wanasiasa ha...
Athari ya Uraibu wa Dawa za Kulevya katika Jamii kupitia Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni
Athari ya Uraibu wa Dawa za Kulevya katika Jamii kupitia Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni
Kiswahili Suala la dawa za kulevya ni mojawapo ya masuala ibuka lenye athari kubwa katika jamii huku mtandao ukichangia hali hii. Makala haya yalichunguza madhara yake yalivyosawir...

Back to Top